Sylvester Rwegasira wa TRAWU hatunae tena

RIP kamanda Rwegasira watanzania hawatakusahau kwa kuwaongoza wafanyakazi kumfukuza mwekezaji wa kihindi pale TRL na kama sikosei ndio mwekezaji wa kwanza kufukuzwa kwa nguvu za wafanyakazi
 
RIP Rwegasira! You will be remembered for your efforts
in improving the living conditions of the workers
 
Wakat naangalia news za huu msiba machoz yalinitiririka ghafla, kweli huyu alikuwa kipenz cha wafanyakaz wa secta zote, kama ni mkono wa mtu bas huo mkono utachukua wengi RIP KAMANDA, TUTAKUKUMBUKA DAIMA.
 
hakika Tanzania tuna kazi, ukionekana wewe uko agaist with government, basi tegemea lolote. Nadhani ifike mahali taifa litambue kuwa nchi ni yetu sote. Rwegasira tangulia tutakukuta
 
KATIBU Mkuu wa Chama Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), Silyvester Rugwesira, amefariki dunia muda mfupi kabla ya kutoa tamko kuhusu kikao kilichokuwa kifanyike makao makuu ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) jana saa 4:30 asubuhi.Rugwesira alikuwa maarufu kutoka na ujasiri katika kuwatetea wafanyakazi wa sekta hiyo na hasa wa TRL.

"Ni vigumu kuamini … lakini ukweli utabaki pale pale kwamba, Silyvester ambaye alikuwa tegemezi katika kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi wa reli, hatunaye tena duniani," alisema mmoja wa wafanyakazi wa reli.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwa marehemu, mkewe, Anna Njau alisema, Rugwesira alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo.

Alisema wiki iliyopita alipeleka katika Taasisi ya Moyo Tanzania (THI) kwa matibabu."Hata hivyo hatukumkuta daktari aliyekuwa akimtibia tangu awali na badala yake, alifanyiwa vipimo na kupewa dawa za kutuliza maumivu na kurudi nyumbani,"alisema Anna.

Alisema baada ya kurudi nyumbani, hali ya mumewe ilianza iliimarika zaidi.Alisema ilipofika saa 2:30 jana asubuhi, asubuhi alimtayarishia uji akanywa na kwamba baadaye, alitemngea maji ya kuoga, ili ajiandae kwenda kwenye kikao.

"Alipomaliza kunywa uji alingia bafuni, lakini ghafla alitoka baada ya kuanza kujisikia vibaya. Alijitupa kwenye kochi lililokuwa sebuleni huku akipepesa macho. Tulimchukua na kumpeleka katika Hospitali ya Dar Group,"alisema Anna.Alisema wakiwa njiani, hali ya mumewe ilizidi kuwa mbaya na kwamba ilipofika saa 2:30 asubuhi, alifariki kabla hajafikishwa hospitalini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Trawu Bakari Kiswala, aliliambia gazeti hili kuwa marehemu alikuwa akisumbulia na maradhi ya moyo na kisukari.Kwa mujibu wa Kiswala Alhamisi iliyopita alipelekwa katika Hospitali ya Hindu Mandal, ambako alilazwa kwa mapunziko.

Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake ya Trawu,Rose Mwambe alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwa wanachama.
 
Poleni wafanyakazi wa Reli,poleni wapenda haki wote nchini,kweli kizuri hakidumu!
 
Dah!! tumepoteza moja ya nguzo(mpiganaji) muhimu katika utetezi wa haki za wafanyakazi na maslai ya nchi.pole kwa wafanyakazi wote.Mola ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.
 
huyu jamaa na mgaya wa TUKTA walikua imara sana katika kusimamia maslahi sema walikosa support tu ya wanaowaongoza kutokana na wengi wao kua na hali ya woga!
Dah!! tumepoteza moja ya nguzo(mpiganaji) muhimu katika utetezi wa haki za wafanyakazi na maslai ya nchi.pole kwa wafanyakazi wote.Mola ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.
 
Upumzike kwa AMANI - Wewe ni mmoja wa "Wapambanaji wa Kweli" ...

Mungu uwapenda wema - Mungu agonza abarungi
 
Dah wafanyakazi tumekwisha!!!! Katika jamaa niliokuwa nawapenda katika kutetea haki za wafanyakazi huyu namba wani kha R.I.P kamanda. Wafiwa poleni sana
 
Back
Top Bottom