Synod 2009 na mtizamo wake dhidi ya Afrika

mimi binafsi naogopa sana TZ tunapoelekea kuhusu udini..cha muhim tusiingizwe kwenye siasa za western countries na udini..leo mmarekani anampinga afghanstan na talleban ambae anamuita terrorist lakini ndo huyo alimuezesha kinguvu za kijeshi wakati wa kuibomoa soviet union....
iran na USA hawapatani lakini iran huyohuyo anafanya biashara na Russia...
USA ame force nchi za Africa kuingiza terrorst Legislation katika nchi zao, ambazo kweli zinalinda maslahi yao
hebu niambieni maana ya Terrorist ni ipi?
je terrorist ni yule ambae ni anti USA?


Semenya nadhani bado kuna jambo haliko sawa hapa mzee .
 
First of all, huhitaji uanachama ili kuwa observer.Ukifutilia elimu inayotolewa na thread hii kutoka kwa watu mbalimbali utagundua hawa watu tayari wanahudhuria kama observers bila ya kuwa wanachama.Wanachotaka sasa ni kuwa wanachama kamili ili watoke katika status ya observers na kuweza ku influence policy.

Kuruhusu non-african states au non state organisations kutafungua a can of worms ambayo italeta matatizo mengi kuliko itakayofungua.

Hivi EU kuna non-European state member? hata baadhi ya European states hazijapata uanachama.Kama tunataka chombo serious tuiache katiba kama ilivyo, with membership to African states only.

Otherwise kama tunataka zoo turuhusu haya mabadiliko, hata mimi na familia yangu tuta apply membership tuwe na sauti, si kutakuwa na precedent bwana?

It is my hope that the Holy See appoints a permanent representative to the AU who should attend all the meetings whenever they take place and who could keep in personal contact with the Catholic members of that important institution,- Archbishop Souraphiel said.
-This special representative preferably would have diplomatic credentials comparable to the one of an Apostolic Nuncio,- he explained. .
The idea received the support of the bishops of Southern Africa. The Southern Africa Bishops' Conference would like to endorse Archbishop Berhaneyesus Souraphiel's (Addis Ababa) suggestion that a full time Catholic permanent representative be appointed to the African Union, with more than simply observer status,- Auxiliary Bishop Barry Wood of Durban told the Synod.
Archbishop Souraphiel said that a Catholic representative could be appointed to the AU to be fully committed and available for his mission in such a way that he may attend the meetings and meet the persons who have key influence in the decision making process.


Mkuu Bluray. Hawa wakatoliki hawaombi uanachama AU kama ulivyowashutumu. Pamoja na kibri chao wanajua kuwa ombi kama hilo halitapokewa vyema. Swali la kwanza watakaloulizwa ni kwa nini wasiombe uanachama EU badala ya kukimbilia AU.

Wanachotaka kuomba ni uwakilishi wa kudumu AU (wakibakia na observer status) badala ya hali iivyo sasa ya kuwakilishwa na balozi wao aliye Ethiopia. Uwakilishi huo wa kudumu utahakikisha kuwa wanaweza kufuatilia kwa karibu masuala ambayo wataona yanawahusu na kuwapa nafasi ya kujaribu kushawishi nchi wanachama zenye influence. Tofauti na ndugu zetu wa kiislamu wanavyofikiri, masuala haya si ya ushindani wa kidini bali ni ya kitamaduni. Masuala hayo yanajumuisha, uhalalishaji wa kutoa mimba, uzazi wa mipango n.k. Masuala haya bila shaka hata wale ambao sio wakatoliki watawaunga mkono ( mimi sio mmoja wa wanaounga mkono msimamo wa Kanisa Katoliki kwenye masuala haya). Mengine yanaweza kuhusu kile ambacho wanaweza kuona kama unyanyaswaji wa waumini wao katika baadhi ya nchi.


Wanaposema wanataka awe zaidi ya observer ni huko ku-lobby na sio uanachama. Hii wataweza kufanya vyema zaidi kama watakuwa na mtu maalum dedicated kwa shughuli hiyo. badala ya kumtegemea huyo balozi. Wasiwasi mkubwa wa kanisa Katoliki ni secularism na sio uislamu.

Ni hicho tu.

Amandla........
 
Mh Zitto,

Nisingedhani hilo la Askofu lingekuwa la ajabu kwa mtu kama wewe to the extent ya kudemand explanation! - Afterall yeye ni askofu wa kikristo, na pia nadhani anaisemea Africa nzima. Naamini kuwa ma Immam wengi tu wanashinda kuusema ukristo actually hata mwongozo wa waislam unaongea sana kuhusu ubaya wa ukistro! Why make a big fuss about the presentation ya Askofu. Let serious politicians do clean politics! Hivi leo na kesho akiibuka Kakobe, Gamanya, Sheikh Ponda na wenzao na statements kama hizi tutademand explanation toka kwao!


Umeongea vizuri sana hapa.Tatizo tunaliogopa sana kanisa katoliki na viongozi wake ndiyo mana chochote kitokacho huko basi kinakuwa nongwa
Hivi kwanini wakuu?
 
Semenya nadhani bado kuna jambo haliko sawa hapa mzee .

Me nachoogopa kuona TZ ni kuona kanisa katoliki kama haliridhiki vile na Uislam TZ, sijui tunaelekea wapi..unakumbuka yule askof alivyomshambulia benard membe wakati ule wa mjadala wa Kadhi? kwakweli sio picha nzuri...tanzania bila waislam na wakristo si Tanzania...ndo dini tulizo achiwa na wakoloni hizo, so hamna jinsi we should embrace each other....
 
Shura ya Maimamu said:
Katika dimbwi hili la huzuni, bado Waislam wanaandamwa na propaganda kila uchao kuwa nchi hii inafuata katiba na mtu habaguliwi kwa dini yake na kuwa misingi ya haki, usawa na umoja iliwekwa na “Baba wa Taifa.” Haya yakiendelezwa huku nchi nzima iko mikononi mwa Kanisa Katoliki na fursa zote zimeshikiliwa na Wakristo. Kama hizo fursa walizonazo leo hazitoshi Kanisa Katoliki sasa wanataka kwa dhahiri kabisa kuigeuza Tanzania kuwa ni Jamuhuri ya kikristo.



Askofu Mtega said:
We love Moslems. It is our history and culture to live with them. But the danger which threatens Africa's freedom, sovereignty, democracy and human rights is first the Islamic political factor, i.e., the intended plan and the clear process of `identifying Islam with politics and vice versa' in each of our African countries. Secondly it is the Islamic monetary factor whereby huge sums of money from outside countries is being poured in our countries to destabilize peace in our countries and to eradicate Christianity.

wana Jamii Forums,

..hebu linganisheni kauli za Shura ya Maimamu na ya Askofu Mtega.

..sijui msingi wa mikwaruzano kati ya Waislamu na Wakristo, haswa Wakatoliki, chanzo chake ni nini.

..nadhani badala ya kuwanyooshea vidole upande mmoja wapo, au kudai maelezo na uthibitisho wa wadai wanayotoa, ni bora madai yao kwanza yangefanyiwa kazi kuona wapi tatizo linapoanzia.
 
Sasa hapa mbaya ya baba Askofu iko wapi?

From what I know, conservative Islam iko na zero tolerance kwa watu wasiokuwa waislam!! yaani "wanazuia kutoa mimba kwa sababu kubwa na nzuri tu, kwamba mwenye Umungu na Uumbaji ni Mungu tu na hakuna mwingine!! lakini kitabu hicho hicho kinaruhusu mtu kuua mtu mzima na akili yake ati kwa sababu ni Kafri!! yaani mimba usitoe lakini akisha zaliwa hakawa si mwislmu hana haki ya kuishi!! jiripue kwa bomu na waue unavyoweza!! The bigger the number of dead the bigger the promotion with allah!!

Kosa la baba Askofu ni lipi kama mtu ana mafuta analeta hela kusaidia kupunguza makafri kwa kuwaua ebu kamuulize, sasa hawa watu kudistabilaze serikali zisisokuwa za kiislamu hawana shida kwao hizi ni serikali za "makafri" the unfortunate thing is not so!! yaani watu wote wako sawa na wanahaki ya kuishi !! Mimi sijaona alikokosea Baba askofu!! hayo ya kuzuia maaskofu wasitoe waraka au masheik mimi nafikiri ni kwa watu wenye akili ndogo!! maana la msingi ni kudeal na root of the problem!! kama kinachosemwa je kina ukweli na je tunajisahihishaje??

It is not a question of the Pope or Cardinal,"You can cheat people for the time but you cannot cheat all the people or the time" the earier the better, yaani tuambizane ukweli so long as ni constructive, wacha huu upuzi ati ""His Lordship the Bishop ana makosa.!!!!!!!kwa kutoa paper ya ukweli.
 
Sasa hapa mbaya ya baba Askofu iko wapi?

From what I know, conservative Islam iko na zero tolerance kwa watu wasiokuwa waislam!! yaani "wanazuia kutoa mimba kwa sababu kubwa na nzuri tu, kwamba mwenye Umungu na Uumbaji ni Mungu tu na hakuna mwingine!! lakini kitabu hicho hicho kinaruhusu mtu kuua mtu mzima na akili yake ati kwa sababu ni Kafri!! yaani mimba usitoe lakini akisha zaliwa hakawa si mwislmu hana haki ya kuishi!! jiripue kwa bomu na waue unavyoweza!! The bigger the number of dead the bigger the promotion with allah!!

Kosa la baba Askofu ni lipi kama mtu ana mafuta analeta hela kusaidia kupunguza makafri kwa kuwaua ebu kamuulize, sasa hawa watu kudistabilaze serikali zisisokuwa za kiislamu hawana shida kwao hizi ni serikali za "makafri" the unfortunate thing is not so!! yaani watu wote wako sawa na wanahaki ya kuishi !! Mimi sijaona alikokosea Baba askofu!! hayo ya kuzuia maaskofu wasitoe waraka au masheik mimi nafikiri ni kwa watu wenye akili ndogo!! maana la msingi ni kudeal na root of the problem!! kama kinachosemwa je kina ukweli na je tunajisahihishaje??

It is not a question of the Pope or Cardinal,"You can cheat people for the time but you cannot cheat all the people or the time" the earier the better, yaani tuambizane ukweli so long as ni constructive, wacha huu upuzi ati ""His Lordship the Bishop ana makosa.!!!!!!!kwa kutoa paper ya ukweli.

Kama watu tunawawategemea kuleta mabadiliko ndio wenye fikra kama hizi hapo juu, bado tuna safari ndefu ya kuijenga nchi yetu..
 
Sichukui kipande cha hotuba na kumake opinion. Nadhani kipande kile ni muhimu na kinasema mambo mengi sana katika hotuba ya Baba Askofu Mtega. Sitaki kuhukumu. Napenda kujua maana pana ya alichosema.

Wasiwasi wangu ni kwamba mbegu ya kutoamianiana kati ya Waislam na Wakristo nchini imeanza kumea na tusipokuwa makini itachanua na matunda yake ni HATARI.

Naomba U-NOTE kuwa adui mkubwa wa wakatoliki duniani kote ni Uislam na wanasababu kufanya hivyo.

lakini kubwa kuliko yote ni wakatoliki kuzidi kupoteza waumini ndani nchi za America na Ulaya wakati waislamu wanaongezeka huko.

Hivyo usishangae
 
No way unaweza kumzuia mtu kusema. Ninashangaa zaidi pale ambapo wanaozuia watu kusema nao wanasema. unaweza usikubaliane kabisa na kitu mtu anasema but haki yake ya kusema iwepo
 
Mkutano (Synod) wa maaskofu wa Kikatoliki kutoka Africa ulioitishwa na Papa Benedict XVI unaendelea huko Vatican kwenye makao makuu ya kanisa hilo. Maaskofu kadhaa wamekuwa wakitoa kauli au nyaraka nzito zinazochangamkiwa na waandishi wengi duniani wakati waandishi wa nchini Tanzania ni kama vile tukio hilo halipo.
Moja ya waraka ambao umesomwa duniani kote ni nia ya maaskofu wakatoliki kupata kiti cha ujumbe katika Umja wa Africa (AU) kama vile Vatican ilivyo mjumbe katika umoja wa Mataifa.

