Synod 2009 na mtizamo wake dhidi ya Afrika

We love Moslems. It is our history and culture to live with them. But the danger which threatens Africa's freedom, sovereignty, democracy and human rights is
first the Islamic political factor, i.e., the intended plan and the clear process of `identifying Islam with politics and vice versa' in each of our African countries. Secondly it is the Islamic monetary factor whereby huge sums of money from outside countries is being poured in our countries to destabilize peace in our countries and to eradicate Christianity.

Baba Askofu ana maana gani katika maneno hayo ambayo nimehighlight kwa kijani?
Is he saying Islam is a threat in Tanzania? I would like him to substantiate this claim as it might sow seeds (or fertilize them) of mistrusts between Muslims and Christians in Tanzania.

Nimeogopa kidogo kutokana na hiyo kauli maana inasema mengi sana..............................!
 
Baba Askofu ana maana gani katika maneno hayo ambayo nimehighlight kwa kijani?
Is he saying Islam is a threat in Tanzania? I would like him to substantiate this claim as it might sow seeds (or fertilize them) of mistrusts between Muslims and Christians in Tanzania.

Nimeogopa kidogo kutokana na hiyo kauli maana inasema mengi sana..............................!


Usiogope hata kidogo.
Mwaka wote mzima nimekuwa nikisikia mambo ya mtaani kwamba uteuzi wa mkuu wetu wa nchi umekuwa ukiongozwa na 'u-dini'

Haya ni mambo ya mtaani. Kwa taarifa hii inayosemwa na Askofu, isije ikawa ina maana kwamba anao uthibitisho. Sijui. Tatizo kasema nje tena ndani ya Vatican ambako mazungumzo ya huko ni vigumu nchi kama Tz kuyahoji.
 
nadhani islam is a threat not as a religion but the way it is spread lots of funds coming from unreliable sources like alkaeda, osama na na target kubwa inakuwa vijana ambao wanakuwa na munkari wa kutaka utaifa wa dini husika mafundisho ya radicalism na kuzaa kitu kinaitwa extremist ndo hapo watu wanaanza kujilipua ndo maana akasema hiyo ni threat lkn uislam km dini si hatari maana miaka yoote hii tumeishi wote tumeoleana lkn hakukuwa na athari zozote
 
Zitto,
Mimi nisingependa kuchukua kipande cha speech na kukifanya kikubwa kuliko kilivyo. Mimi ningeshauri kitu kimoja kuhusu hawa viongozi wa dini na wale wa waislam tungewashauri kuhudumisha elimu na afya. Viongozi wa dini wangeweza kukutana na kuweka mikakati muhimu ya elimu hii ingesaidia nchi kuliko siasa. Kitu kimoja ni kwamba viongozi wa Waislam kwa miaka mingi walikuwa wanajihusisha na siasa kwa miaka mingi lakini kina kinacho badilika ni kwamba wakatoliki wameamua kutoa misimamo yao.

Hawa jamaa wana nguvu kuliko siasa wana shule, NGO money, wafuasi wenye uwezo sana, wanaaminika, wana hospitali n.k. Vitu vyote vinavyoendesha na wakatoliki vinafanya vizuri kuliko serikali kuanzia shule hadi hospitali. Kitu kingine ni kwamba elimu ya viongozi hawa ni tofauti sana na elimu ya viongozi wa waislam. Mimi nashauri hasa kwa wanasiasa kulichukulia swala la dini muhimu na kubadilisha mijadala ya hawa viongozi kuwa ya elimu na afya.

Itakuwa vigumu kuwaambia viongozi wa katoliki kuacha siasa wakati viongozi wa kislam wako kwenye siasa kila siku. Tatizo ni kwamba hawa jamaa wanaamini mambo wanayofanya wametumwa na mungu. Mbona slaa aongei alikuwa Pandre wa katoliki! kwasababu ukweli ni kwamba hawa jamaa wamewasha moto ambao haujawahi kuwashwa Tanzania na kama unashtuka sasa ngoja miaka miwili ijayo ndiyo wameanza tu.

Tanzania itabadilika na Nyie ndio mtaamua iendeje lakini msipokuwa makini na kulemea upande mmoja Tanzania itagawanyika.
 
Habari ndiyo hiyo kuna forum uwa hazigusiki unaweza kunyimwa maharagwe ukienda kuomba siku nyingine
 
Zitto,
Mimi nisingependa kuchukua kipande cha speech na kukifanya kikubwa kuliko kilivyo. Mimi ningeshauri kitu kimoja kuhusu hawa viongozi wa dini na wale wa waislam tungewashauri kuhudumisha elimu na afya. Viongozi wa dini wangeweza kukutana na kuweka mikakati muhimu ya elimu hii ingesaidia nchi kuliko siasa. Kitu kimoja ni kwamba viongozi wa Waislam kwa miaka mingi walikuwa wanajihusisha na siasa kwa miaka mingi lakini kina kinacho badilika ni kwamba wakatoliki wameamua kutoa misimamo yao.

Sichukui kipande cha hotuba na kumake opinion. Nadhani kipande kile ni muhimu na kinasema mambo mengi sana katika hotuba ya Baba Askofu Mtega. Sitaki kuhukumu. Napenda kujua maana pana ya alichosema.

Wasiwasi wangu ni kwamba mbegu ya kutoamianiana kati ya Waislam na Wakristo nchini imeanza kumea na tusipokuwa makini itachanua na matunda yake ni HATARI.
 
Secondly it is the Islamic monetary factor whereby huge sums of money from outside countries is being poured in our countries to destabilize peace in our countries and to eradicate Christianity.

Ethnicity is a cancer which torments Africa. We must immediately inculcate reconciliation as our spirituality and life as well as our immediate action.
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -

Baba Askofu yuko sahihi kabisa kusema hayo aliyoyasema; ushahidi upo katika nchi nyingi sana barani Africa. Al-Queda wanafanya kazi usiku na mchana kufikia lengo la kuweka Serikali za Kiislamu duniani. Hilo lengo sio siri na wala hawatafuni maneno wakiulizwa.

Baba Askofu amekuwa makini kwa kutokusema "specific" hela zinatoka wapi huko nje; iwapo zinatoka kwenye nchi fulani, taasisi binafsi au vikundi.
 
Kila rais anapokuwa muislam, basi makanisa haayaachi kulalamika kuna udini,kikwete ana mengi mabovu ya kumhukumu but sio udini.

Sasa kama kuna muislamu ana faa kwa uteuzi afanyeje?

Kwani ni nani anaependekeza majina ya uteuzi?
 
Baba Askofu yuko sahihi kabisa kusema hayo aliyoyasema; ushahidi upo katika nchi nyingi sana barani Africa. Al-Queda wanafanya kazi usiku na mchana kufikia lengo la kuweka Serikali za Kiislamu duniani. Hilo lengo sio siri na wala hawatafuni maneno wakiulizwa.

Baba Askofu amekuwa makini kwa kutokusema "specific" hela zinatoka wapi huko nje; iwapo zinatoka kwenye nchi fulani, taasisi binafsi au vikundi.

Je, kuna uwezekano kuwa fedha hizo pia zinaingia Tanzania na kwamba kuna juhudi ya kuweka serikali ya kiislam Tanzania?
 
Baba Askofu ana maana gani katika maneno hayo ambayo nimehighlight kwa kijani?
Is he saying Islam is a threat in Tanzania? I would like him to substantiate this claim as it might sow seeds (or fertilize them) of mistrusts between Muslims and Christians in Tanzania.

Nimeogopa kidogo kutokana na hiyo kauli maana inasema mengi sana..............................!

Zitto,
Baba askofu hajataja Tanzania. Ndiyo aana wakati nafikisha mada hii niliuliza ni nchi gani ina hati miliki kumbana hata kutoa ushahidi wa alichdai Askofu Mtega.

Ni kweli una haki ya kuuliza lakini naomba uondoe neno Tanzania maana sicho alichotamka Askofu Mtega.

Kuna dhana kwamba kwa sababu Askfu Mtega ni wa jimbo la Songea huenda anazungumzia Tanzania. Kumbukeni kwama Askofu yeyote ni askofu wa Kanisa Katoliki. Askofu Mtega ni asofu wa kanisa Katoliki. Ile kupewa jimbo la Songea ni moja ya majukumu anayoweza kupewa askou yeyote. Vinginevyo basi hata yeye hana asingeweza kuongelea eneo lolote zaidi ya jimbo lake la Songea.

Hivyo kauli yoyote ya Askofu wa Kanisa Katoliki ni kauli ya kanisa zima maana mwenye dhamana na kanisa hilo ni Papa ambaye ndiye anayewapa uaskofu na hata hayo majimbo.

Hivyo Mheshimiwa Zitto, naliheshimu sana swali lako lakini kikubwa kwangu naomba uondoe neno Tanzania na uweke neno Africa kama alivyosema Askofu mwenyewe.

Tusiusemee moyo wake wala tusimuewekee neno lolote.

Tuje kwenye alichokisema. Kama kuna watu wanafadhili kampeni kuufuta ukristo katika Africa mimi sidhani kama wanadunia wote waliokusanyika huko Roma hawtamuuliza. Synod inaisha Oct. 25 na yeye sidhan kama anaweza kuitamkia dunia kitu hiki kama vile ni uzushi.
 
Baba Askofu yuko sahihi kabisa kusema hayo aliyoyasema; ushahidi upo katika nchi nyingi sana barani Africa. Al-Queda wanafanya kazi usiku na mchana kufikia lengo la kuweka Serikali za Kiislamu duniani. Hilo lengo sio siri na wala hawatafuni maneno wakiulizwa.

Baba Askofu amekuwa makini kwa kutokusema "specific" hela zinatoka wapi huko nje; iwapo zinatoka kwenye nchi fulani, taasisi binafsi au vikundi.

Tunaomba ututajie hizo nchi ambazo zimekuwa zikipokea msaada huo hapa Africa. Hii mbegu ya chuki inayozidi kupandikizwa italifikisha taifa hili pabaya.
 
je, kuna uwezekano kuwa fedha hizo pia zinaingia tanzania na kwamba kuna juhudi ya kuweka serikali ya kiislam tanzania?

wewe zitto na wenzio hamuwajui vizuri makanisa.hasa kanisa katoliki.hata ndani ya chadema wana influence...
Hata reginald mengi ni mojawapo ya watu wanaolitumikia kanisa catholic.

Huwajui vizuri hawa...

As long as rais ni muislam na makamu wake ni muislam...
They will never be comfortable....
 
wewe zitto na wenzio hamuwajui vizuri makanisa.hasa kanisa katoliki.hata ndani ya chadema wana influence...
Hata reginald mengi ni mojawapo ya watu wanaolitumikia kanisa catholic.

Huwajui vizuri hawa...

As long as rais ni muislam na makamu wake ni muislam...
They will never be comfortable....

Naomba nitofautiane na mtizamo wako. Tatizo tulilo nalo sasa hivi hapa nchini ni watu wachache (wenye uroho wa kutajirika na kupata madaraka) toka pande zote yaani wakiristu na waislamu - ambao wanapenda kuona nchi ikisambaratika ili waweze kufikia malengo yao. Kutokana na matatizo mengi tuliyo nayo wananchi kwa sasa...tunadanganyika kirahisi na hizi kelele za udini na zitatufikisha kubaya tusipokuwa waangalifu...Sasa hata viongozi wa dini wanaanza kutumiwa tutafika kweli? Mungu atuepushe na hilo balaa..
 
Wasiwasi wangu ni kwamba mbegu ya kutoamianiana kati ya Waislam na Wakristo nchini imeanza kumea na tusipokuwa makini itachanua na matunda yake ni HATARI.

Mh. Zitto,

Mbegu ilishapandwa na ilishaanza kuchipua tunasubiri matunda baada ya miaka si mingi. Huo ndio ukweli. Mbona CHADEMA mliambiwa ni chama cha watu wa Kanda ya Kaskazini? Hiyo inatofauti na anachokisema Askofu Mtega? CUF walishaitwa kwamba ni chama cha kidini kuna mtu aliwahi kukemea hilo? Tena waanzilishi wa hoja hizo ni CCM, chama Tawala ambacho kimeshika dola. Au kwa kuwa leo amesema Askofu ndiyo tunashangaa?

Tukae tusubiri haya mambo, tatizo ni kwamba watawala wetu waliamua kutumia weakness ya udini ili wapate madaraka na wataendelea kuipanda mbegu hiyo taratibu na kuimwagilia maji ili istawi na soon tunaona matunda ya huo uchochezi. Na mbegu ya u-kanda ama ukabila nayo inakuja na imeanzia kupandwa hapo kwenu, baada ya kuonekana kwamba CHADEMA ni tishio. CUF walipotikisa waliitwa wadini, leo hii hakuna aneongelea hoja ya udini ndani ya CUF maana umaarufu wa CUF haupo tena bara bali uko Unguja ambako hoja ya Udini haina nguvu ila kuna hoja ya Upemba na Uunguja, Hizbu vs Shiraz, asili ya umanga vs ungazija. Haya yote siyo mapya, na SMZ imeendelea kuyabariki mpaka kwenye majukwaa ya siasa, hata appointments za viongozi wa SMZ. Au Zanzibar siyo sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Je, JK alipotuhumiwa kwamba ana close ties na Iran na kwamba wame-fund kampeni yake alikanusha? Kwanini CCM walikuja na hoja ya kuanzisha mahakama ya kadhi kwenye Ilani yao? Nilitarajia kwamba waislam wenyewe wangeomba Mahakama ya Kadhi irejeshwe na then serikali iliyo madarakani iwe ya CCM ama CHADEMA ingefanyia kazi ombi hilo na siyo kuiweka kama chambo cha kupata kura nyingi kwa kuwa tu JK ni mwislam.

Je, NGOs zote zilizo kwenye ground ambazo kwa siri zinaendeleza siasa tunajua zinapata wapi hela? Juzi juzi hapa kuna chama cha wanaharakati ambacho kinajipambanua kwamba kiko kila kona kimefungua tawi Tanzania na malengo yake ni kuleta uamsho wa waislam kwenye politics, chama chenyewe siyo cha kisiasa lakini kina malengo ya kisiasa. Je, hiyo siyo kutumia dini kuingiza politics kwenye dini? Je, hao watu tunajua wanapata wapi hela za kuendeshea kampeni zao ama shughuli zao?

Kwa hiyo mpaka sasa naweza kusema maji yameishamwagika soon tutaanza kuwindana wenyewe kwa wenyewe. Ukishaanza kuchora mistari ya udini na ukabila, ujue ndo unaelekea kubaya, na ndiko tunakoelekea.
 
naomba nitofautiane na mtizamo wako. Tatizo tulilo nalo sasa hivi hapa nchini ni watu wachache (wenye uroho wa kutajirika na kupata madaraka) toka pande zote yaani wakiristu na waislamu - ambao wanapenda kuona nchi ikisambaratika ili waweze kufikia malengo yao. Kutokana na matatizo mengi tuliyo nayo wananchi kwa sasa...tunadanganyika kirahisi na hizi kelele za udini na zitatufikisha kubaya tusipokuwa waangalifu...sasa hata viongozi wa dini wanaanza kutumiwa tutafika kweli? Mungu atuepushe na hilo balaa..

actually mi na wewe tunaongea kitu kimoja....i am with u.
 
Nafikiri hapo aliposema "Identifying Islam with politics in each of our African Countries" Ndio penye uzito. Shutma kuhusu ugaidi ni kwamba unafadhiliwa kwa kupitia miasaada ya kifedha kutoka Islamic countries especially Saudi Arabia and Iran among others. Kwenye jamii yetu Tanzania tumekuwa na mikwaruzo ya hapa na pale kati ya islam and christianity mfano halisi ulikuwa ni ile hoja ya mahakama ya kadhi,issue ambayo imepelekea migawanyiko ambayo ni ideological lakini yenye kuingiliana na siasa za nchi moja kwa moja.....

Inawezekana kuna watafiti ambao wameona kuwa kuna kama pattern ama wave ya ideologies hizo kuwa spreaded kwenye nchi za Afrika na kupelekea machafuko na migawanyiko,hii ni kama kuna ushahidi wa wave kama hii kwenye nchi nyingine za kiafrika kwa wakati huu,hilo likiwa kweli kunaweza kuwa naimplication ya arrangement ama well planned and coordinated events. Alkaeda kwa kiasi kikubwa wameweza kuifanya vita ya jihad kuwa ni ya kisiasa,hilo ni wazi kwani kuna nchi nyingi tu ambazo ni za kiislam lakini zenye kudai kupingana na Alakaeda,hapo ni siasa tayari licha a kwamba Alkaeda wenyewe wanadai ni vita ya kidini na kusapotiwa na wengi,kama si wazi wazi bali hata kisiri kwa michangi nk. Bin Laden si mjinga kwani hata malengo halisi ni ya kisiasa licha ya kwamba ameyabebesha jina la jihad kuwa ni vita dhidi ya uislam,na ndiyo inayomfanya na yeye afanye mashambulizi ya kisiasa....


Kama Alkaeda ambao hata mashambulizi ya 911 walipata fedha kutoka misikiti ya Saudi,wanaweza wakawa wanaonekana mashujaa kwa wengi wa waislam na pia kuoenekana kama walifanikiwa kwa kiasi kikubwa dhidi ya wapinga uislam,hata ambao hawapingi uislam bali tu si waislam ama makafiri....Pesa hizo huletwa kama charity lakini zikipenyezwa kwenye mambo ya kiasiasa kwa kutumia mwavuli wa vita dhidi ya uislam ama jihad kwamba hatupewi haki,tunataka mahakama zetu nk,basi tatizo ni lazima litakuwepo. Extermism siyo jambo zuri,kama watu ambao walichangia 911 ndio hao hao wanaochangia misikiti ama institutions za kiislam za Afrika,then ni kivipi utaweza kutofautisha nia,ambapo hata maextremist wenyewe hawataki dini nyingine zaidi ya Islam na kwamba wengine wote ni infidels?Hapo ndipo penye ugumu ambapo mtu anaweza kuconclude kwamba nia ni ku eradicate christianity....

Badala ya fedha hizo kuwa radicalise watu,basi ni vyema zingetumika kuwaletea maendeleo. Waafrika ni muhimu sasa tujue kuwa hakuna manufaa yeyote kwa nchi zetu kutumika kama battle grounds za ideological warfares ambazo sasa its obvious zimekuwa political kutokana na kuwa injected kwenye political system kwa kuwaburuza watu bila kujielewa,wengi wao wakiamini kabisa kuwa ustawi wa dini yao uko hatarini.

