Mtwara reli itapekeka nini weweMh. Zitto hongera kwa vipaumbele vinavyolenga kutukomboa kutoka katika hali hii ngumu ya maisha. Hata hivyo nina maswali machache:
- Nasikia Mtwara kulikuwa na reli je, kwanini bajeti yenu haikuigusa hiyo reli
- Kushinikiza kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma sio kipaumbele chenu? Hamuoni umuhimu wa hili?
- (Wadau) naombeni elimu kidogo ya kitu hiki tozo za development skills. Pia ni kwanini wakatwe watumishi wa serikali na mashirika ya umma tu?
Vinginevyo vimesimama imara kwa maoni yangu