Wale wenzetu wenye kupenda kukimbilia hoja ya "kulinda umoja wa kitaifa" sijui sasa watasemaje maana hizi hoja zinatolewa huko Roma au Vatican ambako dunia yote inangalia kila kinachotamkwa. Labda sasa waje na hoja ya kusema "kulinda umoja wa kidunia" maana kilichotajwa ni bara zima la Africa.

mambo wamezungumzia kanisani basi najua wazi yataishia kanisani na wala nje hatutayasikia.

Lakini lazima tuwe na tahadhari ya hali ya juu sana . Kwani hawa wakatoliki wapo smart sana katika lobbing.
 
Balatanda,
Anza kupunguza wewe kwanza ..ndio useme wengine...kwahiyo..ndio wapewe uwakilishi kwenye political organ (AU)?? does it make sense?
Hayo yote ulioweka kuna dini zingine nazo zina shule na universities kibao....after all tukianza kujadili hapa source of income ya hizo services ni "TRA" meaning kodi za kila mtu hata mimi utasema udini kwasababu "UKO PROGRAMMED"
kwako wewe udini ni kama ukiwa na mtazamo nje ya askofu lakini pro-askofu siyo udini...kazi kwelikweli...

Totally out of mind.........!
 
The AU charter says this about membership



Sasa hao wa Vatican / Holy See wataomba membership kwa minajili gani wakati wao si African state?

Bluray,

Haya ni mapendekezo tu yaliyotolewa na Archbishop wa Addis Ababa kwa Holysee. Yale ni mawazo yake binafsi ambayo kwa bahati nzuri au mbaya yakaungwa mkono na maaskofu wa kusini mwa Africa. Hata na hivyo haina maana eti kanisa katoliki Africa limeazimia kuomba uwakilishi kule wa kuparticipate kny shughuli za AU!

Pengine wakija na hoja za msingi, hiyo AU charter can be amended to accomodate such institutions..........!
 
First of all, huhitaji uanachama ili kuwa observer.Ukifutilia elimu inayotolewa na thread hii kutoka kwa watu mbalimbali utagundua hawa watu tayari wanahudhuria kama observers bila ya kuwa wanachama.Wanachotaka sasa ni kuwa wanachama kamili ili watoke katika status ya observers na kuweza ku influence policy.

Kuruhusu non-african states au non state organisations kutafungua a can of worms ambayo italeta matatizo mengi kuliko itakayofungua.

Hivi EU kuna non-European state member? hata baadhi ya European states hazijapata uanachama.Kama tunataka chombo serious tuiache katiba kama ilivyo, with membership to African states only.

Otherwise kama tunataka zoo turuhusu haya mabadiliko, hata mimi na familia yangu tuta apply membership tuwe na sauti, si kutakuwa na precedent bwana?

Mkuu nadhani umemiss point somewhere. Kama nikisoma nia za hao maaskofu na mleta hoja.....wanataka "FORMAL REPRESENTATION". wanataka wawe na mwakilishi wa kudumu pale Addis Ababa. Kama balozi. Na kwa hili Vatican haitakuwa ya kwanza kufanya hivyo. EU, US na nchi kibao wana wawakilishi wao wa kudumu pale AU Addis Ababa. Kazi yao kubwa ni kudumisha ushirikiano baina ya wahusika na vile vile..kuangalia maslahi ya hizo nchi/taasisi husika katika majukumu ya kila siku ya AU. This shows you that..both sovereign countries and international institutions can seek and be granted formal representation. Sasa hili ni tofauti na membership ya State. Na maaskofu wamekuwa very very clear kwamba interests yao ni peace and justice (if I may add-social justice). Sasa hii ina maana gani? ina maana kwamba wanataka wawe na sauti haya mambo endapo yatakuwa yanajadiliwa.

Sasa status yao itakuwa ni ipi?..well they can do it through two ways. Either Pope anaweza kumuappoint mwakilishi pale AU, ambaye ingawa atakuwa mwakilishi wa papa..atakuwa focal point kwa mambo ya Africa. Njia nyingine ni kwa maaskofu wa Africa (kupitia umoja wao either Africa as a whole or through regional groupings zao) kuiomba AU Assembly kuwaruhusu wawe na mwakilishi. To me either means inawezekana. Sioni ugumu wake.

