Swali la Shyrose kwa Sophia Simba lazua kasheshe katika Mkutano Mkuu UWT

Hongera SS sasa anza kumshughulikia S. Banji asipate hata kazi ya kufagia popote pale,analeta mazarau ee!
 
ubaya wa hilo swali uko wapi?
Au ndo ubabe wa sophia tu?

Kama Sophia angekuwa kiongozi makini angekuwa mvumilivu akamjibu kwa ustaarabu na unyenyekevu. Swali hili lingemjenga sana kama asingekurupuka na kujibu kihuni. Ajifunze kutoa kwa wana CDM wanavyokabiliana na maswali ya kejeli, lakini hili ni swali la msingi.

" JE MHESHIMIWA SIMBA, KAMA MWENYEKITI WA CHAMA, NI LINI AU WAPI UNGEKUWA TAYARI HATA KUFA KUKITETEA AU KUKIPIGANIA CHAMA?"

hili ni swali la kawaida kabisa? inaonyesha udhaiifu wa ccm na jumuia zake zote katika kuchagua viongozi na kufanya maamuzi.

images
images

Shyrose Banji mjumbe wa mkutano mkuu umoja wa wanawake Tanzania ambaye pia ni mbunge katika bunge la Afrika Mashariki amenusurika kufukuzwa kwenye mkutano wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo baada ya kumwuliza swali gumu Sofia Simba kama ifuatavyo:
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Wafuasi wa Simba walilipuka kama gas iliyoshika moto kwa kutaka atolewe nje ya ukumbi.
Mwenyekiti wa uchaguzi Profesa Tibaijuka alitumia mamlaka yake kumlinda Shyrose Bhanji asitolewe njie kwa vile ni haki yake kumwuliza swali mgombea.

Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."

Jibu ni out of CONTEXT!
 
Kumbe magamba hawataki kiongozi anayeweza kujibu hoja...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Sophia Simba kaeleza wazi "wajumbe...wajumbe huyu muuliza swali kaja juzi juzi hapa tukampa ubunge wa Africa mashariki...hajui kitu huyu, ndiyo maana anauliza hili swali, kwa sababu hajui huku chini kinamama tumefanya mambo mengi, mambo makubwa...."

Pengine Shyrose amesahau kazi ya umoja wa wakinamama wa CCM. Jiulize kwa nini moto uwake kwa swali dogo tena ambalo ndiyo swali 'common' kwa mgombea yeyote duniani anayetetea kiti chake?

Hili swali la Shyrose lingeweza kushangiliwa sana ikiwa lingebadilishwa kidogo na kuwa "utatuhakikishiaje kuwa huku chini wanawake tutafanya kazi kubwa zaidi kama tulivyofanya kipindi cha uongozi wako uliopita?"

Kwani Shyrose hajui kuwa CCM inaimarishwa kuanzia chini, kwenye ngazi ya shina?

Mkuu nimeelewa. Kumbe CHINI ndo kila kitu kwa ccm! I mean kila kitu hufanyika CHINI?
 
Ni kwa sababu tu ya nguvu kubwa aliyonayo Sophia Simba, vinginevyo swali lilikuwa la kawaida sana na SS angelitumia kujipatia kura zaidi. Inaonekana wajumbe waliozomea walishajipanga kwamba mtu yeyote kutoka kwenye kambi ya Anne Kilango angeishia kuzomewa. Sasa naelewa ni kwanini SS alisema hamwogopi Mama Kilango
 
images
images

Shyrose Banji mjumbe wa mkutano mkuu umoja wa wanawake Tanzania ambaye pia ni mbunge katika bunge la Afrika Mashariki amenusurika kufukuzwa kwenye mkutano wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo baada ya kumwuliza swali gumu Sofia Simba kama ifuatavyo:
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Wafuasi wa Simba walilipuka kama gas iliyoshika moto kwa kutaka atolewe nje ya ukumbi.
Mwenyekiti wa uchaguzi Profesa Tibaijuka alitumia mamlaka yake kumlinda Shyrose Bhanji asitolewe njie kwa vile ni haki yake kumwuliza swali mgombea.

Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."
Swali limekaa vizuri sana, ila majibu yake yamekaa vibaya sana.
 
ubaya wa hilo swali uko wapi?
Au ndo ubabe wa sophia tu?
...Mkuu hata mimi nilisikitika kwa jinsi walivyomshambulia Shyrose utadhani alichouliza hakina maana. Tatizo la wanasiasa wa aina ya akina Sophia ni kujiona wao ndio mwanzo na mwisho kwamba hauguswi na yeyote kitu ambacho si kweli. Kwanza yeye ili kujipambanua na wengine angejibu swali kama alivyoulizwa badala ya kutoa mipasho kuwa Shyrose ni mchanga na hajui siasa za chini ya kapeti sijui ndio zipi? Huyu Sophia nimeona profile yake kwenye thread moja humu kwa maoni yangu hafai kuwa kiongozi. Typically ni muhuni kama mwenyewe alivyoeleza historia ya maisha yake....we mtoto wa kulelewa kwenye nyumba yenye bar ndani unategemea atakuwaje?
 
Mkubwa, hakuna swali hapo!

Shyrose amemwambia Sofia "Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Hicho ndicho tulichonacho jukwaani hapa.

Watu wengi wamehadaika na kichwa cha habari cha thread hii. Shyrose Bhanji, hajauliza suali lolote-kwa mujibu wa nukuu katika thread hii- alichofanya ni kumshutumu Sofia Simba kuwa hajakitetea chama kwa kipindi chote cha miaka minne ya uenyekiti wake wa UWT

Kama Bi. Banji alipewa fursa ya kuuliza suali na badala yake akatoa statement ya kumshutumu mgombea na kumalizia hapo, inabidi tujiulize uelewa wa huyu Ms.Banji kabla ya kuchambua jibu la Bi. Simba.

Labda tuseme

1. mleta thread hii amemnukuu vibaya Ms. Banji licha ya hizo quotation marks alizobandika
2. mleta thread hakumaliza nukuu yote ya Ms.Banji, na alichokinukuu kilikuwa ni background ya suali lake lililofuatia
3. Ms. Banji hakuwahi kuuliza suali lake, akavamiwa na "jibu" la Ms. Simba

Vyenginevyo, Shyrose kachemsha, maana hakuuliza suali lolote
 
Mbona swali ni la msingi kabisa nadhani hao wapiga kura walio mzomea ni kwa sababu ya ushabiki tu
 
Swali limekaa vizuri sana, ila majibu yake yamekaa vibaya sana.

"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."

Jibu la Sofia Simba ni tata mno na halionyeshi mtu mwenye upeo wa kiwango chake katika kujibu swali la aina ile ambayo kijana huyu Shyrose alimwuliza ambalo lilihitaji jibu lenye kuonyesha jitihada zake katika kukijenga chama.

Jibu kwamba amejiimarisha katika ngazi zote kuanzia matawi, kata, wilaya hadi mkoa, ni jibu jepesi lenye kuonyesha kwamba amejiimarisha kusaka ushindi katika kutetea nafasi aliyo nayo badala ya kukijenga chama na kukitetea kama swali lilivyoulizwa.

Hii ndiyo aina ya viongozi tulio nao ambao uchaguzi huu ukishapita wanachohangaikia ni kuwa karibu na wapiga kura ili kujenga mazingira ya kuchaguliwa tena nafasi ijayo badala ya uwajibikaji unaotakiwa. Mfumo uliopo CCM unaruhusu hayo kwa vile kila aliyeko CCM asipofanya hivyo inakula kwako na wawajibikaji watabaki kutembwa kwa sababu hawajaweka masilahi kwa wananchi wanaowatumikia bali kwa wajumbe wapiga kura kuwapa mlo.

Hawa wanaotaka utendaji wa kweli, kukilinda chama na uwajibikaji kwa wananchi ndio Nnape Mnauye anayewaita oil chafu inayochukuliwa na Chadema. Ufa mkubwa sana nauona sasa hivi, ipo siku nitatoa mada kuuonyesha.
 
Back
Top Bottom