Sweden yaipa Tanzania Sh. bilioni 44 kusambazia umeme vijijini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,041
Serikali ya Sweden imesaini mkataba wa kuipatia Serikali ya Tanzania Sh.bilioni 44 kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo jana na Serikali ya Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhani Khijjah, alisema msaada huo utasaidia kuondoa umaskini kwa wananchi vijijini pamoja na kuendeleza uchumi wao.
Alisema ni asilimia moja tu ya wananchi wa vijijini wanaofaidika na umeme unaozalishwa nchini.
Alisema lengo la msaada huo ambao umetolewa kupitia mfuko wa Uendelezaji wa Nishati ya Umeme Vijijini (Rea) ni kufanikisha Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini (Mkukuta) na kuendeleza Kilimo Kwanza sehemu za vijijini.
Khijjah alisema umeme huo utawezesha pia kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa ajili ya utengenezaji wa mazao ya wakulima vijijini pamoja na kuongeza ajira. Khijjah aliongeza kuwa uanzishwaji wa viwanda sehemu za vijijini utasaidia pia kuongeza thamani ya mazao.
Alisema malengo ya kufanikisha Kilimo Kwanza hayawezi kufikiwa endapo hakutakuwepo mpango madhubuti wa kufanikisha umeme vijijini na kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa wakulima. Aidha, alisema jambo kubwa ambalo limekuwa likichangia wakulima vijijini kutofikia maendeleo ni ukosefu wa umeme. Alisema mikoa 16 ya Tanzania bara ndio inatarajia kunufaika na mradi huo.

CHANZO: NIPASHE

Je Serikali itasambaza umeme vijijini? kama huo msaada Serikali ya Tanzania iliyopewa na Sweden? au ndio hizo pesa zitwafikia Mafisadi? Nawaombeni mnijibu Wakuu wenzangu.
 
Tatizo sio fedha. Tatizo ni TANESCO inahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo na ya kiutendaji. umeme haugawanjwi bure, tunalipia wanashindwa nini kusambaza umeme. Tanesco imefikia ilipo kutokana na ufisadi, mawazo mgando ya uongozi wake.Hizo fedha watazichakachua hazitafanya chochote!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Rai yangu kwa Serikali ya Kifalme ya Sweden; Chonde simamieni wenyewe zoezi zima la sivyo zitachachuliwa na walengwa hawatafikishiwa huduma!
 
ohh no! pesa zote zitaishia kwenye administration hizo! africa ni laana tupu!
 
Vijiji vipi? Wasahau si ajabu zishaingia kwenye accounts za mafisadi. Mara ngapi tumeambiwa hayo?
 
Serikali ya Sweden imesaini mkataba wa kuipatia Serikali ya Tanzania Sh.bilioni 44 kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo jana na Serikali ya Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhani Khijjah, alisema msaada huo utasaidia kuondoa umaskini kwa wananchi vijijini pamoja na kuendeleza uchumi wao.
Alisema ni asilimia moja tu ya wananchi wa vijijini wanaofaidika na umeme unaozalishwa nchini.
Alisema lengo la msaada huo ambao umetolewa kupitia mfuko wa Uendelezaji wa Nishati ya Umeme Vijijini (Rea) ni kufanikisha Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini (Mkukuta) na kuendeleza Kilimo Kwanza sehemu za vijijini.
Khijjah alisema umeme huo utawezesha pia kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa ajili ya utengenezaji wa mazao ya wakulima vijijini pamoja na kuongeza ajira. Khijjah aliongeza kuwa uanzishwaji wa viwanda sehemu za vijijini utasaidia pia kuongeza thamani ya mazao.
Alisema malengo ya kufanikisha Kilimo Kwanza hayawezi kufikiwa endapo hakutakuwepo mpango madhubuti wa kufanikisha umeme vijijini na kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa wakulima. Aidha, alisema jambo kubwa ambalo limekuwa likichangia wakulima vijijini kutofikia maendeleo ni ukosefu wa umeme. Alisema mikoa 16 ya Tanzania bara ndio inatarajia kunufaika na mradi huo.

CHANZO: NIPASHE

Je Serikali itasambaza umeme vijijini? kama huo msaada Serikali ya Tanzania iliyopewa na Sweden? au ndio hizo pesa zitwafikia Mafisadi? Nawaombeni mnijibu Wakuu wenzangu.

Hizo fedha zitatafunwa tu. Unaona hela ni za kusambaza umeme vijijini inakuwaje ziende kuendeleza kilimo kwanza? Ina maana Kilimo kwanza ni umeme? Tunahitaji kujua idadi ya viji na kaya zilizopata umeme kutokana na fedha hiyo. Zisije ishia katika Per Diem kwa wakuu wakifanya upembuzi yakinifu.
 
Kwa kweli hizo pesa wakipewa TANESCO zitaishia mifukoni
Mwa vigogo wachache. TANESCO kwa muda mrefu sasa imekuwa haitumii
Gharama zake gharama zake kusambaza umeme lakini cha kushangaza
Unapokwenda kutaka kusambaziwa umeme ukienda pale utazungushwa
Mwisho wake wanataka pesa. Utakuta kuna eneo lina wakazi wa kutosha
Wanaomba umeme na wanaambiwa watapelekewa kama project,
Na ili kufanikisha hili wanataka uwape rushwa ya atleast 6M.
Mfano pale ilala kuna mtu anaitwa MUSHI, huyu ni kinara wa rushwa.
Yuko idara ya planning. TAKUKURU inabidi iingilie kati suala hili.
Ikasafishe pale.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom