TAARIFA juu ya maombi ya CCM kuwa Dkt. Willibrod Slaa awanie ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki

Sikuona umuhimu wa CDM kumjibu Nepi. Haina maana,wangempotezea.

CCM wana mipango mibaya dhidi ya CDM. Chondechonde NAOMBA Dr. SLAA asigombee kiti chochote cha Ubunge kipindi hiki. Akigombea CCM yata iba kura na kutangaza matokeo feki ili kumdhalilisha Dr. Mh. Rais wa Tanzania wa 2015.
 
Hivi huyu Makene ameenda shule kweli? mbona anamawazo ya kipumbavu namna hii? kwamba nafasi ya ubunge ni hadhi ndogo kwa Dr. Slaa ?! Kivipi? kwa vile alishagombea urais? Vipi Kuhusu Kamanda Mbowe? Makene umeonyesha usivyo na akili sawawasa hufai kushika nafasi hiyo katika chama. Kwani ilikuwa razima ujibu kila wanachosema CCM? Mbona unakuwa na akili kama ya Makamba?

Kwakawaida mtu mwenye kuelewa hawezi kupendekeza Dr. Slaa agombee mbunge kwa sasa hata kama ushindi ungelikuwa ni 100%. CHADEMA haiwezi kupeleka machine zake zote bungeni ikawa na ufanisi ilionao sasa. Pili, Dr. Slaa kugombea ubunge laweza kutafsiriwa kama uchu wa madaraka kitu ambacho si vyema. Hasara za Dr. Slaa kugombea ubunge ni kubwa sana kwa CHADEMA na kwakwe pia.

Namlaumu John Mnyika kwa kudelegate madaraka kwa Makene atoe tamko bila yeye Mnyika Kulifanyia uhariri. Kama CHADEMA waliona kuna umuhimu wa kusemea propaganda ya Nape walipaswa kuwa makini sana na si kukurupuka.

Nionavyo mimi MAKENE ametengeneza mgogoro usio walazima kati ya wabunge wetu na Dr. Slaa.
 
he!.....................kumbe Dr. slaa alishakuwa mgombea urais wa kudumu wa chadema??.................. mie sikulijua hili!!.................. mnarudia yaleyaleee...................

halafu si vyema chama kuwa na dharau namna hii..................... nani kasema ubunge ni kazi ndogo na duni sana kiasi ambacho ni aibu mtu kama slaa kuifanya??................... kwa hiyo slaa sasa ni superior kwa wabunge wote?................. hivi mnajua kuwa hata rais kibaki na odinga wa kenya ni wabunge mpaka sasa?................ so slaa yuko kwenye viwango vya juu hata ya kibaki na raila??................... hebu acheni kudharau kazi ya ubunge na wabunge wetu................. tumhwshimu kila mtu na kazi aifanyayo kwa maslahi ya taifa tafadhari...............

mtaharibu chama chenu sasa na hii kasi ya kumjibu kila mtu chochote asemacho....................... mingine ni mitego tu, msiwe mnajibu.................. ni ushauri tu wakuu.......................
mkuu katika matamko yote yaliyowahi kutolewa hilo ni tamko la hovyo na chovu kuliko yote. Limejaa kejeri na majigambo! Tamko linadhihirisha kwamba sasa CDM ina mgombea wa kudumu wa Urais, limeziba mianya yoote ya watu kujitokeza kugombea Urais ndani ya CDM. Linawakejeri wabunge akiwemo Mwenyekiti wa CDM! Linaonyesha kuwa ubunge ni kazi ya watu ambao hawawezi kugombea Urais huku likisahau kuwa wabunge ndio wanaunda serikali kupitia Baraza la Mawaziri.

Mods iondoeni hii thread manake inaonyesha jinsi chama chetu kisivyo na viongozi makini na pia inaonyesha kwamba ndani ya Chama kuna virusi vya udikteta.
 
Huo ndio msimamo wa mambo, ubunge sii kitu! Kama ubunge ungekua na maana Kwanini Tanzania tuna sheria mbovu? Na hizo sheria mbovu zimetungwa na bunge? Ubunge sii kitu kama bunge linalotokana na ubunge linashindwa kuiwajibisha serikali hilo ni bunge? Kazi ya bunge nini? Kwanini bunge linaitetea serikali ilehali bunge linapaswa kuiwajibisha serikali? Kwanini Sisi watanzania tunakua maskini wa fikra(poverty mentality)? Unahitaji kwenda shule ili ujue ubora wa bunge letu? Je kama wabunge wangekua wanalipwa mishahara kutokana na taaluma zao watu wangekimbilia kuwania ubunge? Umaskini na uroho /uchu wa pesa ndio unaomfanya mtu akimbilie kuwania ubunge kanakwamba ubunge ndio solution ya umaskini! Na pia Dkt Slaa hatagombea ubunge kwa kigezo eti yeye ni mgombea wa kudumu wa urais hapana Dkt yupo kwa ajili ya kuwafunda vijana ndani ya chama wawe kama yeye, watambue u muhimu wa maslahi ya taifa kwanza na pia umuhimu wa kutoa haki kwa mtanzania wa leo na kesho! Dkt yupo ajili ya CHADEMA na watanzania kwa ujumla na sio kwa ajili ya urais!

Unashindwa kuelewa ni kwa vipi CHADEMA itakamata dola bila kuwa na wabunge wakutosha? ilikuwa ni muhimu sana kwa CDM kujikita katika majimbo kwanza.
 
Hivi huyu Makene ameenda shule kweli? mbona anamawazo ya kipumbavu namna hii? kwamba nafasi ya ubunge ni hadhi ndogo kwa Dr. Slaa ?! Kivipi? kwa vile alishagombea urais? Vipi Kuhusu Kamanda Mbowe? Makene umeonyesha usivyo na akili sawawasa hufai kushika nafasi hiyo katika chama. Kwani ilikuwa razima ujibu kila wanachosema CCM? Mbona unakuwa na akili kama ya Makamba?

Kwakawaida mtu mwenye kuelewa hawezi kupendekeza Dr. Slaa agombee mbunge kwa sasa hata kama ushindi ungelikuwa ni 100%. CHADEMA haiwezi kupeleka machine zake zote bungeni ikawa na ufanisi ilionao sasa. Pili, Dr. Slaa kugombea ubunge laweza kutafsiriwa kama uchu wa madaraka kitu ambacho si vyema. Hasara za Dr. Slaa kugombea ubunge ni kubwa sana kwa CHADEMA na kwakwe pia.

Namlaumu John Mnyika kwa kudelegate madaraka kwa Makene atoe tamko bila yeye Mnyika Kulifanyia uhariri. Kama CHADEMA waliona kuna umuhimu wa kusemea propaganda ya Nape walipaswa kuwa makini sana na si kukurupuka.

Nionavyo mimi MAKENE ametengeneza mgogoro usio walazima kati ya wabunge wetu na Dr. Slaa.
Mgema ukimsifia, tembo hulitia maji!
 
Dr. Slaa is a presidential material elewa.
 
TAARIFA K
WA VYOMBO VYA HABARI

KURUGENZI ya Habari na Uenezi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inapenda kutoa taarifa kuhusu habari zilizoripotiwa kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, juu ya maombi ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinafanya usiku na mchana ili eti Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, agombee ubunge, kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Jimbo la Arumeru Mashariki, Aprili 1, 2012.

Ingawa haijajulikana maombi hayo yanafanyika msikiti upi au kanisa lipi au sehemu ipi yoyote ile nyingine ya kufanyia maombi, Kurugenzi imeshangazwa sana na mantiki ya kuwepo kwa maombi hayo ya CCM yakionesha upendo wa kutiliwa mashaka kuwa chama hicho kimefikia mahali kinaweza kufanyia maombi vyama vingine ili vipate wagombea makini wa kukibwaga vibaya sana katika uchaguzi.

Kurugenzi inapenda kusema yafuatayo juu ya maombi hayo ya CCM, ambayo kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, kama ilivyoripotiwa katika njia mbalimbali za upashanaji habari, imedhihirika dhahiri kuwa ni maombi yanayoongozwa zaidi na hila, husuda kwa CHADEMA na Katibu Mkuu wake, Dkt. Slaa;

Tunapenda CCM wajue kuwa CHADEMA na viongozi wake makini, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa, si watu wa kurudi nyuma. Chama hiki daima muda wote kinapanga mikakati na mipango ya kusonga mbele, kikionesha utawala mbadala, kikijiandaa kushika dola na kutekeleza malengo ya Watanzania!

Kwa mantiki hiyo, chama hiki hakiwezi kurudi nyuma, hakiwezi kumrudisha nyuma Katibu Mkuu wake, Dkt. Slaa kuwania ubunge. Kiongozi huyu makini, ambaye umma wa Watanzania una imani kubwa naye, ameshavuka viwango vya ubunge, si mtu wa kuwania nafasi ya ubunge tena, (is not parliamentary material).

Kwa nafasi yake ndani ya CHADEMA, anao wajibu mkubwa kujenga chama. Kwa kutimiza wajibu huo, Dkt. Slaa anafanya kazi ya kutengeneza na kuivisha watu wengine makini zaidi, kuweza kuwa viongozi ndani ya chama, nafasi za udiwani na ubunge, ili kuendeleza umakini na uimara wa chama hiki ambacho dhahiri ni tumaini jipya la Watanzania katika kutoa uongozi mbadala wa nchi.

Kwa umakini wa CHADEMA, uwezo wa Dkt. Slaa na matumaini makubwa ya Watanzania, ambayo wameendelea kuyaonesha kwa chama hiki tangu mwaka 2007, kilipoanzisha rasmi mapambano dhidi ya ufisadi na mafisadi, kisha kudhihirika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, nafasi pekee inayomstahili Dkt. Slaa ni urais kwa maana ya kuwa ni ‘presidential material’, si ubunge.

Lakini pia, tunatambua kuwa CCM, wameweza kutoa kauli hiyo ya kukurupuka baada ya Dkt. Slaa kuwa tayari ametamka wazi tangu awali na kurudia kauli yake thabiti mara kadhaa kuwa hana nia wala mpango wa kuwania ubunge mahali popote pale nchini. Hawezi kufanya hivyo kwani hata ubunge wa Karatu hakushindwa bali aliacha mwenyewe kwa hiari yake, ili kutekeleza mahitaji ya umma wa Watanzania.

Kurugenzi ya Habari na Uenezi inatumia nafasi hii kuwaambia CCM kuwa watambue CHADEMA ni chama makini. Kimedhihirisha hivyo mara kadhaa katika masuala makubwa kwa maslahi ya Watanzania. Kitaendelea kudhihirisha hivyo pia katika uchaguzi wa Arumeru kwani kina utaratibu wa kuwapata wagombea wake, kutokana na maamuzi ya wanachama wake.

Tunatambua kuwa kauli hiyo ya CCM pia ni sehemu ya mkakati wa makusudi kuwakatisha tamaa baadhi ya watu wanaotaka kugombea jimbo hilo kupitia CHADEMA. Kurugenzi ya Habari na Uenezi inapenda kusisitiza taarifa ya awali, kuwataka wanachama wetu wajitokeze kwa wingi kuwania uteuzi wa kugombea ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.

Tunataka CCM wajue kuwa suala la kuteua mgombea wa CHADEMA ni la CHADEMA yenyewe, kwa kutumia utaratibu wake, ikiongozwa na katiba, kanuni na mahitaji ya umma, wala hatuhitaji ushauri wa chama ambacho kadri siku zinavyokwenda, kinadhihirisha kila dalili ya kuchoka kujisimamia chenyewe, kusimamia wanachama wake, kusimamia serikali na maendeleo ya watu, hivyo kupoteza kabisa ushawishi kwa wananchi. Wala hatujawahi kuomba ushauri kutoka kwao hata siku moja.

Lakini maombi hayo ya CCM, kama ambavyo Nape amenukuliwa katika vyombo vya habari akisema, yamedhihirisha namna ambavyo chama hicho bado kinaandamwa na mzimu wa CHADEMA na Dkt. Slaa tangu baada ya uchaguzi mkuu, kwa kuiba kura na kuvuruga matokeo ya uchaguzi huo.

Kauli ya Nape kuwa iwapo maombi yao yatafanikiwa na Dkt. Slaa akawania ubunge, CCM watakuwa wamemaliza kazi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, inathibitisha tuhuma hizo na namna ambavyo CCM hakikushinda kwa haki uchaguzi huo.

Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya pia inataka CCM waelewe kuwa umaarufu wa CHADEMA hautokani na umaarufu wa mtu mmoja mmoja wala hausubiri matukio pekee, bali unatokana na uongozi makini, kuanzia ngazi ya taifa hadi ya msingi, kikijikita katika kusimamia masuala yenye maslahi kwa Watanzania na nchi yao muda wote!