Tatizo tulilonalo waafrika ni kwamba kwa level ya maendeleo bado tuko nyuma mithili ta time za kina Aristotle na kina Ptolemy,wakati ule ambapo kulikuwa na mapambano ya kikweli kati ya dini na sayansi,wakati dini ikiongoza maisha ya kila siku na hivyo kupelekea misuguano kwani sayansi ndio kwanza ilikuwa inachipukia,kina Kepler,Corpenicus na hata baadaye Darwin,mwanzo wa sayansi kuongoza ndio yalipoanzia,Corpenican Revolution amongst other revolutions ni mfano halisi,dini haikufa lakini sayansi na teknolojia vilitake over,sisi watanzania na waafrika kwa ujumla bado tunaongozwa na mambo ya kiimani zaidi ie religion na si science and technology,na ndio maana hata mkuu wa nchi anaweza kuja na kusema kukatika kwa umeme ni mambo ya Mungu na wananchi wakakubaliana naye.

Na kwahivyo ni kweli kabisa kuwa ni HATARI kwani uelewa wa wananchi kuhusu mambo haya ni mdogo kwani watu wanaongozwa na imani zaidi,kama si ya ukristo ni uislam na wengine uchawi ambapo wengine wana imani kabisa kuwa viungo vya albino ni dawa ya utajiri nk,mtu kama huyo hata akibadilika hakuna la maana kwa i either atakuwa muislam ama mkristo,hakuna fikra mbadala za kisayansi ili kuondokana na umasikini nk. Ili kuweza kuisadia Afrika ni lazima viongozi wake walitambue tatizo hili,mentality zao ni lazima zikubaliane na ukweli kuwa mechanism watakazozitumia si lazima ziwafurahishe wao wenyewe,sidhani kama Mh Rais aliposema kuwa ni mambo ya Mungu kukosa umeme alikuwa anamaanisha hivyo kiukweli,bali nadhani ameamua kula na kipofu,hajali,kama mambo ake yako safi na maisha ni mazuri basi mwingine atafix,almuradi yeye yuko madarakani na kwamba ni Rais.

Kama wanasiasa wetu wataendelea kuact kama wanavyofanya basi sitashangazwa sana machafuko yakitokea kwani ukosefu wa busara,uzalendo,mapenzi ya kweli na kuijuwa historia yetu waafrika vyema ni tatizo kubwa miongoni mwa viongozi wetu. Wengine wanaijuwa historia lakini hawajui namna ya kijifunza kutokana na historia.

Kwa kifupi viongozi wetu wangejikita kwenye kuwaletea wananchi maendeleo,kwani maendeleo huleta ustaarab na wastaarab hawawezi kuuana kwasababu tu ya utofauti wa dini.
 
Upuuzi mtupu...Ni nchi gani iliyokuwa ya Kikristu ama yenye mtawala Mkristu leo hii inatawaliwa na Kiislaam..
Ujinga huu wanauleta hawa viongozi wa dini.. Somalia, Sudan, Chad, na nchi zote kaskazini mwa sahara viongozi wake ni waislaam na wanaoteswa ni waislaam, iweje hoja hizi badala ya kuzingatia viongozi wabovu kwa tabia zao wanapenda sana kutumia dini za watu. Ni mawazo haya haya kuna watu wanayatumia kumhukumu Nyerere na Mkapa upande mmoja kisha Mwinyi na Kikwete upande wa pili pasipo kuelewa Tanzania ni nchi ilojengwa tofauti kabisa na nchi nyingine.. tazama nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda, Kongo ambazo kwa miaka yote zimetawaliwa na marais wakristu mbona sioni mtu akisema kanisa katoliki linafanya mbinu hizo hizo. Ni shutuma kama hizi hupelekea watu kuamini kanisa Katoliki linatumia fedha zake kuhakikisha watawala wa nchi za kusini mwa jangwa zinakuwa chini yao.. Sasa kama maneno haya ni kweli hamuoni umaskini unaojengwa na kanisa hili ktk nchi hizi?.. I mean kila nchi ya kiafrika ilojikita ktk Ukristu ndio maskini zaidi kuna kitu gani.

