taarifa kwa umma

Mar 2, 2011
86
29
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu wanatakiwa kuwa makini na taarifa zao kwa umma.

1.Kuepuka makosa ya kisarufu na uandishi katika Kiswahili
rejea aya ya tatu sentensi ya pili wameanza na kiunganishi "Na" jamani katika Kiswahili hakuna tungo huru wala tegemezi inayoweza kuanza na kiunganishi hicho.
Ngoja niwarudishe shule.
Matumizi ya NA
i.Kuunganisha neno na neno.
mfano -Mkapa na Kikwete.
ii.Kuunganisha tungo na tungo iwe huru au la.
Mfano –Rais Kikwete anaongoza nchi yetu na Mkapa aliongoza nchi yetu.
Muhimu - Kiunganishi NA hakianzi mwanzoni mwa tungo.

2.Kuepuka matumizi ya lugha kavu.
Mfano neno Upuuzi katika aya ya pili sentensi ya kwanza na neno la mwisho.
Tafsiri yake ni kwamba-Ni jambo la kijinga, la kishenzi au lisilo na maana.
Sentensi sahihi ilikuwa ni Kauli hii ya Bwana Lema si ya kweli(ondoa neno Upuuzi).
Muhimu. lugha ya Kiswahili ina desturi zake, kubwa matumzi ya tafsida.

3.Kwa uandishi wa taarifa kwa umma mwandishi anapashwa kuepuka ushabiki (unatakiwa kuwa kati katika mizani) na taarifa inapaswa kuwa fupi ya maneno machache.

4.Kuepuka makosa ya kimantiki
Mfano. Ikulu haipaswi kuisemea Mahakama au kumsemea Jaji Gabriel Rwakibalira lakini mnalo jukumu la kuisemea Ikulu.

5.Kukwepa matumizi ya ubunge kama mtu, ubunge ni jamii- anapigiwa kura na watu wanampa ridhaa ya kuwa mbunge kwa hiyo panapotokea lolote lile iwe kifo, maamuzi ya mahakama, kuachia ngazi aú lingine hatusemi ni la mbunge au Lema au Sumari au Makwega, bali jambo hilo ni la wananchi wote.
Sentensi sahihi tunasema, Wananchi wa jimbo la Arusha Mjini hawana mwakilishi kwa sababu ya... (Msiba, maamuzi ya mahakama, ugonjwa n.k)

6.Kukwepa matumizi ya lugha za dini
Aya ya sita sentensi ya kwanza imemaliziwa ...hakuna mtu mwingine wa kumbebesha msalaba.
Hapo msalaba si kwa lema kukosa ubunge bali wananchi wa jimbo la Arusha Mjini kukosa mwakilishi wao Bungeni. Hilo linaweza kusababisha watu wengine kumbebea huo msalaba.

Muhimu.
Taarifa kama hii inawapa nafasi umma kuhuzunika pamoja na yule anayetajwa katika jambo hilo wakati dhumuni lake lilikuwa na kuondoa utata.
Tuwe makini.
 
Binafsi nimefurahishwa na namna unavyoelekeza matumizi sahihi ya misamiati ya kiswahili pamoja tungo pia aina mbalimbali hata hivyo sitaki kukosoa ujumbe uliotolewa na ikulu.

Kama wewe si mwlimu wa kiswahili basi unafaa sana kuwa mwalimu fungua darasa mkuu tutakuja kujifunza.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Duh Mkuu wangu basi itabidi wawe wanaipeleka Taarifa pale BAKITA kwa Mackey Hassan ili aipitie kabla ya kutolewa. Watanzania wengi hatukijui kiswahili fasaha; tungo huru, tungo tegemezi, kishazi, nk.
 
Rweyemamu ni kama Mzee Yusuph kila kitu anaona ni kama mipasho. Halafu siyo mara ya kwanza kutoa taarifa tata, kuna haja ya kumbadili huyi jamaa na kazi yake hiyo.
 
Tukiambiwa ubora wa elimu yetu umeshuka watu wanakataa,yaani kwa sasa mwanafunzi wa kenya atafanya vizuri katika mtihani wa kiswahili kuliko mtanzania
 
Huo ushauri mpelekee Rostam bosi wake Salva Rweyemam labda ndo atazingatia,kwan hamjui huyu jamaa kazi alopewa haikufuata taratibu za ajira,ilitumwa email kwa mnene akiagizwa ampe kazi Salva nae akaitikia,haya ni matokeo ya kazi za vimemo!
 
nimeikubali hoja yako, tatizo hatuangalii ubora ila undugu na uccm katika kupeana kazi.
 
Ndugu mimi nakubaliana na wewe lakini kwa ikulu hii yetu uandishi wa kishabiki, kiupendeleo na kinafiki katika taarifa ambazo zinatarajiwa kuwa za umma ni jambo la kawaida.

Sijui nani kawaloga ila zao zinahesabika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom