Taarab

Hivi humu JF kuna wapenzi wa Taarab kweli? Mimi napenda sana Taarab aisee. Napenda midundo yake. Napenda jinsi nyimbo zake zilivyo ndefu. Unasikiliza hadi unaridhika.

Napenda jinsi watunzi na waimbaji wake wanavyotumia ujuzi wa lugha kufikisha ujumbe. Hususan napenda jinsi sitiari zinavyotumiwa.

Aah mirindimo ya Taarab swaaafi sana.
mi naichukia na siipendi.
 
nakatiza majadiliano yenu.
nilianza kuipenda taarabu siku moja nilienda Traventine kulikuwa na taarabu nikacheza na jimama moja likanikunjia mgongo na mimi nikalionyesha ujuzi wimbo ulipoisha jimama likaniambia lakini mimi ni mamako.
haya anzani kunishambulia mimi sasa badala ya mtoa maada
 
Duu mkuu taarab ina raha yake hasa pale ile mijimama inavoimba na kunesa, na ukifikiria ile taaaarabu yenyewe :love: ha ha haaaa!!:love:
 
Tupo pamoja NN, hata mi napenda taarabu na rusha roho pia. Taarabu napenda inavyobembeleza, yani unaweza sahau shida zote, rusha roho yale masebene wacha tu yani.
 
Unapenda taarabu, then hujui Mayasa ni jinsia gani? Shame on you!

Wewe kila jina la mwanachama wa JF unaijua jinsia yake ya kweli? We ngumbaru kweli wewe...yaani hujui kuwa JF ni chaka la kuficha utambulisho wa watu? Hebu nipishe huko ebo!!!!
 
Hebu cheki mistari hiyo yaani raha tupu....
kama unaweza mpe asitoroke nyumbani, kama unaweza mume asibanduke chumbani,
Muandalie mapishi akishiba ajirambe, awakomeshe wazushi apitapo ajigambe
 
Huwa unakwenda wapi.......Travertine au???

Sikosagi mimi hapo. Halafu Jahazi wanazindua vitu vipya Jumapili ya Pasaka....I can't wait aisee. That Mzee Yusuf ni mwisho hahahahaaaaaaa big up Jahazi Modern Taarab
 
Sikosagi mimi hapo. Halafu Jahazi wanazindua vitu vipya Jumapili ya Pasaka....I can't wait aisee. That Mzee Yusuf ni mwisho hahahahaaaaaaa big up Jahazi Modern Taarab

Hebu nipe ratiba bana wanazindua wapi nikija fasta nihudhurie au sio nipe update plz..................
 
Wewe kila jina la mwanachama wa JF unaijua jinsia yake ya kweli? We ngumbaru kweli wewe...yaani hujui kuwa JF ni chaka la kuficha utambulisho wa watu? Hebu nipishe huko ebo!!!!
Ka ni njemba halafu anajiita Mayasa, basi ana walakini huyo...
 
NN mimi napenda sana taarab ingawa si nyimbo nyingi saana.mashairi yake yamepangwa vzr na huliwaza na kuburudisha muda mwingi na huku nyingi zikituongezea ujasiri wanawake dhidi ya wakaka na wanaume wengne.angalia hiki kipande 'kupendwa bahati yangu si mzizi kutumia,asili na jadi yangu wangu kumringia. Na 'penzi hili siri yangu kazi bure unanuna,yeye ametua kwangu mimi haswa namkuna.amependa umbo langu nini kinachokutona,amependa umbo langu nn kinachokutona. kwa ujumla taarab iko muzuri sana
 
Dah swaafi sana Firstlady....

Yaani mimi Taarab naipenda sana. Na hiyo mistari hapo juu ndo ushahidi tosha kwa nini napenda taarab. Cheki hii ya mfalme wa wafalme....

chakula nnapikiwa, nnawekewa mezani,
nikila nnapepewa, kishuke vema tumboni,

sigombwi mimi, nnadekezwa,
na nikiumia napulizwa,
kufanya utundu nnakatazwa,
siwahi kusema, nnaulizwa,
nikiwashwa hunikuna na muwasho ukaisha,
na maradhi nnapona, presha ananishusha,
shuu shuu shusha, ananishusha
 
tafadhali sijigambe kama nakupenda sana
sio kweli hata chembe uongo unaonena
unavyotaka jipambe siridhiki kwa kuona
sitouchezea wembe unikate najiona

kwangu mm si rahisi moyo nimefunga sana
hugeuki ibilisi hizo bure zako dhana
wameshindwa walopasi wazuri kila aina
wote hutangaza basi hutangaza najiona

kukusalimu wajibu utu kusalimiana
isiwe ndio sababu kusema yasio maana
watu wakataajabu uongo kwao kunena
kupenda sitojaribu bibi samahani sana

usijipe ufakhari uso wako kuuchuna
ukatangaza habari bahati kuvunjiana
mwenye kutaka hukiri akipata hujivuna
ndipo akatafakhari alipolima kavuna
 
Back
Top Bottom