To me, I dont see any problem of membership. Ndo maana mashirika kibao hata ya UN..wana wawakilishi wa kudumu pale AU. Mfano UNHCR kwa sababu ina deal na wakimbizi na Africa ndo kuna tatizo la wakimbizi kubwa, ina muwakilishi wa kudumu pale AU mwenye hadhi ya kibalozi. Kazi yake kubwa ni kuwa advocate wa maswala ya wakimbizi barani Africa. Mifano ni mingi sana tuu.

Sasa hili swala watu wasilipeleke kusiko kuanza kutafsiri doctrines na mengineyo. Its simple. Catholic Bishops want a say in issues affecting their congregation. Namely, peace, justice nk. And they can do so.

If I may say, hata waislamu they can do that. The only problem they have, in my views, hawako organized kama wakatoliki. In otherwords hawana higher up authority kama ya Papa..Vatican ambaye anasema kwa sauti moja. Otherwise if they are organized..they can as well ask formal representation to represent their people`s interests. After all....Haya mashirika kama UN, AU..yapo-atleast theoretically..kuinua hali za wananchi....sasa tatizo liko wapi kama wadau husika wakishirikishwa..katika kutafuta hiyo suluhu? Thats what we call participatory democracy to eliminate inherent democratic deficit kwenye mashirika kama AU.

Masanja,
 
  • Asema ni washirikina, na wezi
  • Asema wanataka watu wapige kura 'gizani'
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Katoliki Songea, Norbert Mtega amewasilisha mada katika mkutano wa kimataifa Vatican, Italia akiwatolea uvivu viongozi wa kisiasa Afrika, Tanzania ikiwamo, na kueleza kuwa wengi wao ni washirikina, wakandamizaji wa elimu ya uraia na wamebobea katika wizi wa raslimali za mataifa yao wakitelekeza haki za wanyonge, hususan wakulima.

Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kuwa ni dukuduku la muda mrefu la Kanisa Katoliki Afrika, Askofu Mtega anasema kwa viongozi wa Afrika “amani na uchaguzi huru na wa haki” vimebeba tafsiri tofauti na inayofahamika kwa raia wengi wa kawaida.

Anasema kwa viongozi hao, tafsiri ya amani ni “anga tulivu linalowawezesha viongozi kuiba na kufuja fedha za wavuja jasho wa nchi zao na uchaguzi huru na wa haki tafsiri yake ni “kuwapa fursa watu kupiga kura wakiwa katika giza la kutojua haki zao.”

Maelezo hayo yanayoweza kutafsiri kuwa ni msimamo mkali dhidi ya wanasiasa Afrika yalitolewa na Askofu Mtega alipokuwa akiwasilisha mada Vatican, Italia, Oktoba 15, mwaka huu. Askofu Mtega aliwasilisha mada iliyoitwa “Ukabila: Kansa inayoitafuna Afrika.”

“Kwa wanasiasa Afrika amani maana yake ni anga tulivu linalowawezesha kuiba na kufurahia mabilioni ya walalahoi katika nchi zao. Kwao, uchaguzi huru na wa haki maana yake ni kufanikiwa kupeleka watu vituo vya kupiga kura bila elimu ya uraia na pamoja na kuruhusu uovu unaofanywa na wagombea. Wanasiasa wanaamini kuwa kuchaguliwa kiongozi maana yake ni kupewa tiketi ya kuiibia nchi,” anasema Askofu Mtega katika mada yake hiyo na kuongeza kuwa;

“Watu wetu wengi wananyanyaswa, kuteswa na kuuawa kwa sababu tu ya imani za kishirikina. Hakuna sheria madhubuti za kuwalinda, serikali inalaani matukio hayo, lakini baadhi ya viongozi wanakula njama na waganga wa kienyeji kufanikisha uchafu wao na maeneo mengine serikali zimehalalisha shughuli hizo.

Anatoa ushauri kwa akisema; “Kunahitajika ushauri mahsusi kwa serikali na viongozi.”

