[h=1][/h]
Katika Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe 10 Agosti 2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye maana kuwa Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu.
Katika habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo kufuatia ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa benki na utawala bora.
Benki Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama zilivyo benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufanya biashara na benki hii kama kawaida.
IMETOLEWA NA BENKI KUU YA TANZANIA11AUGUST 2012
Nasikia kuna jamaa walitoka Vodacom kuhamia hapo ndo wamepiga sana dili hapo NBC, ila inarudisha sana nyuma imani kwa vijana!Mkurugenzi alikuwa anatoa mikopo kama njugu kuna watu wengi sana wamechukuwa mikopo ya milioni 100 wametoa 10% hawa ndio wasomi wetu tunaojitapa nao kila siku humu JF.
Ni kweli kusimamishwa kwa Mafuru kumetokana na matatuzo lakini hiyo haimaanishi kwa BoT imechukua operations xa hiyo benki. Inapofikia Central Bank kuweka operations za bank chini yake lazima hali ingejionyesha dhahiri na nadhani BoT huwa haifanyi taarifa hizo kuwa siri. Hao watu wa Business Times wanapaswa kuweka ushahidi wa taariya yaoHuenda kuna shida huko
NBC. Masuala ya kibenki ni very sensitive hivyo BOT wanakanusha hata
kama kutakuwa na shida iwe kimya kimya kuepuka piblic punic.Nadhani
wangetuambia sababu ya Mafuru kusimamishwa na ni nani anaongoza NBC.
Uongozi katika masuala ya kibenki ni muhimu sana hivyo kuondolewa kwa
CEO kunaashiria kuwa mambo si shwari hapo NBC.
Ninachojua NBC ilinunuliwa na Baclays so haya yote ni njama za Baclays kuonyesha kuwa wazawa hatuwezi kumeneji na ndo maana wamempiga cHin mshikaj ili mzungu atake over. Sku c nyingi utackia mzungu ndo kachukua nafasi. NBC ilikua inafanya vizuri sana basi tu hawa wenzetu wana strategy za kufa mtu
Mkuu Kiranga BOT wanasimamia mabenki yote. Akiondoka CEO lazima BOT wajue kaondoka kwa sababu gani na hata anayeingia lazima lazima apate baraka za BOT.Hivyo nadhani BOT wako well informed kuhusu matatizo ya NBC na hasa sababu ya kuondolewa kwa CEO. Hivyo basi hawatakiwi tu kukanusha wanatakiwa waende mbele kidogo na kutuambia kidogo kuhusu sababu ya CEO kuondolewa ili public isiwe na mashaka kuhusu akiba zao.
Mkuu Kiranga kuna hii kitu inaitwa CAMEL ambayo hutumika katika ku assess banks. CAMEL -Capital, Assets, Management, Earnings and Liquidity. Hivyo vitu vinatakiwa vibalance kwa namna fulani. Sasa hapo NBC kuna tatizo la MAnagement basi hii inaonyesha kwamba hiyo CAMEL haiko vyema hata kidogo. Ni muhimu ikaangaliwa kwa jicho la tatu. Naamini kuwa kwa sasa BOT haiko Directly kwenye ku manage NBC lakini kukiwa na tatizo la kiuongozi katika commercial bank ama financial institution yoyote inayopokea amana za wananchi basi haraka Central Bank yoyote lazima iwe makini sana na mwenendo wa hiyo bank. Naamini pia kwamba BOT wako makini juu ya kadhia hii ya kiuongozi pale NBC
Ndio mkuu tulikuwa nae Kombania mojaAlienda hadi JKT Unajua...
Mkurugenzi alikuwa anatoa mikopo kama njugu kuna watu wengi sana wamechukuwa mikopo ya milioni 100 wametoa 10% hawa ndio wasomi wetu tunaojitapa nao kila siku humu JF.
Huenda kuna shida huko NBC. Masuala ya kibenki ni very sensitive hivyo BOT wanakanusha hata kama kutakuwa na shida iwe kimya kimya kuepuka piblic punic.Nadhani wangetuambia sababu ya Mafuru kusimamishwa na ni nani anaongoza NBC. Uongozi katika masuala ya kibenki ni muhimu sana hivyo kuondolewa kwa CEO kunaashiria kuwa mambo si shwari hapo NBC.
Business Times inabidi ije na taarifa ya kukanusha, manake wanafanya sasa hata baadhi ya wateja hawaamini hiyo taarifa ya kutoka BOT, kwa habari ambazo sijazidhibitisha ni kuwa BOT wanafanya special review ya NBC ila hawataki wateja wajue, kuna shida sana ya hawa janaa wakaburu na repatriation of income katika services za ICT wanazotoa kwa NBC. Tusubiri tuone mwisho wa hii saga!