Sasa ukitaka kutazama picha ya Afrika kwa jicho hilo sidhani kama tutaweza kutafuta the real problem ambalo ni Viongozi wabovu kwani Uislaam ni sheria. Katiba ya Tanzania au nchi nyinginezo haijabalika na haitabadilika kwa misingi hiyo..hakuna mfano hata mmoja. ni katiba ile ile uweke Muislaam au mkristu isipokuwa haki za wahusika ni lazima zitazamwe kwa kufuata mjumuiko wao..Na hakuna kitu kibaya duniani zaidi ya kutumia mapungufu ya Uongozi bora ni kutumia dini zao wakati viongozi wote wabaya na mashenzi walikuwa na bado ni wakristu..toka kina Bokossa, Mobutu hadi Mugabe au hawa wana sababu nyinginezo...

Viongozi wa dini na hasa Katoliki sasa hivi wamefikia hatua za kurudisha mafundisho yao ya karne ya 14 zilizopita..Kujenga Uadui baina ya jamii ili kanisa lipate kutawala imani za watu kuliko dini yenyewe. Kwa Askofu mzima kutujmia neno WE LOVE MUSLIMS, but... ni upotofu mkubwa wa kiimani. Ni ujenzi wa chuki na kutoifahamu Biblia zaidi ya elimu ya Kukariri..kama yule Padre wa rwanda ambaye leo anakabiriwa na mashtaka makubwa. Kiongozi huyu wa dini ni mchafu, ni mbwa mwitu alovaa ngozi ya kondoo.. ni kiongozi mbaya anayetumia joho la kanisa kutangaza Ufirauni wake. Tumwogope, tumwogope kama UKOMA..
 
Hii hapa chini inaeleza kila kitu mkuu


-It is my hope that the Holy See appoints a permanent representative to the AU who should attend all the meetings whenever they take place and who could keep in personal contact with the Catholic members of that important institution,- Archbishop Souraphiel said.
-This special representative preferably would have diplomatic credentials comparable to the one of an Apostolic Nuncio,- he explained. .

Mbona hawaongelei chochote kuhusu membership hapo? Wanaongelea tu The Holy See i appoint mtu, kitu ambacho hata sasa hivi kinawezekana katika capacity yao kama observers?
 
Mitaa michafu ya umaskini haiwezi kuzaa watakatifu...Kuna gape kubwa sana kati ya walionacho na wasionacho ambalo limeendelea kukua kila kukicha,wachache wanaopata uongozi wanatumia nafasi zao kujilimbikizia mali kwa njia za kifisadi,jambo la kufurahisha Baba Askofu Mtega amegundua kwamba viongozi wa dini hawa kufanya kazi yao sawasawa kwa kutowahubiria viongozi wa serikali ,ndio maana anasema;

Required: Deeper evangelisation, advocacy and prophetic voice to our governments...

Nafikiri umefika wakati viongozi wa dini wakaacha kulalamika badala yake waanze kazi yao ya kuwarudisha viongozi wetu wa serikali za kiafrika katika maadili ya kweli kwa kuwahubiria na kuwahudimia kiroho,maana ni vigumu sana kuondoa ufisadi kwa kulalamika tu ama ndani au nje ya nchi.
 
Watanzania ni lazima tujuwe kuwa si dini ndiyo itakayotuondolea matatizo yetu,matatizo waliyonayo wananchi wengi bado ni yale basic,kama vile chakula,maji,matibabu nk. Wananchi kama hao hawahitaji complications za ideology,wanahitaji mobilization kwa kutumia mbinu mpya za kisayansi ili kuondokana na umasikini,maradhi na ujinga. Huwezi ukaomba Mungu tu bila kutunza mazingira ukitegemea mvua na hali nzuri ya hewa,kadhalika maendeleo huletwa na jitihada za pamoja na si migawanyiko ya kiimani ambayo in return inaturudisha nyuma tu.
 
Back
Top Bottom