Imetolewa leo Februari 18, 2012, Dar es Salaam na

Tumaini Makene
Afisa Habari wa CHADEMA

Tumaini umetimiza wajibu wako na hupaswi kulaumiwa kulingana na uwezo wako mdogo. Ni dhahiri kwako chama sasa ni ushabiki na kusahau mantiki ya nini maana ya kushika dola!

Taarifa hii haikuathiri chochote kwa CCM wala kwa Wananchi unaohisi ni muhimu kupata taarifa hizi, labda utumie gari la matangazo huko Arumeru na wala si hapa JF.

''Presidential material'' what do you mean? Kabisa kwa majigambo mfu umemdharirisha kiongozi wa chama Bw. Mbowe kwa kugombea ubunge (parliamentary material) baada ya kushindwa urais.Hivi tujiulize Mbowe hakuwa ''presidential material''?.

What if 2015 Dr. Slaa asipopata Urais as a presidential material itakuwaje? Msijihakikishie dola na ushindi wa Urais kwa wabunge 20(majimboni) na toeni Demokrasi ya watu kufikiri kuchukua hata fomu za kugombea Urais ndani ya chama badala ya kujiwekea vijinasaba vya ''parliamentary na presidential material''

Huu ni ulimbukeni utakao wazika mkiona.Shit.

na
 
Hii taarifa naona imekaa kimipasho zaidi, nadhani mtoa taarifa amekurupuka na ninapenda kuamini kuwa Dr. Silaa hajashirikishwa kabla ya kutoa hii taarifa.

Amekurupuka nini? Wewe ndio unaonekana mtu wa mipasho.Hii taarifa imetulia mno na imekuja wakati muafaka
 
Tumaini umetimiza wajibu wako na hupaswi kulaumiwa kulingana na uwezo wako mdogo. Ni dhahiri kwako chama sasa ni ushabiki na kusahau mantiki ya nini maana ya kushika dola!

Taarifa hii haikuathiri chochote kwa CCM wala kwa Wananchi unaohisi ni muhimu kupata taarifa hizi, labda utumie gari la matangazo huko Arumeru na wala si hapa JF.

''Presidential material'' what do you mean? Kabisa kwa majigambo mfu umemdharirisha kiongozi wa chama Bw. Mbowe kwa kugombea ubunge (parliamentary material) baada ya kushindwa urais.Hivi tujiulize Mbowe hakuwa ''presidential material''?.

What if 2015 Dr. Slaa asipopata Urais as a presidential material itakuwaje? Msijihakikishie dola na ushindi wa Urais kwa wabunge 20(majimboni) na toeni Demokrasi ya watu kufikiri kuchukua hata fomu za kugombea Urais ndani ya chama badala ya kujiwekea vijinasaba vya ''parliamentary na presidential material''

Huu ni ulimbukeni utakao wazika mkiona.Shit.

na

Nyie watu wa Magamba mna matatizo sana
 
Hivi huyu Makene ameenda shule kweli? mbona anamawazo ya kipumbavu namna hii? kwamba nafasi ya ubunge ni hadhi ndogo kwa Dr. Slaa ?! Kivipi? kwa vile alishagombea urais? Vipi Kuhusu Kamanda Mbowe? Makene umeonyesha usivyo na akili sawawasa hufai kushika nafasi hiyo katika chama. Kwani ilikuwa razima ujibu kila wanachosema CCM? Mbona unakuwa na akili kama ya Makamba?

Kwakawaida mtu mwenye kuelewa hawezi kupendekeza Dr. Slaa agombee mbunge kwa sasa hata kama ushindi ungelikuwa ni 100%. CHADEMA haiwezi kupeleka machine zake zote bungeni ikawa na ufanisi ilionao sasa. Pili, Dr. Slaa kugombea ubunge laweza kutafsiriwa kama uchu wa madaraka kitu ambacho si vyema. Hasara za Dr. Slaa kugombea ubunge ni kubwa sana kwa CHADEMA na kwakwe pia.

Namlaumu John Mnyika kwa kudelegate madaraka kwa Makene atoe tamko bila yeye Mnyika Kulifanyia uhariri. Kama CHADEMA waliona kuna umuhimu wa kusemea propaganda ya Nape walipaswa kuwa makini sana na si kukurupuka.

Nionavyo mimi MAKENE ametengeneza mgogoro usio walazima kati ya wabunge wetu na Dr. Slaa.

Ukiona nyie watu wa Magamba mnalalamika hivi ni wazi tamko limegusa panapohusika.Hongera Makene keep it up
 
he!.....................kumbe Dr. slaa alishakuwa mgombea urais wa kudumu wa chadema??.................. mie sikulijua hili!!.................. mnarudia yaleyaleee...................

halafu si vyema chama kuwa na dharau namna hii..................... nani kasema ubunge ni kazi ndogo na duni sana kiasi ambacho ni aibu mtu kama slaa kuifanya??................... kwa hiyo slaa sasa ni superior kwa wabunge wote?................. hivi mnajua kuwa hata rais kibaki na odinga wa kenya ni wabunge mpaka sasa?................ so slaa yuko kwenye viwango vya juu hata ya kibaki na raila??................... hebu acheni kudharau kazi ya ubunge na wabunge wetu................. tumhwshimu kila mtu na kazi aifanyayo kwa maslahi ya taifa tafadhari...............

mtaharibu chama chenu sasa na hii kasi ya kumjibu kila mtu chochote asemacho....................... mingine ni mitego tu, msiwe mnajibu.................. ni ushauri tu wakuu.......................

Upende usipende Dr Slaa ni Presidential material.Utake Usitake Dr Slaa atagombea urais 2015.CCM mnatumia kila njia kuhadaa umma ili Dr Slaa asigombee Urais.Kwa taarifa yako Dr Slaa asipogombea urais tutafanya maandamano nchi nzima kumshinikiza agombee.Tutakwenda kuzunguka na kuweka kambi makao makuu ya chama hadi Slaa atakapotii kilio cha watanzania.Wafuasi wa Magamba endelezeni porojo kwenye mtandao mkidhani mnaweza kuzuia Dr Slaa kutawazwa Rais 2015.Makene endeleza moto huu ulio nao.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KURUGENZI ya Habari na Uenezi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inapenda kutoa taarifa kuhusu habari zilizoripotiwa kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, juu ya maombi ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinafanya usiku na mchana ili eti Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, agombee ubunge, kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Jimbo la Arumeru Mashariki, Aprili 1, 2012.

Ingawa haijajulikana maombi hayo yanafanyika msikiti upi au kanisa lipi au sehemu ipi yoyote ile nyingine ya kufanyia maombi, Kurugenzi imeshangazwa sana na mantiki ya kuwepo kwa maombi hayo ya CCM yakionesha upendo wa kutiliwa mashaka kuwa chama hicho kimefikia mahali kinaweza kufanyia maombi vyama vingine ili vipate wagombea makini wa kukibwaga vibaya sana katika uchaguzi.

Kurugenzi inapenda kusema yafuatayo juu ya maombi hayo ya CCM, ambayo kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, kama ilivyoripotiwa katika njia mbalimbali za upashanaji habari, imedhihirika dhahiri kuwa ni maombi yanayoongozwa zaidi na hila, husuda kwa CHADEMA na Katibu Mkuu wake, Dkt. Slaa;

Tunapenda CCM wajue kuwa CHADEMA na viongozi wake makini, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa, si watu wa kurudi nyuma. Chama hiki daima muda wote kinapanga mikakati na mipango ya kusonga mbele, kikionesha utawala mbadala, kikijiandaa kushika dola na kutekeleza malengo ya Watanzania!

Kwa mantiki hiyo, chama hiki hakiwezi kurudi nyuma, hakiwezi kumrudisha nyuma Katibu Mkuu wake, Dkt. Slaa kuwania ubunge. Kiongozi huyu makini, ambaye umma wa Watanzania una imani kubwa naye, ameshavuka viwango vya ubunge, si mtu wa kuwania nafasi ya ubunge tena, (is not parliamentary material).

Kwa nafasi yake ndani ya CHADEMA, anao wajibu mkubwa kujenga chama. Kwa kutimiza wajibu huo, Dkt. Slaa anafanya kazi ya kutengeneza na kuivisha watu wengine makini zaidi, kuweza kuwa viongozi ndani ya chama, nafasi za udiwani na ubunge, ili kuendeleza umakini na uimara wa chama hiki ambacho dhahiri ni tumaini jipya la Watanzania katika kutoa uongozi mbadala wa nchi.

