Swimming Pool Dar inapatikana wapi?

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,493
2,247
Jamani nina wageni wametoka nje wanataka kwenda sehemu yenye swimming pool wakaogelee, mahoteli yote naona mpaka uwe unakaa ndo unaruhusiwa kuogelea, mwenye kujua pool ambayo unaweza kwenda kuogelea kwa kulipia anitonye.
Najua kuna kule Wet & Wild lakini mbali sana, kama ingekua mitaa ya mjini ingekuwa bora zaidi.
Ahsanteni
 
wewew vipi banaaa?wa wapi wewe?
hebu nenda WIT 'N WILD ukaogelee na watoto wenzio
 
Mkuu swimming pool nzuri na public ni ya UDSM, wanalipia kidogo lakini
 
Jamani nina wageni wametoka nje wanataka kwenda sehemu yenye swimming pool wakaogelee, mahoteli yote naona mpaka uwe unakaa ndo unaruhusiwa kuogelea, mwenye kujua pool ambayo unaweza kwenda kuogelea kwa kulipia anitonye.
Najua kuna kule Wet & Wild lakini mbali sana, kama ingekua mitaa ya mjini ingekuwa bora zaidi.
Ahsanteni

...keshawaambia anapajua Wet & Wild ila mbali, nyie mmemng'ang'ania kumtajia huko huko,...:D ...'DAWASCO' watu wabaya sana hawa!

Ukivuka kwa pantoni unaweza kula raha South Beach kule, kuna mahoteli yenye pools nzuri tu. Hizi za 'watalii' tutabakia kupigia picha za kumbukumbu tu tena kwa mbaaaali!

Exterior_G_1.jpg

Royal Palm/Movenpick.​


pool.jpg

Kilimanjaro Kempinski​
 
nenda mission to seamen/seafarers ambayo ipo baada ya bendera tatu - inapoanzia kilwa road karibu na mlango wa kuingilia bandarini. ni shilingi elfu tano tu kwa mwogeleaji/msindikizaji kwa siku.

macinkus
 
Kweli nenda UDSM au kama vipi we nenda Kunduchi sio mbali
 
Unaweza kwenda Splash Town (hoping bado ipo).

Jinsi ya kufika hapo:
Ukiwa Old Bagamoyo Road, ingia barabara inayoelekea Msasani Beach Club. Kata kushoto mtaa wa kwanza, Splash Town ni ya pili upande wa kulia.

Vilevile, unaweza kwenda Baobab kule Masaki.

Au unaweza kwenda Mambo Club Oysterbay Mkabala na Karibu Hotel????.

Hizo sites zote hapo juu nilizozitoa ni kwa mujibu wa kumbukumbu zangu za miaka kama mitatu hivi iliyopita.

Swimming Pools za mahotelini unaweza ukazitumia lakini ni lazima uwe mjanja kidogo, ukienda kisamaria hukatizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom