SWALI , Wanaume jadilini wanawake jibuni

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Umeolewa na una mtoto mmoja, mumeo ana rafiki yake wa kiume mpenzi .
Urafiki ambao sometyms huitwa urafiki ndugu, (lake lako , lako lake )
Mko garini mnasafiri Wewe , Mumeo , Mtoto , na Rafikie Mumeo (Shemejio).
Katika safari hiyo mnapata ajali , mzinga wa kisawasawa.
Ajali hiyo inamuachanisha Mumeo na maisha ya Dunia , mliobaki watatu zenu bado.
Msiba umekwisha na mwaka mmoja umepita , aliyekua rafiki kipenzi wa Mumeo (ambae mpaka muda huo ni Msimbe ) anakutokea na option.
Option hii anakwambia "Shemeji nimekaa na kufikiri namna ya kukusaidia mentality na fiziko (physically)
ni vema na napendelea nikuoe ndiyo the only way ya msaada wangu kwako! Kwani Nyoka wa mbali haui Fimbo !
Nina imani kwa jinsi ya ukaribu wa mimi na Marehemu ni lazima ninakua na umuhimu au deni la kukutunza wewe na mwanao"
Je ? Wewe Dada jichukulie wewe ndiyo mjane lengwa hapa , hii option unaipokeaje ? Unamjibuje Shemejio ?
 
"Nyoka wa mbali Haui fimbo" teh nimepapenda hapo ulipogonga kireverse....
 
Kinachowaweka watu wawili kwenye ndoa sio 'huruma' bali ni mapendo na mapenzi. Maana huruma itakapoisha ndio visanga vitakapoanza!
Pili ile heshima na hofu ya ushemeji haitokaa itoke kwangu (labda ndio ninavyoulinda moyo wangu na vishawishi vya shemeji wakware). Sithubutu kumvulia nguo na mume wangu anahisi ataniona na kunishangaa huko aliko!
Kwa majibu hayo mawili, shemeji hawa watoto ni wako wasaidie unapoweza. Mie mkubwa nitajiju, hapana ahsante!
 
nitamwambia tu....sitaki...

Una Msimamo ..safi sana

Kinachowaweka watu wawili kwenye ndoa sio 'huruma' bali ni mapendo na mapenzi. Maana huruma itakapoisha ndio visanga vitakapoanza!
Pili ile heshima na hofu ya ushemeji haitokaa itoke kwangu (labda ndio ninavyoulinda moyo wangu na vishawishi vya shemeji wakware). Sithubutu kumvulia nguo na mume wangu anahisi ataniona na kunishangaa huko aliko!
Kwa majibu hayo mawili, shemeji hawa watoto ni wako wasaidie unapoweza. Mie mkubwa nitajiju, hapana ahsante!​

Vizuri sana....
 
Kinachowaweka watu wawili kwenye ndoa sio 'huruma' bali ni mapendo na mapenzi. Maana huruma itakapoisha ndio visanga vitakapoanza!
Pili ile heshima na hofu ya ushemeji haitokaa itoke kwangu (labda ndio ninavyoulinda moyo wangu na vishawishi vya shemeji wakware). Sithubutu kumvulia nguo na mume wangu anahisi ataniona na kunishangaa huko aliko!
Kwa majibu hayo mawili, shemeji hawa watoto ni wako wasaidie unapoweza. Mie mkubwa nitajiju, hapana ahsante!

King'asti ! But refar huyu ni aliyekua Rafiki tu wa Mumeo, na hawana muungano wa damu.
 
Huwi na mtu kwasababu unamuhurumia ila unampenda, kwasababu huruma huisha lakini upendo hudumu.
 
Kuna makabila hapa Tanzania wana mila za kurithi mke wa kaka kama amefariki. Naomba mnitajie makabila hayo tafadhali.
 
Mmmh! Labda kama nilikuwa nammezea mezea mate kabla husband hajafa. Lol
 
Hata kama alikuwa rafiki tu, ushemeji ubaki pale pale, ndo akiba ya undugu. Hata nikisumbuliwa na mume mupya nakuja kuomba ushauri kwake hehehe
King'asti ! But refar huyu ni aliyekua Rafiki tu wa Mumeo, na hawana muungano wa damu.
 
nashindwa kujadili bila kujibu...
ngoja nisubiri kudesa!!!

Mantik ya wanaume WAJADILI iko wazi wanaume HAMUOLEWI !
Wanawake WATOEJIBU ndiyo WAOLEWAO !
Pasipo na mlio ngoma utaichezaje ?
 
Back
Top Bottom