Kwa umakini wa CHADEMA, uwezo wa Dkt. Slaa na matumaini makubwa ya Watanzania, ambayo wameendelea kuyaonesha kwa chama hiki tangu mwaka 2007, kilipoanzisha rasmi mapambano dhidi ya ufisadi na mafisadi, kisha kudhihirika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, nafasi pekee inayomstahili Dkt. Slaa ni urais kwa maana ya kuwa ni ‘presidential material', si ubunge.

Lakini pia, tunatambua kuwa CCM, wameweza kutoa kauli hiyo ya kukurupuka baada ya Dkt. Slaa kuwa tayari ametamka wazi tangu awali na kurudia kauli yake thabiti mara kadhaa kuwa hana nia wala mpango wa kuwania ubunge mahali popote pale nchini. Hawezi kufanya hivyo kwani hata ubunge wa Karatu hakushindwa bali aliacha mwenyewe kwa hiari yake, ili kutekeleza mahitaji ya umma wa Watanzania.

Kurugenzi ya Habari na Uenezi inatumia nafasi hii kuwaambia CCM kuwa watambue CHADEMA ni chama makini. Kimedhihirisha hivyo mara kadhaa katika masuala makubwa kwa maslahi ya Watanzania. Kitaendelea kudhihirisha hivyo pia katika uchaguzi wa Arumeru kwani kina utaratibu wa kuwapata wagombea wake, kutokana na maamuzi ya wanachama wake.

Tunatambua kuwa kauli hiyo ya CCM pia ni sehemu ya mkakati wa makusudi kuwakatisha tamaa baadhi ya watu wanaotaka kugombea jimbo hilo kupitia CHADEMA. Kurugenzi ya Habari na Uenezi inapenda kusisitiza taarifa ya awali, kuwataka wanachama wetu wajitokeze kwa wingi kuwania uteuzi wa kugombea ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.

Tunataka CCM wajue kuwa suala la kuteua mgombea wa CHADEMA ni la CHADEMA yenyewe, kwa kutumia utaratibu wake, ikiongozwa na katiba, kanuni na mahitaji ya umma, wala hatuhitaji ushauri wa chama ambacho kadri siku zinavyokwenda, kinadhihirisha kila dalili ya kuchoka kujisimamia chenyewe, kusimamia wanachama wake, kusimamia serikali na maendeleo ya watu, hivyo kupoteza kabisa ushawishi kwa wananchi. Wala hatujawahi kuomba ushauri kutoka kwao hata siku moja.

Lakini maombi hayo ya CCM, kama ambavyo Nape amenukuliwa katika vyombo vya habari akisema, yamedhihirisha namna ambavyo chama hicho bado kinaandamwa na mzimu wa CHADEMA na Dkt. Slaa tangu baada ya uchaguzi mkuu, kwa kuiba kura na kuvuruga matokeo ya uchaguzi huo.

Kauli ya Nape kuwa iwapo maombi yao yatafanikiwa na Dkt. Slaa akawania ubunge, CCM watakuwa wamemaliza kazi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, inathibitisha tuhuma hizo na namna ambavyo CCM hakikushinda kwa haki uchaguzi huo.

Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya pia inataka CCM waelewe kuwa umaarufu wa CHADEMA hautokani na umaarufu wa mtu mmoja mmoja wala hausubiri matukio pekee, bali unatokana na uongozi makini, kuanzia ngazi ya taifa hadi ya msingi, kikijikita katika kusimamia masuala yenye maslahi kwa Watanzania na nchi yao muda wote!

Imetolewa leo Februari 18, 2012, Dar es Salaam na

Tumaini Makene
Afisa Habari wa CHADEMA

hapo ambako CDM wamejidai ni wapi..? hiyo statement mbona iko clear.. hapo ambapo kupo highlighted mbona panajieleza..?

Ujumbe umefika!Kulikuwa hakuna ulazima wa kuweka maneno mengi yasiyohusika.Am cdm member and i didn't like this release.I expected just a short and clear one.
 
Upende usipende Dr Slaa ni Presidential material.Utake Usitake Dr Slaa atagombea urais 2015.CCM mnatumia kila njia kuhadaa umma ili Dr Slaa asigombee Urais.Kwa taarifa yako Dr Slaa asipogombea urais tutafanya maandamano nchi nzima kumshinikiza agombee.Tutakwenda kuzunguka na kuweka kambi makao makuu ya chama hadi Slaa atakapotii kilio cha watanzania.Wafuasi wa Magamba endelezeni porojo kwenye mtandao mkidhani mnaweza kuzuia Dr Slaa kutawazwa Rais 2015.Makene endeleza moto huu ulio nao.

Sio kila wakati unazi tu, jaribu kuipa fursa ata kidogo akili yako kufikiri. Ulimbukeni huu wa kukosolewa mnakimbilia eti mtu wa magamba utawagharimu sana. Utaandamana na nani? inaonyesha jinsi ulivyo mvivu wa kufikiri na usiye jua wigo wa demokrasia. Am very skeptical on your view. You need to learn more on elementary politics kabla ya ku-shout all the time with political blindness in the umbrella of "CDM adopter".
 
he!.....................kumbe Dr. slaa alishakuwa mgombea urais wa kudumu wa chadema??.................. mie sikulijua hili!!.................. mnarudia yaleyaleee...................

halafu si vyema chama kuwa na dharau namna hii..................... nani kasema ubunge ni kazi ndogo na duni sana kiasi ambacho ni aibu mtu kama slaa kuifanya??................... kwa hiyo slaa sasa ni superior kwa wabunge wote?................. hivi mnajua kuwa hata rais kibaki na odinga wa kenya ni wabunge mpaka sasa?................ so slaa yuko kwenye viwango vya juu hata ya kibaki na raila??................... hebu acheni kudharau kazi ya ubunge na wabunge wetu................. tumhwshimu kila mtu na kazi aifanyayo kwa maslahi ya taifa tafadhari...............

mtaharibu chama chenu sasa na hii kasi ya kumjibu kila mtu chochote asemacho....................... mingine ni mitego tu, msiwe mnajibu.................. ni ushauri tu wakuu.......................
Mimi nadhani baada ya kuisoma hii taarifa ulipaswa ujipe muda kuzielewa hoja zilizoandikwa, naona kama unajitungia maswali na kujijibu mwenyewe, mbaya zaidi unaandika vitu ambavyo havipo kwenye hii taarifa. Usiwe na preconceived mind wakati unasoma taarifa fulani, wewe isome kama ilivyoandikwa bila kuibebeshea maneno yako. Kama vipi ungeandika taarifa yako ili hii ya watu uiache isomeke kama ilivyokusudiwa.

1. Hakuna aliyesema kuwa ubunge umedharauliwa, ila kilichoelezwa hapo ni kuwa Dr. Slaa keshavuka hiyo level, yeye ni Presidential material. CDM is forward looking hivyo si busarakwa Dr. kugombea ubunge ilihali alishasimama katika kugombea nafasi ya urais,Kama Slaa angesimama Arumeru, CCM hao hao wangeleta maneno mingi kuwa CDM si strong na kinaona hakiwezi kuongoza nchi thats why Slaa karetreat na kugombea Ubunge,Usisahau kuwa hii ni Siasa Kiongoz. Aidha, hakuna aliyesema kuwa Dr. Slaa atasimama nafasi ya Urais uchaguzi ujao, just read between lines. Mara nyingi CDM inasema na hata katika hii taarifa imesemwa kuwa CDM kina utaratibu wa kuteua/kupata wagombea kupitia vikao halali vya wanachama wake.

2. Hoja inapotolewa na msemaji rasmi kwenye vyombo vya habari hususan toka kwa mpinzani wenu dhidi yenu haina budi kujibiwa mana ukikaa kimya wanachama na umma kwa ujumla wake hautajua msimamo wa chama chao/chenu. Pia usisahau kuwa ujumbe wa Nape umebeba siasa hivyo anatakiwa kujibiwa kisiasa na kuprove kwa umma kuwa Nape/CCM ni wakurupukaji.
 
Ujumbe umefika!Kulikuwa hakuna ulazima wa kuweka maneno mengi yasiyohusika.Am cdm member and i didn't like this release.I expected just a short and clear one.
Kama wewe kweli ni mwanachadema basi utakuwa Mamluki, hii press release ipo sawa kabisa, kumbuka hii release haiendi kwa wasomi peke yake mnaotaka just a summary. Hii inamfikia hadi babu yangu kule Kazuramimba. Hivyo inahitaji kuwa self explanatory.
 
Back
Top Bottom