Taarifa kwa umma kuhusu kusitishwa kwa fao la kujitoa

elimsu

Member
Aug 27, 2010
31
3
Je hii ni sawa? yeyote mwenye hiyo sheria iliyotumika kusetisha fao la kujitoa airushe hapa JF pliz

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU KUSITISHWA KWA FAO LA KUJITOA


Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda kutoa ufafanuzi juu ya mafao ya kujitoa. Ufanunuzi huu unakwenda sambamba na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya habari na kuleta mkanganyiko miongoni mwa Wanachama na Wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Kufuatia hali hiyo, Mamlaka inatoa ufafanuzi ufuatao:


  • Marekebisho kuhusu kusitisha fao la kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa Mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu hali ya maisha uzeeni.
  • Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho. Mchakato wa marekebisho hayo ulihusisha wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi kutoka Vyama vya Wafanyakazi, Chama cha waajiri pamoja na Serikali.
  • Kwa kutambua tofauti ya ajira, tofauti ya mazingira ya kazi, tofauti ya sababu za ukomo wa ajira, na umuhimu wa Mwanachama kunufaika na michango yake wakati angali katika ajira, Mamlaka inaendelea na mchakato wa kuandaa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni kuboresha maslahi ya Wanachama. Miongozo na kanuni hizo zitajadiliwa na Wadau wakiwemo Wafanyakazi, Waajiri na Serikali kabla ya kuanza kutumika.
  • Kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa Wadau.
  • Tangazo hili halitowahusu Wanachama waonachangia katika Mfuko wa Akiba (GEPF), Mifuko ya Hiari (Supplementary Schemes) zinazoendeshwa na PPF,NSSF na LAPF, pia Wanachama waliojitoa kabla ya tarehe 20/07/2012.
  • Mamlaka inakanusha vikali kwamba, sitisho la fao la kujitoa si kwa sababu za Kiserikali au kwa sababu Mifuko imefilisika. Tunapenda kuwahakikishia kwamba Mifuko yote ipo thabiti na michango yote ya Wanachama ipo salama.
  • Hivyo, Mamlaka inawaomba Wanachama na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu wakati mchakato huu ukiendelea kwa lengo la kulinda na kutetea maslahi ya Mwanachama.
  • Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji

SSRA-Makao Makuu
 

Attachments

  • TAARIFA-KWA-UMMA.pdf
    216.8 KB · Views: 239
Huo utetezi bado haujaniingia akilini.... Yani niache kazi au nifukuzwe kazi afu nisubirie mafao yangu baada ya kuzeeka? Kipindi chote kingine ntaishi vipi? Si afadhali nipewe kabisa ili niizungushe mwenyewe kibiashara? Kuna umuhimu wa kuikataa hiyo sheria
 
wanazidi kutoa matamko ya kutukandamiza kwa sababu hadi sasa hatujachukua hatua yeyote ya kuwastua zaidi tu ya kulalalmika ovyo.
 
Hao wameanzisha SSRA ya kipuuuzi kabisa wameshindwa kubuni jinsi gani kupata pesa za kuchezea wanasiasa,yaani mimi wasiniambie lolote!!
 
watatoa sana mataarifa kwa umma... na ukishaona hivi ujue walifeli zoezi la kwanza la kuuweka umma sawa na sheria zao wanazoandikia makwapani
 
Hawana lolote zaidi ya kuchochea moto!! ndiyo maana malawi wanataka ziwa nyasa lote liwe lao sababu makachero wao walishaona kuna dalili za kulipata lote kwani hatuna vichwa vinavyojali maslahi ya nchi na wananchi kwa ujumla.
 
Hii sheria ya kusubiri hadi ufikishe miaka 55 au 60 ndiyo uchukue mafao ya pensheni inawezakana tu kwa nchi zilizoendelea, sio kwa nchi kama Tanzania.

Nchi zilizoendelea mtu anapoachishwa au kufukuzwa kazi, serikali humpatia pesa kiasi fulani ya kujikimu wakati ambao anakuwa anatafuta kazi. Ataendelea kugharamikiwa na serikali hadi siku atakayopata kazi nyingine. Hili Tanzania halifanyiki hivyo sheria hii inaonekana NULL AND VOID.

Pili nchi zilizoendelea inflation ni ndogo sana, lakini kwa nchi kama TZ amabyo inflation ina stand 20%, Thamani ya pesa ya 2012 haitakuwa sawa na miaka 20 ijayo i.e 2013, hivyo kuifanya sheria hii kuwa NULL AND VOID.

Huyu Irene Isack hakufanya utafiti wa kutosha amekwenda Denmark na Sweeden na ku copy sheria za huko na kuzi paste hapa Tanzania bila kuangalia mazingira ya Tanzania, kama nilivyoyataja hapo juu including life expectancy ya Mtanzania ambayo ina stand 46 yrs for male and 48 yrs for female.
 
Je hii ni sawa? yeyote mwenye hiyo sheria iliyotumika kusetisha fao la kujitoa airushe hapa JF pliz

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU KUSITISHWA KWA FAO LA KUJITOA


Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda kutoa ufafanuzi juu ya mafao ya kujitoa. Ufanunuzi huu unakwenda sambamba na taarifa mbalimbali ambazo .................................
SSRA-Makao Makuu

SSRA acheni kutoa taarifa na matamko kuhusu swala hili.
Swala hili tayari lina kesi mahakanai, kesi iliyofunguliwa na vyama vya wafanyakazi.
Hivyo SSRA kwa kutoa taarifa na matamko, mnaingilia swala ambalo tayari liko mahakamani.
 
