T.C.R.A Wanatumaliza; TiGO Nao Wanatunyofoa Ngozi, Chukua HATUA

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Miezi ya hivi karibuni, kampuni ya simu ya Tigo imelalamikiwa sana kutokana na tabia zao za kihuni. Wamekuwa wakiwaibia wananchi mchana kweupe, na shirika letu la TCRA kushindwa kuchukua hatua yoyote licha ya malalamiko lukuki. Leo mchana, nimenunua vocha za Tsh 10,000 (yaani 5 mbli) nimehangaika sana kuziingiza bila ya mafanikio. Rafiki yangu ambaye nilienda kukutana naye pale Jacky's akawa anajaribu kuweka naye kashindwa 5,000 nzima. Kwa pamoja tukajaribu sana kuwapigia kastama kea yao 0713-800-800 kwa takribani lisaa lizima, simu ikawa haipokelewi.

Wananchi, leo tunatangaza rasmi kuanza kuwasusia hawa majambazi. Tunajua serikali yetu imeoza na hakuna pa kupelekea malalamiko, TCRA yenyewe ndo hao wanaoenda shule na 2billion. Sasa kujikomboa dhidi ya hawa wezi ni kutupa smcard zao.

Tunatangaza tarehe 15/11/2011 iwe ni siku ya kutokutumia laini za tigo. Zimekuwa ghali mno na ni wezi wa kutupwa. tafadhali sambaza ujumbe
 
Miezi ya hivi karibuni, kampuni ya simu ya Tigo imelalamikiwa sana kutokana na tabia zao za kihuni. Wamekuwa wakiwaibia wananchi mchana kweupe, na shirika letu la TCRA kushindwa kuchukua hatua yoyote licha ya malalamiko lukuki. Leo mchana, nimenunua vocha za Tsh 10,000 (yaani 5 mbli) nimehangaika sana kuziingiza bila ya mafanikio. Rafiki yangu ambaye nilienda kukutana naye pale Jacky’s akawa anajaribu kuweka naye kashindwa 5,000 nzima. Kwa pamoja tukajaribu sana kuwapigia kastama kea yao 0713-800-800 kwa takribani lisaa lizima, simu ikawa haipokelewi.

Wananchi, leo tunatangaza rasmi kuanza kuwasusia hawa majambazi. Tunajua serikali yetu imeoza na hakuna pa kupelekea malalamiko, TCRA yenyewe ndo hao wanaoenda shule na 2billion. Sasa kujikomboa dhidi ya hawa wezi ni kutupa smcard zao. Tunatangaza tarehe 08/11/2011 iwe ni siku ya kutokutumia laini za tigo. Zimekuwa ghali mno na ni wezi wa kutupwa. tafadhali sambaza ujumbe

Pole sana kaka hawa watu wanapata faida kubwa lakini hawawajali kabisa wateja wao kuhusu serikali yetu ni ya wafanya biashara na wengine wanahisa zao humo unategemea nani atakemea ni kuwahama tu kwenda ambako mambo hayajawa Mabaya
 
Point yako sijaielewa,ni wezi kwa kua VOCHER zimekataa kuingia au kuna sababu nyingine?
 
Miezi ya hivi karibuni, kampuni ya simu ya Tigo imelalamikiwa sana kutokana na tabia zao za kihuni. Wamekuwa wakiwaibia wananchi mchana kweupe, na shirika letu la TCRA kushindwa kuchukua hatua yoyote licha ya malalamiko lukuki. Leo mchana, nimenunua vocha za Tsh 10,000 (yaani 5 mbli) nimehangaika sana kuziingiza bila ya mafanikio. Rafiki yangu ambaye nilienda kukutana naye pale Jackys akawa anajaribu kuweka naye kashindwa 5,000 nzima. Kwa pamoja tukajaribu sana kuwapigia kastama kea yao 0713-800-800 kwa takribani lisaa lizima, simu ikawa haipokelewi.

Wananchi, leo tunatangaza rasmi kuanza kuwasusia hawa majambazi. Tunajua serikali yetu imeoza na hakuna pa kupelekea malalamiko, TCRA yenyewe ndo hao wanaoenda shule na 2billion. Sasa kujikomboa dhidi ya hawa wezi ni kutupa smcard zao. Tunatangaza tarehe 08/11/2011 iwe ni siku ya kutokutumia laini za tigo. Zimekuwa ghali mno na ni wezi wa kutupwa. tafadhali sambaza ujumbe
Nakuunga mkono, lakini kwanza ungeanzisha kakampuni kako kasikoibia wateja, hata kama mawasiliano yake yataishia k/koo tu inatosha kuanzia. Tuachane na makampuni ya mafisadi wezi au sivyo?
 
Nakuunga mkono, lakini kwanza ungeanzisha kakampuni kako kasikoibia wateja, hata kama mawasiliano yake yataishia k/koo tu inatosha kuanzia. Tuachane na makampuni ya mafisadi wezi au sivyo?

Maneno yako yameniingia hadi kumtema hakika .It is about time na watanzania kwani hawawezi kugomea tigo ? Bora sina simcard ya tigo na sitampigia mtu wa line ya tigo tena .
 
Mimi wamenipigia kwa namba yao hiyo 800800 na balance yote ikaondoka. Nimeweka buku mbili dk 4 alfu mia 300.tunaibiwa.I Will never recharge again.
 
Hata kitengo chao cha tigo pesa ni wizi mtupu,cumission zao mbovu!,customer care nayo kimeo! Unahudumia mteja mmoja nusu saa !aaaaaagh bora kuhamia airtel wewe na jamaa zako
 
Siku nyingi nilishalalama hapa jamvini I think 2008 lakini hakuna chochote kilichoendelea wakati niko home. Huku US tunauza m-a-t-a-k-o na biashara ni nzuri. Kataeni TiGo kwa nguvu zote. Kibaka mwingine ni TISIARAEI was-h-e-nzi sana, hawafuatliii wala ku-regulate chochote wamekaa tu kama mchuzi wa ngama. Kudaddadeki.
 
Na hapo kuna mtu analipwa mshahara kufanya kazi ya PR/Communications! Kadhia yote hii lakini hakuna maelezo!
 
Hii Kitu itangazwe mahali pengi ili kweli tuwasusie, me ni victim wa muda mwingi sasa
 
Wale wanaotumia Tigo-Pesa subirini msiba zaidi.................
 
Mi binafsi nilishaweka thread ya uhuni unaofanywa na tigo. Mimi nimeshampunguzia vocha mtu na haikumfikia, nikajaribu kupiga 800800 nikaishia kukatwa pesa tu maana hawapokei simu kamwe! Mbaya zaidi hii namba 800800 wanakuja kukupigia nayo na kukuwekea maelezo yaliyorekodiwa.
 
Tigo kwanza hata kwenye top 10 za makampuni yanayolipa kodi vizuri haimo ilhali wenzao air tel wamo. Wapuuzi tigo jamani tusimame pamoja na tuseme inatosha. Mafisadi watushinde hata hawa nao? Hapana.
 
Tigo wanasahau kuwa wateja ni kama joto, mara zote utoka sehemu moja na kwenda nyingine! Katika kipindi cha miaka 3 wateja wengi waliamia tigo kwasababu ya gharama zao kuwa nafuu.

Lakini kama kawaida ya wengi, sasa wamejisahau na kudhani wateja hawa ni wakudumu na hawana pa kwenda!. Kosa kubwa, na si muda mrefu wataona nguvu ya Airtel endapo watabaki na tabia yao ya kuwalaghai wateja!
 
Back
Top Bottom