Taa za barabarani

Elusive

JF-Expert Member
Nov 26, 2008
223
4
Nakumbuka katikati ya mwaka jana 2008 barabara inayoanzia Kijitonyama science kupitia Rose Garden mpaka kwa Mwalimu Nyerere iliwekewa taa ambazo siyo tu zilipendezesha barabara ile lakini pia iliifanya iwe na usalama katika nyakati za usiku.

Lakini hivi sasa taa zile zimeondolewa katika nusu ya barabara, kutoka kwa Mwalimu Nyerere mpaka kwenye corner ya karibu na maflat ya NSSF.

Tunawaomba wahusika watufahamishe kwa nini wameondoa taa ambazo zilikwishazoeleka au eneo hilo halina umuhimu wa kuwekewa taa?
 
Siyo hizo tu barabara ya Morogoro yote ina taa ambazo haziwaki sasa kwa muda mrefu.Kwenye junctions karibu zote kuna walakini wa taa hata za kuongozea magari.Unajua sababu kubwa ni kuwa hakuna Mamlaka moja husika inayoshughulikia taa hizi.Mara Manispaa zinazohuska ,Mara Tanroad kwa barabara kuu nk.

Sasa unajua kukiwa na chombo kimoja kinachosimamia taa za bararabarani hakutakuwa na sababu ya msingi kwanini taa au alama zingine za barbarani zisiwepo na zifanye kazi!
 
Back
Top Bottom