POLITE MAN
Member
- Oct 14, 2011
- 41
- 7
Mimi nimeacha kupiga simu za tigo jioni maana nimeweka mia tano nimetumia sekunde 10, nimewapigia c.care hawapokei,
TTCL wako wapi tuamie huko kizalendo?
yaaan hii kampuni wezi wakubwa tena wote tu hata hao eyatel ku mamazao wizi tu. tumechoooka kuibiwaaa.
Miezi ya hivi karibuni, kampuni ya simu ya Tigo imelalamikiwa sana kutokana na tabia zao za kihuni. Wamekuwa wakiwaibia wananchi mchana kweupe, na shirika letu la TCRA kushindwa kuchukua hatua yoyote licha ya malalamiko lukuki. Leo mchana, nimenunua vocha za Tsh 10,000 (yaani 5 mbli) nimehangaika sana kuziingiza bila ya mafanikio. Rafiki yangu ambaye nilienda kukutana naye pale Jackys akawa anajaribu kuweka naye kashindwa 5,000 nzima. Kwa pamoja tukajaribu sana kuwapigia kastama kea yao 0713-800-800 kwa takribani lisaa lizima, simu ikawa haipokelewi.
Wananchi, leo tunatangaza rasmi kuanza kuwasusia hawa majambazi. Tunajua serikali yetu imeoza na hakuna pa kupelekea malalamiko, TCRA yenyewe ndo hao wanaoenda shule na 2billion. Sasa kujikomboa dhidi ya hawa wezi ni kutupa smcard zao. Tunatangaza tarehe 08/11/2011 iwe ni siku ya kutokutumia laini za tigo. Zimekuwa ghali mno na ni wezi wa kutupwa. tafadhali sambaza ujumbe
TTCL wako wapi tuamie huko kizalendo?