Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,277
- 9,912
Nimefarijika sana kwa maelezo yako yakumtia moyo kijana jasiri ,mwenyekudhubutu na mpambanaji LEMA.Nafarijika nikiwa Muasisi wa Chadema na Mwenyekiti Taifa wa kwanza, (mstaafu) kwamba Mhe. Godbless Lema ameonyesha ujasiri thabiti katika kupinga uonevu wa wanyonge na ukandamizaji wa demokrasia unaoonekana kuidhinishwa na Serikali ya nchi yetu. Mhe. Lema ameonyesha uzalendo uliotoka moyoni na kujitolea kwake kutumikia umma. Mungu atambariki na kumlinda.
Tamko lake kwa waandishi wa habari lime-cover kikamilifu misimamo ya CHADEMA kama ninavyoielewa na kuiamini, na nina hakika Kamati Kuu ya Chama itaridhia.
Hata hivyo, nionavyo mimi binafsi, Tanzania tunaelekea njia inayohatarisha amani na uhuru wa watu wetu; hasa pale Polisi wanapojiingiza kutekeleza maagizo ya chama tawala na kupindisha sheria na taratibu tulizojiwekea na zinazohakikisha kwamba Mahakama zinakuwa na uhuru kamili kuamua kesi zilizo mbele yao.
Kwa maoni yangu, vituko vya Arusha kuhusu Chadema na maagizo kwa Polisi yanayoashiria kwamba yana baraka za Serikali, yanastahili kujadiliwa na viongozi tuliwachagua, na tamko kutolewa kuhusu uhuru wa wanachama kuandamana na kukutana. 'ROLE' ya Polisi katika shughuli za vyama vya siasa ni lazima ifafanuliwe kama uongozi unadhamiria kwa dhati kudumisha amani.
Ni mfano wa vijana wachache ambao wana udhubutu wa namna ya Lema. Ikiwa vijana tukasimama tukapinga kwa nguvu udhalimu huu unaendelea kukuwa siku hadi siku wa ukandamizaji unaofanywa na polisi naamini tutashinda lakini muhimu zaidi tutakuwa tumetimiza wajibu wetu kama vijana wazalendo.
Big up Lema, Viva CDM.