Synovate walilipwa na ikulu kufanya utafiti

KILE kinachoitwa umaarufu wa Jakaya Kikwete, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeelezwa kuwa ni “taarifa za kupanga” za asasi zinazoendesha kura ya maoni, MwanaHALISI limeelezwa.

Kwa mujibu wa uchunguzi, asasi zilizotoa taarifa za umaarufu wa wagombea urais nchini, zina uhusiano wa karibu na ikulu, kampuni ya Synovate imekuwa na uhusiano wa kibiashara na ikulu.
Gazeti la hili linazo nyaraka mbili zinaonyesha kuwapo kwa mahusiano ya karibu, ya kibiashara na kibinafsi, kati ya ikulu na kampuni ya Synovate.

Mahusiano hayo yameonekana katika madokezo kadhaa yaliyotoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu kwenda kwa katibu wa rais, mwenyekiti wa bodi ya tenda ya ikulu na mkuu wa shughuli za ikulu (Mnikulu).

Rweyemamu katika maelezo yake anasema, tayari amefanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Synovate Tanzania (zamani ikiitwa Steadman Group) na kukubaliana kufanya kazi ya kitafiti.

Rweyemamu amemthibitishia katibu wa rais katika dokezo lake, kwamba kinachotakiwa na ikulu ndicho kitatekelezwa na uongozi wa Synovate, na kwamba baadhi ya huduma hizo watazipata bila kulipia chochote.

Kuvuja kwa taarifa za kuwapo kwa mawasiliamo ya kibiashara na binafsi kati ya serikali na Synovate kulikuja siku tatu baada ya kampuni hiyo kutoa kile ilichoita, “Ripoti ya utafiti wa kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.”

Katika moja ya madokezo, kutoka kwa Rweyemamu kwenda kwa katibu wa rais, mapema mwaka huu, mkurugenzi huyo wa mawasiliano anaithibitishia ofisi ya rais, kuwa tayari amefanya majadiliano na watendaji wakuu wa Synovate, na kuahidi kutekeleza kile ambacho ikulu inataka.

Rweyemamu anataka Synovate iwaandalie kura ya maoni. Aidha, Rweyemamu anataka kampuni hiyo ieleze kuhusu “nguvu ya vyombo vya habari nchini kwa sasa kutokana na utafiti wao ambao unaonyesha ni chombo kipi kina nguvu ipi na katika maeneo yapi ya nchi au makundi gani ya wananchi.”

Anasema tafiti hizo ni nyenzo muhimu kwao hasa kutokana na kujiandaa na matukio yajayo. Hakuyataja matukio hayo.

Mkurugenzi huyo wa mawasiliano ya rais anasema amethibitishiwa na Synovate kwamba “presentation ya kura ya maoni tutaipata bure, lakini ile ya vyombo vya habari tutalazimika kulipia kama tunahitaji kupata ripoti kamili. Nitakujulisha gharama zao baada ya kuwa nimezungumza nao kwa kina.”

Akisisitiza kuwa hakuna mabadiliko ambayo yatatokea, Rweyemamu anasema, “Nakuomba kama unaweza kuwaarifu maofisa wengine wa OBR – ofisi binafsi ya rais – ambao wako Dar es Salaam kuja kushiriki nasi katika kuona presentations hizo kuanzia saa tisa mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais.”
CCM imetenga Bilioni 150 kwa ajili ya upuuzi wa aina hii wa kuhakikisha Pombe inaingia ikulu hata kwa bao la mkono. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo wapi kuhakiki gharama za uchaguzi zilipangiwa kisheria. Inaonekana CCM inacheza faulo mbaya na za wazi wakati TUME imekaa kama kuku anayehangaika kutaka kutaga mayai bila la kujua la kufanya. STAR TV kwa mfano imenunuliwa 100% mpaka inatia kichefuchefu kuiangalia! TBC ndiyo kabisa, ... Lumumba Branch! Haya yote yanachochea NGUVU YA UMMA kwa umati uliochoka na uzandiki wa aina hii.
 
Tumewachoka ukawa! kila mnachoshindwa mnadai ccm imetoa fedha mshindwe! kubalini ukweli watanzania hawana imani na Lowasa.
 
Siku Yangu Ya Leo Yaenda Vyema Baada Ya Kusoma Andiko Hili, Japo Limepigwa Marufuku Lumumba
 
Babo wewe ni mfata mkumbo unachokiandika hata kichaa mwendawazimu akiona atakushangaa kabisa subiri ushibdi wa kishindo ndani ya ccm waja kaa ukiandia uongo oct ndiyo mwisho wako
 
Babo wewe ni mfata mkumbo unachokiandika hata kichaa mwendawazimu akiona atakushangaa kabisa subiri ushibdi wa kishindo ndani ya ccm waja kaa ukiandia uongo oct ndiyo mwisho wako

Wewe ndio mwendawazimu usieangalia thread ni ya mwaka gani
 
Back
Top Bottom