“Uhai wa wakulima wetu upo shakani. Juhudi zao haziungwi mkono kwenye bajeti za serikali zetu na mara kwa mara wamekuwa wakipewa ahadi za uongo. Kanisa barani Afrika lazima lipiganie wakulima na wafugaji sasa:

“Lazima wapate haki yao ya kibajeti kwa kupewa angalau miundombinu na mahitaji ya msingi katika shughuli zao na mazao yao yawe na uhakika wa soko, mipango ya kuwapa masoko ya uhakika ifanyike na masoko ya ndani yalindwe, wapewe fursa ya kukopa kupitia vyama vyao vya ushirika,” anasema Askofu Mtega.

Anasema ukabila ni kansa barani Afrika ambayo ni lazima idhibitiwe na kusuluhishwa kiroho sambamba na kuchukua hatua nyingine za haraka.

Kutokana na mada hiyo ya Askofu Mtega ni wazi kuwa Kanisa Katoliki Tanzania linaendeleza hadharani dhamira yake ya kuhakikisha mgawanyo wa rasimali za nchi unafanyika kwa usawa, likiwa tayari limetoa waraka wa elimu ya uraia kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani.

Mara baada ya kutoa waraka wa elimu ya uraia mapema mwaka huu, ikiwa ni utaratibu wa muda mrefu wa Kanisa hilo kufanya hivyo, makundi ya kijamii nchini wakiwamo wanasiasa waliotoa maoni tofauti baadhi wakipinga na wengine wakiunga mkono.

Waliopinga wamekuwa wakisisitiza kuwa si kazi ya kanisa kutoa elimu ya uraia na kwamba hiyo ni kazi ya vyama vya siasa na wanasiasa. Viongozi hao ambao ni pamoja na Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru wa CCM na Seif Shariff Hamad wa CUF, wamesema taifa linaweza kuingia kwenye mpasuko na hatimaye kusambaratika kama viongozi wa dini wataendelea kuruhusiwa kuingiza masuala ya imani katika siasa na kwamba si ajabu Tanzania ikawa kama Lebanon.

Katika maelezo yao waliweka bayana kwamba hatua hiyo ya Kanisa Katoliki ingepingwa bila woga na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama angekuwapo na kwamba Kanisa hilo ni vema likaufuta waraka wake huo.

Hata hivyo, wakati wanasiasa hao wakitoa hoja zao kwa malengo ya kupinga viongozi wa Kanisa Katoliki, Polycarp Kardinali Pengo na Askofu Method Kilaini walijitokeza hadharani na kueleza kuwa waraka wa kanisa hilo unalenga kutoa elimu ya uraia na si kuelekeza kiongozi gani achaguliwe katika madaraka ya kisiasa.

Viongozi hao walikwenda mbali na kuhoji sababu hasa za viongozi wa kisiasa kuhofia wananchi kupewa elimu ya uraia na hususan katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010, na kuweka bayana kuwa “anayeogopa wananchi kupewa elimu ya uraia ni fisadi.”

Msimamo wa viongozi hao uliongeza mjadala ndani ya makundi ya kijamii, huku serikali na CCM vikibaki kimya na walijitokeza viongozi wengine wa kisiasa waliounga mkono waraka huo, akiwamo Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa.

Viongozi na wanajamii waliounga mkono waraka huo wamekuwa wakieleza kuwa ingawa si sahihi viongozi wa dini kushawishi achaguliwe mgombea wa aina gani katika uongozi wa siasa lakini ni haki yao kutoa elimu ya uraia kama ambavyo waraka huo unavyojieleza.

Kutokana na mvutano huo, katika kikao cha mwisho cha Halmashauri Kuu ya CCM, mjini Dodoma ilipendekezwa viongozi wakuu wa serikali kukutana na viongozi wa dini ili wachukue mapendekezo au malalamiko yao kwa ajili ya kuyafanyia kazi.

Hata hivyo, msimamo huo umeonekana kupingwa na Kanisa Katoliki kupitia kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam, Policarp Kardinali Pengo, ambaye amesema itakuwa ni jambo la ajabu kwa viongozi wa dini kushauriana na wasiasa wakati wa kutimiza majukumu yao.

Msimamo huo wa Kardinali Pengo uliungwa mkono na Jaji Joseph Warioba ambaye katika mazungumzo yake hivi karibuni na waandishi wa habari alieleza kushangazwa na wazo la kutaka viongozi wa dini washauriane na wanasiasa kabla ya kuzungumzia masuala yanayoiumiza jamii kama rushwa na ufisadi.

Kwa mujibu wa Jaji Warioba, kilichoandikwa kwenye waraka kuhusu elimu ya uraia, madhara ya rushwa na ufisadi ndicho wanachohubiri kila mara viongozi wa dini makanisani na misikitini akihoji; “Tunakwenda wapi kama viongozi wa dini lazima washauriane na wanasiasa kuhusu shughuli zao.”

“Nimesoma waraka sioni tatizo lake, nimekuwa nikisoma kwa muda mrefu tangu 1994 kama ingawa mimi si mkatoliki lakini nasoma kwa kuwa ni elimu ya uraia kama ambavyo mimi ni CCM lakini nasoma ilani za uchaguzi za CHADEMA, CUF na vyama vingine,” aliwahi kuzungumza Jaji Warioba akiweka bayana kushangazwa na wanaosema waraka huo utaifanya nchi kuwa kama Lebanon.

Wakati mivutano hiyo ikiendelea, kundi la waislamu pia lilitoa mwongozo kwa waumini wa dini hiyo lakini wao wakielekeza bayana waumini wao kuchagua mtu atakayelinda maslahi ya kundi hilo kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani na kwamba waumini hao wapige kura ya pamoja.

Katika mazungumzo yake na wananchi wakati wa kipindi cha maswali kwa rais, Rais Kikwete alisema si busara kwa wananchi kwenda kupiga kura kwa kuzingatia ukristo au uislamu wao na kwamba hali ikiwa hivyo taifa litakuwa limesambaratika.

Viongozi wengine wa madhehebu mengine ya kikristo yalionekana kuweka msimamo wao wazi kwa kuunga waraka wa katoliki, akiwamo Askofu Valentino Mokiwa.

Hata hivyo, viongozi wengine akiwamo Askofu Zakaria Kakobe ambaye mwaka 1995 alijiingiza moja kwa moja kwenye siasa kwa kumuunga mkono aliyekuwa mgombea urais wa NCCR-Mageuzi, Augustino Mrema, alipinga waraka huo akisema utaligawa taifa.

Msimamo huo wa Askofu Kakobe dhidi ya waraka katoliki ulionekana kuwatibua viongozi wa Kanisa Katoliki kiasi cha Askofu Kilaini kukaririwa na vyombo vya habari akisema hawezi kuzungumzia kauli za mtu ambaye hajui uaskofu wake umepatikana wapi.

Hali ya mambo kwa sasa inaonekana kutulia huku kukiwa na taarifa za kuwapo kwa mapendekezo ya kuanzishwa kwa baraza maalumu litakalojumuisha viongozi wa dini na wa serikali ili kujadili masuala ya kitaifa, vikiwamo viashiria vinavyoweza kuwa chanzo cha machafuko ya kidini nchini.

Mapendekezo hayo yametolewa na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kufanya utafiti na kuchapisha kitabu kinachoitwa “Religion and Politics” (dini na siasa) ambacho mapendekezo hayo yametolewa.

Tayari viongozi wakuu wa dini nchini wameelezea msimamo wao kuhusu kuundwa kwa chombo hicho. Miongoni mwa masharti yao ni kwamba chombo hicho kianzishwe na viongozi wa dini na si serikali.


http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1772
 
Askofu Mkuu kasema ukweli mtupu. Na kwenye sehemu yake yuko Waziri Mdogo mwenye vyeti feki ambaye ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa. Kama nitakumbuka vizuri ni kwamba katika uchaguzi mkuu uliopita, huyo kihiyo wa south alileta vurugu hadi ndani ya ibada!
 
Yani Askofu hapo amesema ukweli kabisa natamani ingekuwa rahisi mambo hayo yakarekebishika kama yanavyosemwa.

Lakini swali linakuja: kwa nini ameenda kusemea huko mbali kote si angesema hapa hapa ndani ya Tz wamsikie? Au mnaonaje wanaJF?
 
Back
Top Bottom