Shame on you na matamko yenu ya kifedhuli na kifisadi hayo. Maisha mazuri nayaanda mimi mwenyewe nikiwa na nguvu zangu na sio kuanza kuyatafuta uzeeni. Mmeshazoea kutupeleka peleka kama magari mabovu enzi zile mnadhani na zama hizi mtafanya hivyo hivyo tuwaangalie tu.............imekula kwenu, tunataka pesa zetu tu na si vinginevyo.
 
Jamani, je sheria hii inawabana na walioitunga yaani wabunge? na wao hawatachukua mafao yao mpaka wafikishe umri wa kustaafu? Na kwanini sheria hii inarudi nyuma badala ya kuanza na wanachama wanaojiunga leo yenyewe inawachukua hata waliojiunga miaka ya 80. Kwanini? Tetesi kwamba hali ya kiuchumi ya mifuko hii pamoja na serikali kukopa toka kwenye mifuko na kujengea UDOM etc huenda zinaukweli.
 
Je hii ni sawa? yeyote mwenye hiyo sheria iliyotumika kusetisha fao la kujitoa airushe hapa JF pliz
TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU KUSITISHWA KWA FAO LA KUJITOA



  • Mamlaka inakanusha vikali kwamba, sitisho la fao la kujitoa si kwa sababu za Kiserikali au kwa sababu Mifuko imefilisika. Tunapenda kuwahakikishia kwamba Mifuko yote ipo thabiti na michango yote ya Wanachama ipo salama.
  • Hivyo, Mamlaka inawaomba Wanachama na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu wakati mchakato huu ukiendelea kwa lengo la kulinda na kutetea maslahi ya Mwanachama.
  • Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji.
  • SSRA-Makao Makuu
  • wanazidi kutoa matamko ya kutukandamiza kwa sababu hadi sasa hatujachukua hatua yeyote ya kuwastua zaidi tu ya kulalalmika ovyo.
    hapa ndio unaweza kujua hii nchi ni ya kuongozwa ma mmatukio kwa kiasi gani, kila kitu ni kusikilizia tu na ku-assume kuwa 'ni upepo tu utapita'.

Kama kweli hawa SSRA wako makini kwani nini waliiitwa kwenye debate nzuri pale Channel Ten wakakwepa kwenda, hata jana Radio 1 kipindi cha jioni (alikuwepo Mzee Mkinga) wamekwepa kwenda alafu watushawishi na haya 'matamko' kuwa wana uwezo! Naamini wangelitokea kwenye hivyo vipindi walivyosema na vinginevyo interactions zingekuwa kubwa na watanzania wangelielewa uongo wao lakini waliogopa.

Hapo kwenye red wanataka kumdanganya nani maana taariza zipo kwenye majumuisho ya Mkaguzi Mkuu wa Serikari - CAG!

Kwa wale wenye nia njema na nchi hii tukubaliane tu kuwa hii taasisi kiutendaji iko chini sana hata kama ni kutumiwa kisiasa. Ukitaka kuamini hili angalia ata ofisi zao zilipo alafu ufanye tu tafakari ndogo.

 
Hawa watu hawako serious kabisa.........hata website yao imejaa mapicha ya IRENE as if ni FACEBOOK

ssra6.jpg


Informing media houses during a press conference held at SSRA Board Room the Director General Ms. Irene Isaka informed journalists that as per Section No.5d of the SSRAAct, one of the roles and functions of the Authority is to protect and safeguard the interests of members, while making sure that all social security schemes are strong and sustainable. "The guideline addresses the immediate and some of the intermediate actions that are needed to improve the governance of investments and investments returns" said the Director General.
 
Huo ni upuuzi kabisa!Nani amewambia hayo mafao yatakuwa bora uzeeni wakati hela kila siku inaporomoka thamani?Hawa watu sidhani hata kama shule walifaulu kwa ubongo wao!
 
Hao wameanzisha SSRA ya kipuuuzi kabisa wameshindwa kubuni jinsi gani kupata pesa za kuchezea wanasiasa,yaani mimi wasiniambie lolote!!

Wengine humu waoga mkuu tutafutane washikaji kama mia hivi tukawapetimbwili pale makao makuu hili suala serikali inatutania kabisa yaani mkuu haliwezekani iache kucheza na pesa zetu kabisa.
 
Wengine humu waoga mkuu tutafutane washikaji kama mia hivi tukawapetimbwili pale makao makuu hili suala serikali inatutania kabisa yaani mkuu haliwezekani iache kucheza na pesa zetu kabisa.

Upo katika mpango wa kustaafu soon nini?
 
Huo utetezi bado haujaniingia akilini.... Yani niache kazi au nifukuzwe kazi afu nisubirie mafao yangu baada ya kuzeeka? Kipindi chote kingine ntaishi vipi? Si afadhali nipewe kabisa ili niizungushe mwenyewe kibiashara? Kuna umuhimu wa kuikataa hiyo sheria

eehh, wanakusubiria ukizeeka ni rahisi kukuzurumu kwa kukumwagia maji ya pilipili kama wazee wa iliyokuwa East Africa
 
Hawa watu hawako serious kabisa.........hata website yao imejaa mapicha ya IRENE as if ni FACEBOOK

ssra6.jpg


Informing media houses during a press conference held at SSRA Board Room the Director General Ms. Irene Isaka informed journalists that as per Section No.5d of the SSRAAct, one of the roles and functions of the Authority is to protect and safeguard the interests of members, while making sure that all social security schemes are strong and sustainable. “The guideline addresses the immediate and some of the intermediate actions that are needed to improve the governance of investments and investments returns” said the Director General.

Hawa wanacheza na maisha yetu ngoja.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom