Chocolate
Senior Member
- Feb 5, 2009
- 117
- 48
Wana JF ninaomba mnisaidie kuelewa katika hili. Ninashindwa kuelewa jinsi nguzo za taa za barabarani zilizowekwa katika barabara ya Kawawa - kutoka kwa Makamba (Karume) mpaka njia panda ya Kigogo na nadhani zitaendelea mpaka magomeni. Binafsi naona kama zimewekwa karibu karibu mno yaani kutoka nguzo hadi nguzo ni pafupi mno je ni utaalamu umetumika ama vipi? Na Je kwa nguzo za taa zilizowekwa katika barabara mpya ya kilwa mfano nguzo moja iko Mtoni kwa Azizi Ali na inayofuata iko Mtoni Mtongani nako ni sahihi kumefuata utaalamu ama vipi? Naomba kuelewa tafadhali kama ni Utaalamu?, ufisadi?, upendeleo?, siasa?, uzembe?