Swali lisilojibiwa: Ndege ya Qatar iliwezaje kutua KIA?

Kwa kuleta hii kesi mahakamani, serikali imekiri kuwa kuna ndege iliingia nchini aidha kwa kufuata sheria au kinyume cha sheria. Lakini ingekuwa ni ndege ya kiraia hilo lingekuwa kashfa tosha lakini kuwa ni ndege ya kijeshi ni kashfa mabayo kama waandishi wetu wangekuwa na ujasiri wangetaka maelezo toka JWTZ.. muone watu wanavyoweza kujiuma uma meno!! Hii ni kashfa kubwa kweli ambayo Dr. Hussein Mwinyi anatakiwa aitolee maelezo.
Hivi huyu hussein na yule mama aliyekuwa anauza wanyama pale ikulu miaka ya nyuma wana uhusiano wowote?! Anakumbushia alichoona wazazi wanafanya!! Ndege ya jeshi la nje haiwezi kutua nchini bila jeshi letu/wizara ya ulinzi kuhusika. Huyu mtu huyu ni JANGA KWA TAIFA, msijesema hatukujua...
 
Kila kitu kinajibika ila naona tunajadili newspaper article ambo ilikuwa poorly written

Hakuna basic facts na imekuwa kama mtego vile wa waandishi kutaka kupima akili za wana JF

Unless watu wa WANYAMAPORI na UTALIII na JESHI LA POLISI watoe statement lakini hii kujadili newspaper article iliyoandikwa na huyu mwandishi anayeoonekana kama vile anaandika news kwenye gazeti la Primary school is just beyond ridiculous
 
hawa jamaa wameiba sasa wameamua kuamisha nchi.
hapa hakuna siri wote wanajua kuanzia mkuu wa kaya
mbona tausi wetu waliuzwa wakati wa utawala wa mzee rukusa
waziwazi .
hii nchi nilishasema mwanzo jk anapotosha na huyo mzee rukusa
mke usije kuta ndiye muusika mkuu maana mama anawataja wa kila
aina huko arabuni.
swali sio hiyo ndege kutumia tanzania ila ilitokaje huko QATAR bila sekarali ya
Qatar kujua kwamba wana dege lao limeelekea bongo?
ni wazi kulikuwa na mawasiliano ila tu mission imeingia mchanga,
isitoshe unaweza kuta hiyo ndege imeleta mzigo hapa ambao hatujui pia au kuondoka na vitu
vingi zaidi ya hao wanyama.
jk atoke IS TOO MUCH NOW!!!!!!!!!

Hiviii, tangu waanze kuuzauza, kubiNAFSisha... kuibiwa, kuten % na yanayofanana na hayo, tumebakiza chenji yoyote ili tuambulie japo mchuzi au tutafute pa kwenda?
 
Mwanakijiji hii ndege inaonekana ilitua uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA? Swali lingine ni kwa vipi wanyama kama Twiga waliweza kusafirishwa kutoka mbugani hadi uwanja wa ndege? Hapo ndo utajua kwamba nchi yetu ina polisi wa kuwaua raia wema na watanzania wasio na hatia na si kwa ajili ya ulinzi wa mali zetu. Wakati huo huo jeshi la wananchi likifanya mazoezi ya kuwafyatulia mabomu wananchi (Mbagala, gongolamboto) badala ya kupambana na majangili. Ni bahati mbaya kubwa sana kuzaliwa kwenye nchi kama Tanzania.
 
Ile radar ya chenge ishakufa nini? hizo deal inaonyesha zinapigwa siku nyingi hii imekua kama coincidence tu..
 
Kwa hili ina maana kwamba nchi iko uchi kimaadili,kitaaluma,kiuwajibikaji na hata katika viwango wa kawaida tu vya kufikiri. Inakatisha tamaa hali kuwa hivi.
Hivi mtu akituuliza hali yetu ki usalama ikoje kama mambo yenyewe ndio yako hivi, tuna haja kweli ya kuwa na mlolongo wa wana usalama wote hawa?
Tukianza na usalama wa taifa (wazushi), wanajeshi na ofisa wanyamapori wenyewe.

Bora katika hili naweza kuwasifia polisi ambao ndio waliotoa taarifa hizi mwanzo baada ya polisi mmoja kutukanwa mbele ya wageni kwamba asiingilie kazi isiyomuhusu na afisa wa wanyama pori.

Kwa hili Waziri wa ulinzi, na wazima mwenye dhamana ya wanyama pori na usalama wa taifa wote wawajibishwe.

Lakini bahati mbaya nchi ya kishemeji hii hakuna chochote kitakachofanyika.
 
Hamuelewi nini enyi waTz? ccm ni wajinga kuongoza nchi, sio kuibia nchi. Hii ishu baada ya kuonekana imeshagundulika, ikawa lzm izuiwe isihojiwe. Lzm CDM wangembana waziri mkuu, na wazir mhucka. So mbinu ilikuwa simple, peleka mahakamani. Na yeyote atakayehoji leo Makinda atamwambia suala liko mahakamani, so haturuhusiwi kulijadili. baada ya hapo sikilizia litakavyomalizwa huko mahakamani...
 
Sina shaka kwamba ndege hiyo ilifuata taratibu za kuingia nchini, hivyo ilikuwa pale kihalali. Tatizo naloliona ni aliyetoa kibali hicho cha ndege kubwa ya kijeshi kama hiyo kuingia na kutua nchini alizingatia vigezo vipi? kwa kuwa alipaswa kutilia shaka maombi hayo na kuinyima kibali kama kweli anafanya kazi yake kwa kuzingatia sheria, utaratibu na common sense pia.Kwa kuwa mtoa kibali hakutumia common sense ana wajibu wa kutujibu watanzania kwa nini hakutumia common sense, na tuanzie hapo kuwakamata wahusika wote. Pili, wizara yetu ya mambo ya nje isikae kimya kama ilivyokaa kimya kuhusu suala hili, huu ni mgogoro wa kidiplomasia pia, hivyo lazima itoe kauli na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuhitaji twiga hao warudishwe nchini mara moja, na waarabu wote waliokodishwa viunga vya wanyama loliondo mikataba yao isitishwe mara moja na wote wafukuzwe nchini mara moja. Kama hatua zote hizi hazichukuliwi basi kwa kutumia common sense nitakuwa sina budi kuamini kwamba viongozi wajuu wa serikali ni wahusika wakubwa wa wizi huu, na wale ambao wamefikishwa mahakamani ni dagaa tu, kambale wapo nje huru.

Ni kweli, Mugabe angeweza kufanya hivyo (hapo kwenye RED)..

Ipo siku, tutapata wawajibikaji
 
Kila kitu kinajibika ila naona tunajadili newspaper article ambo ilikuwa poorly written

Hakuna basic facts na imekuwa kama mtego vile wa waandishi kutaka kupima akili za wana JF

Unless watu wa WANYAMAPORI na UTALIII na JESHI LA POLISI watoe statement lakini hii kujadili newspaper article iliyoandikwa na huyu mwandishi anayeoonekana kama vile anaandika news kwenye gazeti la Primary school is just beyond ridiculous

Basic facts gani unazozitaka?
Unafikiri sisi wote ni waandishi au wahariri?
Tunajadili transparency na uwajibikaji wa mamlaka husika kulishughulika tatizo..Na kama kesi iko mahakama ni obvious hili tukio lilitokea.
Haiwezekani ndege ya kijeshi inaingia na kutoka bila watu kutilia mashaka!...
 
sasa mjanadili facts au poorly written newspaper article isiyo na fact yoyote?

Poorly written article - what exactly do you mean ndugu SlidingRoof? Kwamba ukisoma hiyo article hauoni/huwelewi ni kitu gani kimeandikwa?!!! Hivi inawezekana kweli hii article haina facts?

Mwandishi ametaja kuwa ndege ni ya kijeshi toka Qartar, imetuwa KIA, ametaja idadi na aina ya wanyama waliosafirishwa pamoja na thamani, pia ameeleza kuhusu kesi iliyofunguliwa dhidi ya watuhimiwa wa sakata hilo (including nchi walikotoka). Sasa wewe unataka facts gani?

Kusema kwamba watu wanajadili poorely written article your are in my view missing the point. Nijuavyo mimi hapa jamvini watu wanajadili hoja kwa maana ya contents na siyo style. Nashauri usome tena hii article and this time around try to be more attentive.
 
Poorly written article - what exactly do you mean ndugu SlidingRoof? Kwamba ukisoma hiyo article hauoni/huwelewi ni kitu gani kimeandikwa?!!! Hivi inawezekana kweli hii article haina facts?

