YAGHAMBA
JF-Expert Member
- Aug 8, 2012
- 545
- 147
Napenda kuipongeza Chadema kwa kazi kubwa waliyokwisha kuifanya hadi sasa ktk kutoa elimu ya uraia ambayo watawala wa mabavu (CCM) hawataki iwafikie watanzania walio wengi na wanafanya kila njia kuhakikisha wanazizima juhudi hizo, msirudi nyuma. Naiomba CHADEMA ukifika wakati wa kuiboresha daftari la kudumu la wapiga kura wafanye oparesheni maalumu nchi nzima ya kuhamasisha vijana kujiandikisha kwa wingi na kuzitunza shahada zao hadi wakati wa kupiga kura, hili litasaidia sana kuwaondoa CCM 2015 kwani watashindwa kuwahonga na kuzinunua shahada sababu zitakuwa nyingi sana.