Sylvester Rwegasira wa TRAWU hatunae tena

RIP Rwegasira mtetezi wa wanyonge ukapumzike kwa amani!.... Ndugu zanguni kusema ukweli napata mashaka sana na kifo cha huyu mpiganaji wa wanyonge kila nikijaribu kutafakari naona kama vile kuna kukolimbwa hapa yaani mtu unaenda mkutanoni kutoa tamko juu ya hatma ya TRL na Serikali then unatutoka ghafla mmmh!

kama kweli ni Mwenyezi Mungu amemchukua kwa mapenzi yake ampumzishe kwa amani ila kama kuna kukolibwa huyo alietenda hayo chamoto atakiona maana machozi ya mnyonge yatamuhukumu hapa hapa duniani!
 
Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mpiganaji huyu, sina jingine ila ni kumuombea kwa mungu apate malipo kwa mema aliyoyafanya, M/Mungu wape moyo wa subira familia yake kwa msiba mkubwa walioupata.
 
Inna lillah waina illaiya rajiuun...yeye ametangulia na sisi tutafuatia,dunia ni mapito jamani tuishi vyema jamani na tuijenge dunia kama tutaishi milele au tujiandae kwa maisha ya akhera kama vile tutakufa kesho......
ni hayo tu!
 
Hii kuvamia vifupisho kazi kweli! Sasa na wewe hiyo LOL ina kazi gani hapo?
Nadhani alitaka kusema ile Loooo! ya masikitiko ya Kiswahili, akajikuta anasema nimecheka sana!

Duuu, huu msiba aisee najipa pole mwenyewe, maana kama unaipenda nchi yako hapa wengi tumepata pigo, sio familia yake tu.
 
RIP comrade Sylvester Rwegasira. Ulionyesha kwa vitendo kwamba haki inatafutwa, tena wakati mwingine kwa kuwa mkali kwa wale wanaotaka kuibana. Lakini pia ulikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa mali za TRL hazichukuliwi na wawekezaji uchwara wa RITES. Hukumung'unya maneno ulipotamka kuwa wawekezaji wa RITES wanachukua engine zetu zile zile na kuzifanyia ukarabati kidogo na kizitumia badala ya kuleta engine mpya kama makubaliano yalivyokuwa. Lakini pia kudhihirisha kuwa lile wanachokifanya kinaweza kufanywa na mafundi wetu wazalendo, mafundi karakana wa Morogoro walijitolea kufufua baadhi ya engine pale Moro wakakualika uende kuzizindua na ukaenda. Hakika umetuacha na majonzi makubwa lakini pia umetuachia fundisho kuwa ni lazima kuwatetea wanyonge na kujali maslahi ya nchi bila woga. RIP COMRADE
 
Back
Top Bottom