Mwandishi ametaja kuwa ndege ni ya kijeshi toka Qartar, imetuwa KIA, ametaja idadi na aina ya wanyama waliosafirishwa pamoja na thamani, pia ameeleza kuhusu kesi iliyofunguliwa dhidi ya watuhimiwa wa sakata hilo (including nchi walikotoka). Sasa wewe unataka facts gani?

Kusema kwamba watu wanajadili poorely written article your are in my view missing the point. Nijuavyo mimi hapa jamvini watu wanajadili hoja kwa maana ya contents na siyo style. Nashauri usome tena hii article and this time around try to be more attentive.

Huyo jamaa atakuwa ni mwalimu wa shule za uandishi wa habari!! ndo maana anacriticise!
Sijui alitaka facts gani?
 
je nikweli ndege ya jeshi iliagizwa nchini kwa nguvu ipi?mana huwezi tua katika nchi yoyote duniani na kutekeleza uhalifu pasipokuwepo mkono wa mwenye nchi. Je ni kweli wale watuhumiwa ndio hasa waliokula njama za kutorosha nyara izo pasipokuwepo watu wazito {vigogo} nyuma yao? Mi nadhani kuna siri ambayo ipo Nyuma ya hawa wanaotuhumiwa.


Hii kama siyo kashfa basi ni ufisadi mwingine mkubwa ambao tunahitaji majibu haraka kutoka kwa akina Membe, Mkuu wa Majeshi, mkuu wa jeshi la Polisi na usalama wa Taifa. Mimi sipati shida sana na hizo nyara kwa sababu ni za huku nchini ila swali langu ni vipi dege kubwa la Jeshi likatua KIA bila hao wakuu niliowataja kujua lolote. Ndugu zanguni hii ni syndicate ambayo ina chain ndefu ya vigogo ila kitakachofanywa hapa ni akamatwaye na ngozi ndiye mwizi. Gaudence Temu ambaye ni mkurugenzi wa SWISS PORT na na wakuu wa KADCO inabidi wabanwe kiutu-uzima la sivyo hii ni dharau kwa usalama wa nchi yetu. Ina maana hii nchi haina usalama au na kama ni hivyo basi kuna mambo mengi sana yanafanywa humu bila serikali kujua
 
JWTZ wana wweza kuwa na jibu la ndege ya Jeshi ilivyo ingia na kama hawana jibu basi huu mpango wa kutorosha wanyama umeratibiwa na Tasisi nyingi sana za Serekari likiwemo JESHI Pamoja na Mkuu wa Kaya. Make kule katari ndo marafiki zake wamejaa
 
Kama kawaida watatafutwa kina Maranda wengine na vyombo vyote vya habari vitawashikilia hao mpaka wahakikishe tumesahau, hata ikibidi kuwafunga kidogo watafungwa ila hakuna atakaye jibu.
 
Shukrani ziwaendee Raiamwema kwa kuibua wizi huu. Hii habari isingeibuliwa,wangeipotezea kwa kisingizio cha kukosa ushahidi. Vilevile sitashangaa kama watashinda kesi yao (kama Zombe) maana inaonekana hii ni kazi ya mtandao mkubwa sana. Ni muhimu kesi hii ikafuatiliwa kwa ukaribu sana na wanahabari, wanaharakati na wote wanaoitakia mema nchi yetu, ili kuhakikisha haki inatendeka. Pia wabunge washinikize viongozi wawajibike kwasababu ile tu kufikishwa mahakamani inaonekana kosa limetendeka na watu hawakuwajibika ipasavyo.
 
Mwe! Hii ni nchi au danguro! Natumai hata kwenye madanguro kuna japo utaratibu unaofuatwa, vipi leo jeshi, usalama wa taifa, na minyororo mingine ikaye kimya kama kondoo wa sufi anayenyolewa ili hali uporaji ni wa kiwango hiki, na ukifanywa mchana kweupe.
Wazee wa magamba wakijiandaa na majibu mepesi kwa maswali magumu. Kazi kweli kweli.
 
Japo nimesema kuwa sitaki kuandikia mambo ya uchunguzi tena; hili nalo linanifanya nifikirie maana documents ambazo zimepitishwa kona hizi zinatisha! ooh well.. !!
 
For so many years ndege za kijeshi from Arab states are caming to KIA to bring Aid to JWTZ so may be this one got to KIA with Aid cargo and left with wanyama pori.
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom