Swali la nyongeza, Bunge litawaka moto

fardia

Member
Jan 16, 2012
41
6
Muheshimiwa spika, kwanza nashuku kwa kuniona na kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
1. Kwa kuwa mawaziri hao wamekubali kuwajibika na kwa kujiuzuru. Je, serikali inampango wa kuwashtaki na kutaifisha mali zao zote?
2. Kwa kuwa mawaziri hao wamejipima wenyewe na kuamua kumwokoa waziri mkuu, Je, lile zoezi la kupiga kura kutokuwa na imani na waziri mkuu liendelee au lisitishwe?
Muheshimiwa naomba mwongozo.
 
kwa kua hukufuata kanuni, Jamani kila siku nasisitiza someni kanuni zinazotuongoza, bunge sio kariakoo, sisi tuna kanuni.

sasa nikirudi kwenye muongozo ulioomba, kwanza haiwezekani, unajua waheshimiwa wabunge kuna mambo mengine sijui tunayaibua ya nini, kama wabunge mmeongea, mawaziri nane wamejiuzuru, huo ni uwajibikaji mkubwa sana, hii haijawahi kutokea tanzania, hii tayari ni heshima kubwa kwa bunge.

kwa hiyo waheshimiwa wabunge mi muongozo wangu ndio huo.
 
kwa kua hukufuata kanuni, Jamani kila siku nasisitiza someni kanuni zinazotuongoza, bunge sio kariakoo, sisi tuna kanuni.sasa nikirudi kwenye muongozo ulioomba, kwanza haiwezekani, unajua waheshimiwa wabunge kuna mambo mengine sijui tunayaibua ya nini, kama wabunge mmeongea, mawaziri nane wamejiuzuru, huo ni uwajibikaji mkubwa sana, hii haijawahi kutokea tanzania, hii tayari ni heshima kubwa kwa bunge.kwa hiyo waheshimiwa wabunge mi muongozo wangu ndio huo.
muongozo wangu hata muheshimiwa mkuu wa kaya afuate hao mawaziri nane!.
 
hayo mahojiano yametokea kweli bungeni? au Fardia na Uswe wanafanya kaigizo kadogo hapa JF??
 
Muheshimiwa spika, kwanza nashuku kwa kuniona na kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
1. Kwa kuwa mawaziri hao wamekubali kuwajibika na kwa kujiuzuru. Je, serikali inampango wa kuwashtaki na kutaifisha mali zao zote?
2. Kwa kuwa mawaziri hao wamejipima wenyewe na kuamua kumwokoa waziri mkuu, Je, lile zoezi la kupiga kura kutokuwa na imani na waziri mkuu liendelee au lisitishwe?
Muheshimiwa naomba mwongozo.

Mheshimiwa mbunge...kwa kuwa tayari mawaziri CHAMI, MKULO, na wengine wamewajibika kwa hiari yao wenyewe...napnendekeza zoezi na Mh Zitto liendelee kwani Waziri mkuu ndio kawalea hawa mafisadi. Sasa Zitto malizia mchakato wako na J3 uwasilishe hiyo hoja na mimi kama spika mzalendo nitaipitisha. Tena napenda kutoa angalizo...jamani wabunge kwenye hili tuweke itikadi za vyama vyetu kando. Tumuunge Mh. Zitto mkono ili waziri mkuu aondoke kwa kishindo katika serikali. Na kama Rais ataona tumemuonea waziri mkuu wake, basi kuna kanuni ambayo inaturuhusu kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais, japo naye anaweza kulivunja bunge. kwa hiyo tutachagua, tumpigie kura rais nae aondoke kabla hajalivunja bunge ili tuwe na uchaguzi wa rais tu..... Muongozo wangu ndio huo.
 
Mwongozo Mheshimiwa Spika..
Je baada ya hao mawaziri kujiuzulu na waziri mkuu kujiuzulu je tunaweza kutafuta kura nyingine 70 za kukuondoa Mheshimiwa spika kwenye icho kiti chako..??
Nawasilisha
 
Mheshimwa speaker AG anatuambiaje kuhusu hawa walikwapua ela za serikali kupelekwa mahakani au ikiwezekana wapigwe mawe hadharani mpaka kufa
 
Waheshimiwa wabunge kulingana na kifungu cha sheria cha bunge katika katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania kifungu cha 76. C. Kama mawaziri watajiuzulu hivyo kuathiri mfumo mzima wa baraza,baraza zima litavunjwa na kuundwa upya na mh.raisi
 
Muheshimiwa spika, kwanza nashuku kwa kuniona na kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
1. Kwa kuwa mawaziri hao wamekubali kuwajibika na kwa kujiuzuru. Je, serikali inampango wa kuwashtaki na kutaifisha mali zao zote?
2. Kwa kuwa mawaziri hao wamejipima wenyewe na kuamua kumwokoa waziri mkuu, Je, lile zoezi la kupiga kura kutokuwa na imani na waziri mkuu liendelee au lisitishwe?
Muheshimiwa naomba mwongozo.
mweshimiwa mbunge hilo la kwanza litawezekana nipe muda . Na kwa hili la pili nashauri mh. zitto abadilishe muhusika awe rais na sio tena waziri mkuu.

ikitokea hivi najiua.
 
"jambazi" ananyanyuka;
Mh spika, nashukuru sana kwa muongozo wako, nilitaka kushukuru pia kwa jina jipya. Naomba mawaziri waliojiuzulu wafilisiwe na wapewe kamtaji kadogo waje kuuza viatu jimboni kwangu.
Naomba kuwasilisha.
 
Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri niliyopatiwa, bado nina maswali mawili ya nyongeza.
1. Kwa kuwa mheshimiwa rais amesharudi nchini, na kwa kuwa inasemekana ana safari nyingine kuelekea Malawi, je, tunasuhusiwa kuizuia ndege yake isiruke mpaka atakapowashughulikia hao mawaziri mafisadi?
2. Kwa kuwa hao mawaziri wamepoteza sifa ya uongozi, je, inaruhusiwa wavuliwe na ubunge kwani hawastahili kabisa kuwawakilisha wananchi?
 
Muheshimiwa Spika, nimesahau kuuliza maswali muhimu sana.
1. Kwa kuwa shirika letu la ndege halina ndege hata moja, je, kwa nini bunge lako lisitoe amri ya kuichukua ndege ya rais na kulikabidhi shirika la ndege ili kulinusuru lisife kabisa?
2. Kwa kuwa rais atakuwa hana ndege hivyo hataweza kwenda safari za nje. Je, serikali haioni haja ya kumkodishia helikopta kwa ajili ya safari za hapa nchini?
 
Haya ni maswali ya [msingi] kabisa....he he he! Vasco dagama, lol. Kuna watu wasiotakiwa kutawala nchi hii kabisa! Aaqrgh!
 
Muuliza swali la nyongeza kaa chini,waheshimiwa wabunge kila cku nasema kuhusu swala la kuvunja kanuni na hili halikubaliki kabisa,na spika nimimi pekee sasa naahirisha bunge mpaka jumatatu saa tatu na nusu maana humui ndani kuna watu wana viherehere sana. Kuna matangazo hapa chama cha magamba kuna kikao cha dharura!
 
kwa kua hukufuata kanuni, Jamani kila siku nasisitiza someni kanuni zinazotuongoza, bunge sio kariakoo, sisi tuna kanuni.

sasa nikirudi kwenye muongozo ulioomba, kwanza haiwezekani, unajua waheshimiwa wabunge kuna mambo mengine sijui tunayaibua ya nini, kama wabunge mmeongea, mawaziri nane wamejiuzuru, huo ni uwajibikaji mkubwa sana, hii haijawahi kutokea tanzania, hii tayari ni heshima kubwa kwa bunge.

kwa hiyo waheshimiwa wabunge mi muongozo wangu ndio huo.

Kama kweli itakuwa vizuri sana
 
Mwongozo Mheshimiwa Spika..
Je baada ya hao mawaziri kujiuzulu na waziri mkuu kujiuzulu je tunaweza kutafuta kura nyingine 70 za kukuondoa Mheshimiwa spika kwenye icho kiti chako..??
Nawasilisha

Asanteeeeeee *in madam speaker's voice*. Kwa kuwa zile yutong zang hazijanilipa bado na sijaanza kula faida, pia zile hekalu hazijakamilika ujenzi, natoa muongozo kuwa sahihi 70 dhidi ya spika zingoje kidogo.
Plus nilishatangaza kuwa sitogombea tena.

Asanteeeeee
 
Back
Top Bottom