Taarifa Kwa CCM na Serikali yake.

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
553
Napenda kutoa ufafanuzi wa mambo hapa ili kia Wilium Marecela na wenzake watuelewe sisi watanzania wazalendo.

1. Tumechoshwa sana na matatizo ambayo hayaishi kila kukicha, mfano issue ya mgawo wa umeme nafikiri imefika mahali mimi binafsi na hata wananchi hatutaki kusikia kiongozi yeyote wa CCM au wa Serikali hii ya CCM anatuhadaa kwa namna yeyote ile. Nimeona mipango na mikakati mingi ambayo aliitoa Ngeleja eti itakamilika 2013/2014 kuhusu swala la umeme, inamaana tutakuwa gizani hadi muda huo? Haiwezekani hii ni janja ya CCM na serikali yake kuwahadaa watanzania ukweli ni kwamba tangu awamu ya pili, tatu na sasa CCM na viongozi wake waliliyafanya matatizo ya umeme kama mtaji wao, angalia IPTL, Songas, Richmond/Dowans/Symbion na sasa yamewashinda tunataka umeme kama imeshindikana waondoke madarakani kabla ya 2015.

2. Tuje kwenye Madini, Gesi asilia, Mafuta ghafi, Utalii etc. Inashangaza kuona huwa hizi pesa sijui zinakwenda wapi, lakini madini yanaisha, wanayama wanabebawa kama shamba la bibi, na majuzi tulisikia wamarekani wanakuja kuchukua uranium kwa watanzania kupewa vyandarua hivi kweli malaria inatuuwa kwa kiwango cha kuwapa Uranium nasi kupewa vyandarua? kama ndiyo ni bora tufe kwa malaria na watakaobaki watumie madini hayo kwa mambo mengine pamoja na kuboresha hospitali na kuongeza idadi ya madaktari. Huu ni usanii wa hali ya juu.
Mimi nataka kujua hela zinazotokana na madini, utalii, Gesi asilia tujue kiasi chake ili tujue inaendaga wapi?

3. Hawa CCM wanafikiri watanzania watakuwa kimya hivi hadi lini? maana siku hizi hadi sehemu za kazi tujikuta hadi wageni wananguvu kubwa hadi imefika viongozi wetu wanawaunga mkono kwa kiasi cha kutuambia eti watanzania hatuwezi kazi, mimi nafikiri si kweli kwamba watanzania hatuezi kufanya kazi bali ni viongozi wetu kutokuwa wazalendo tu. huwezi kumleta mhindi mwenye diploma akaja kufundisha university wakati kuna watanzania wana hadi masters, huu ni uhuni wa viongozi. To be honest viongozi wetu wengi ni vibaraka ndio maana wapo mstari wa mbele kuwatetea wachina, wahindi, waarabu na wazungu eti kwa kuwa wanaweza kufanya kazi. Swali langu kubwa ni Mbona IPP Media, CRDB etc zipo chini ya watanzania na zinafanya vizuri? kwa nini makampuni haya tena madogo yanawaleta wageni wengi?

Mwisho watanzania tutumie nguvu ya Umma katika kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu kwa manufaa ya baadae.
 
Kipimo cha uanadamu ni kutothamini uhai wako pale ambapo maisha yako hayana maana, watanzania tumekaribia kukosa hiyo sifa kwani tunafurahi mahali tunapotakiwa kulia na tunashangilia mahali ambpo tulitakiwa kulaani, tunalinda na kukingia kifua mahali ambapo tulitakiwa kukamata na kupeleka jela kazi kwelikweli.
 
Back
Top Bottom