MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Wakuu mimi nina swali na nina uliza kwa kwa uzuri tu katika kufahamu zaidi nini kipo ndani ya mawazo, fikra na mioyo ya Watanzania. Chadema imetoka kupata washabiki wengi sana ndani na nje ya JF. Baadhi ya hawa mashabiki ni wanachama rasmi nikimaanisha wale wanao shikilia kadi za chama na kuna wale ambao wana support Chadema lakini si wanachama rasmi.
Swali langu haswa lina lengi supporters wa Chadema ambao si wanachama rasmi. Nieleweke kwamba sina neno na mtu kuwa mshabiki wa chama fulani bila kuwa mwanachama rasmi. Ni ukweli usiopingika kuwa nchi nyingi chaguzi hushindwa kwa kuvuta "independence" au wale wasio wanachama. Kwa maana mtu akishakua mwanachama huna haja ya kuuza sana sera za chama kwao kwani tayari wana zielewa na ni matumaini yangu wana ziishi.
Sasa swali langu ni je mashabiki wa Chadema ambao si wanachama bado wataendelea kuwa mashabiki pindi Chadema itakapo bahatika kushika madaraka? Je CCM ikisha anguka adui atakua nani? Je kama Chadema ikibahatika kushika madaraka na waka chemsha na wao kimbilio litakua lipi? Nauliza hivi kwa sababu kuna tofauti kati ya kuwa pro-Chadema na anti-CCM. Kuwa pro-Chadema ina maana wewe umeiva uana Chadema na upo nacho kwa hali yoyote. Kuwa anti-CCM ina maanisha wewe haufuati itikadi zozote bali lengo ni kuiona tu CCM ikiondoka na hata kesho kikitokea chama kingine cha upinzani chenye nguvu basi utahamia huko.
Nauliza swali kwa sababu ukweli utabaki pale pale kwamba katika vita yoyote kuna wale wanajeshi ambao unao tokea mwanzo na ambao wata pambana na wewe hata kama mnaelekea kushindwa vita. Na kuna wale watakao jiunga kwa kuangalia upande gani unashinda na wanakua na haraka sana kuhama pale vita inapoelekea kuelemea kwa upande wa pili.
Natambua wengi watashambulia hii mada kiunafiki kwa kutaka kuonekana kweli wana mapenzi ya dhati na Chadema na kwamba wao ni wana Chadema damu damu. Wapo wale wanachadema halisi ambao watakuja juu na nita waelewa. Lakini pia wapo wale ambao watakejeli mioyoni wakijua fika wao ni wanafiki wanaofuata tu upepo unapo kwenda. Nia ni kuamsha hisia za watu na kupima mawazo ya Watanzania wenzangu.