Synovet: JamiiForums iliegemea upande wa CHADEMA uchaguzi mkuu 2010

Status
Not open for further replies.
Sidhani kama wanaoiunga mkono CCM walizuiwa kujiunga JF, nadhani wapo wengi sana ila walijificha kutokana na kushindwa na hoja za wapinzani wao. Kifupi ni kuwa hakukuwa na upendeleo kwa chadema!
 
hili swali inabidi william @New yorl city alijibu
kwa nini JF iliipendelea chadema?
 
Nina mashaka na uwezo wa kufikiri wa watu wa Synovate Tanzania.

Huwezi ukalinganisha jf na other electronic media like blog ya michuzi. JF ilinganishwe na facebook au twiter. JF ihukumiwe kutokana na mchango wa members sio JF per se
 
Wajinga hawa. Wanailaumu JF bure!

Walioikataa CCM ni members hapa maana hapakuwa na forum ya kusemea na wengi ni wasomi tu watu wa vijijini na wasio na shule hawajui JF ni kitu gani. CCM basi waje humu wake na hoja tukutane. Si kaja Nape anapwaya hapa kila siku? Hapa JF kuna wanachama hawaipendi CCM hakuna mjadala zaidi ya hapo.
 
hivi hiyo blog inayoitwa michuzi ndo blog gani hiyo ambayo umaarufu wake unalinganishwa na jf??!sioni wwa kulinganishwa na jf jamani..msitupotezee!!!
 
Nina mashaka na uwezo wa kufikiri wa watu wa synovate.Huwezi ukalinganisha jf na other electronic media like blog ya michuzi. JF ilinganishwe na facebook au twiter.JF ihukumiwe kutokana na mchango wa members sio JF per se

JF ilinganishwe na Facebook au Twitter?? Tell me you are joking!
 
  • Thanks
Reactions: Wun
Wakimaliza hili tunawaomba watuambie Tume ya Uchaguzi nayo Iliegemea Upande gani!Au ilikuwa Nyutroo!
Waache Mambo laini laini!
 
Siwezi kushangaa na taarifa ya aina hiyo kwa vile watu wenye akili timamu hawawezi kuishabikia CCM kutokana na rekodi yake inayojulikana. Kabla ya uchaguzi JF haikuwa na wapiga propaganda wengi kama walitumwa hapa siku za hivi karibuni. Wanachama wake wengi walikuwa wanachambua mambo objectively, hivyo wasingeweza kuegemea upande wa CCM.
 
JF siyo kama gazeti au kituo cha runinga. Habari nyingi zinatokana na members na michango yao. Kwa hiyo ni members wa JF waliegamia upande wa Chadema ila huwezi sema JF iliegemea upande wa Chadema. Inaonyesha hawajui forum ni nini na madhumini yake ni nini.
Mkuu umemaliz kila kitu. JF inakuwa kuntrolled na members wenyewe na siyo mtu mwingine pembeni.

Naona magamba wanakuja kwa style nyingine.
 
Nina mashaka na idara zao za ubongo. JF inajinadi kwa maandishi makubwa tu hapo chini kuwa ni "User Generated Content" site, wasichoelewa hawa wehu ni nini?

JF does not exist; its USERS does! So does the content and everything in between and beyond.
 
Ila kufananisha Michuzi Blog na JF ni sahihi?nikijiridhisha hapo ndipo nitakapochangia
Si sahihi kabisa. Ila ni obvious forum yoyote yenye watu walioenda shule kidogo haitakuwa na wana magamba wengi, wao wana forum zao kule vijijini.
 
Hata hivyo Synovet si ni wale wale? wao wamejiweka kwenye kundi gani maana wao walikuwa upande wa CCM.
Hawana jipya wanapoteza muda wetu kujadili mambo mengine ya maana maana wao tunawajua. Kuendelea kuwasikiliza ni kupoteza muda wangu kwa heri synovet sihitaji hata kusoma hiyo ripoti yenu.
 
MAVI kabisa kama TBC1 ilikuwa Fair kwenye General election. Kukatiwa mawasiliano kwa CHADEMA walipokuwa wanazindua kampeni yao ndiyo fairness???

Kwa kuwa waliinyima CHADEMA access kwenye media zingine, haikuwa budi kutafuta njia mbadala ingawa haikulingana na Magamba. JF haina ubaguzi, hata coverage za Magamba zilifika humu.

Synovet my A-S-S
 
Wamechemsha, walipaswa kutofautisha jinsi vyombo vilivyo ripoti na jinsi wananchi walivyoshiriki, kwenye JF haukuwa msimamo wa chombo chenyewe bali member - hii ni tofauti na Michuzi, ITV, TBC, Magazeti yote na Radio zote. Hawa jamaa wanatuchanganya ili mradi tuchanganyikiwe, wewe unawezaje kulinganisha JF na TBC au ITV??

JF ni mawazo na misimamo ya wananchi wengi ambao ni member wakati TBC au ITV ni mawazo na misimamo ya wamiliki.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom