Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Mkuu ipi? Nyumba ya Zamani ya Makamo wa Rais?
Usalama wa Taifa
Mkuu ipi? Nyumba ya Zamani ya Makamo wa Rais?
Usichanganye vitu tofauti.
Ikiwa hivyo mbona unasahau kina Maftah? unamjuwa Maftah wakati wa Nyerere na Anti corruption Squad yake, iliyokuwa chini ya UWT?
TAKUKURU imeanza wakati wa Kikwete. Full Stop. usitake kubisha kitoto.
Hamchangii mada hii
tena, kumbe mlikuwa mmeanzisha mada kusubiria mnapoangalia mechi ya LA
Lakers, maana naona mmeshaingia mitini.
Pindeni maneno mtakavyoyapinda wekeni maneno nnɾ ıuıɥɔ ıuıɥɔ nnɾ, ukweli unabaki kuwa ukweli. Jitihada binafsi za Kikwete ndio zinaibuwa haya madudu yote. Na juzi kawaziba midomo, sasa njooni na uzushi na kila kitu.
JMK anaendelea kuweka rikodi njema. Hakuna Rais bora aliyetokea Tanzania kabla yake, ya huko mbele ajuae ni Mungu.
Sasa wewe ndiye unayetuletea pumba. Yaani TAKUKURU haikuwepo kabla ya Kikwete? Na umeme je?Pumba hizo, TAKUKURU imeanza wakati wa Kikwete, kabla ya hapo haikuwepo.
Sasa wewe ndiye unayetuletea pumba. Yaani TAKUKURU haikuwepo kabla ya Kikwete? Na umeme je?
Ningekuwa mimi ndio natoa miundo serikalini takukuru ingekuwa iko chini ya either CAG au DPP, kuwa independet kwa sisi tunaokutana nao mala nyingi tunayajua matatizo yake, usijekuta wazuia rushwa ndio namba moja kwa rushwa! Wangebadirisha structure ingekuwa nzuri saana
Kwangu mimi
naamini vita dhidi ya corruption na masuala mengine haiwezi kufanikiwa
bila DPP kuwa naa nguvu zaidi na bila kuwezeshwa zaidi. Haiwezekani watu
wanaochunguza (CAG na TAKUKURU na Polisi) wanapewa uwezo mkubwa sana wa
kufanya uchunguzi lakini kwenye kuleta mashtaka tunaambiwa "nafasi yao
inazidi kutambuliwa pole pole". Hivi, uchunguzi una faida gani kama
hakuna mashtaka au kuna maana gani uchunguzi ucheleweshwe kwa sababu DPP
hana vitendea kazi au uwezo wa kufuatilia kesi mbalimbali?
Kwa mfano TAKUKURU hata ichunguze vipi sote tunajua ultimately ni DPP
anaamua kesi ipi iendelee au ipi isiendelee na anayo haki ya kujiingiza
kwenye kesi yoyote iliyofunguliwa na chombo chochote nchini! Binafsi
naamini tumeweka vipaumbele vyetu kinyume nyume! kabla ya kuweza uwezo
kwenye uchunguzi tulihitaji kuweka uwezo kwenye prosecution...
sivyo?
Mzee Mwanakijiji hilo ni kama swali la kuku na yai. Kipi kimetangulia? Ukweli ni kwamba bila investigation hakuna prosecution!
in a sense yes;
lakini in practicality uchunguzi unaoishia kwenye uchunguzi hasa kwenye
masuala ya uhalifu na haki hautendi haki. Hivyo, prosecution ina nafasi
ya pekee; kumbuka - na niliwahi kuwa na mjadala hapa muda kidogo
uliopita - DPP anao uwezo wa kuagiza uchunguzi ufanyike na hata kufanya
special 'investigation' yeye mwenyewe.
Naombeni kufahamishwa: Hivi kuna umuhimu kweli wa hii ofisi? Mi nadhani hawa investigators (TAKUKURU etc.) should go on prosecuting by themselves. Otherwise mi naamini kabisa DPP yupo pale kisiasa zaidi.
Mkuu unahoja nzito kwenye majibu yako.............. DDP ni mtu wa ofisini anasuburi watu wa field akina CAG,TAKUKURU na POLISI wafanye uchunguzi wao kisha yeye anatoa matokeo tu,nikama vile unaona walimu TZ nzima wanafindisha form four lakini wanaosahihisha mitihani hawafiki hata asilimia 10 ya walimu Kinadharai DDP anahitaji watu wachache kuliko wakina CAG na wenzake nafikiri ndio sababu wamepewa kipaumbele kupewa majengo..... Lakini mimi sidhani kama hoja hapa ni majengo, hoja ni uwezeshwaji wa hizi taasisi....unaweza kupewa majengo yako na usiwezeshwe inavyotakiwa na unaweza ukakodishiwa majengo na ukawezeshwa inavyotakiwandio maana nilitangulia kusema umuhimu wa DPP sasa hivi unadhihirika. baada yakuimarisha vyombo vya uchunguzi demand ya huduma za DPP imeongezeka. nakubaliana na wewe kuwa kuna ya haja ya kumtengenezea mazingira mazuri ya kazi!
Mzee Mwanakijiji,Kwangu mimi naamini vita dhidi ya corruption na masuala mengine haiwezi kufanikiwa bila DPP kuwa naa nguvu zaidi na bila kuwezeshwa zaidi. Haiwezekani watu wanaochunguza (CAG na TAKUKURU na Polisi) wanapewa uwezo mkubwa sana wa kufanya uchunguzi lakini kwenye kuleta mashtaka tunaambiwa "nafasi yao inazidi kutambuliwa pole pole". Hivi, uchunguzi una faida gani kama hakuna mashtaka au kuna maana gani uchunguzi ucheleweshwe kwa sababu DPP hana vitendea kazi au uwezo wa kufuatilia kesi mbalimbali?
...Ukitaka kuwafikirisha watu, wachokoze wajadili. Au sio?Serikali ya JK jana imejisifia kwa kuwezesha TAKUKURU na CAG. Sote tunajua idara hizo mbili ambazo ni vinara katika kupigana na ufisadi sasa zina ofizi zao za kisasa - makao makuu na hata za mikoa/kanda. Lakini hakuna ofisi yenye matokeo ya moja kwa moja katika vita dhidi ya ufisadi kama ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP). Huyu ndiye mtu wa mwisho nchini anayeamua nani anashtakiwa kwa kosa gani na adhabu gani itafutwe. Baada ya majigambo yote yaliyotolewa jana nimebakia na hili swali
...Kama wapi?. Je, tuna mfano wa kuiga?Tumbiri, nimependa sana; binafsi naamini pia kuna haja ya kuanzisha mfumo wa Emergency Financial Manager chini ya CAG. Baada ya CAG kuona kuwa mahali fulani kuna usimamisi mbaya wa fedha kiasi kwamba kuna ufujaji basi anatoa taarifa kwa wahusika kuwa idara au kitengo hicho kiko kwenye default na hivyo uongozi wake unasimamishwa na kuingizwa EFM ambaye atasimamia finances wakati uchunguzi unaendelea zaidi na kurudisha nidhamu ya fedha. Haiwezekanai CAG anaonesha kitu kile kile kwenye ofisi ile ile miaka nenda rudi bila matokeo ya papo kwa papo kwa wahusika.
...Mazingira mazuri au mamlaka zaidi, kipi cha muhimu?ndio maana nilitangulia kusema umuhimu wa DPP sasa hivi unadhihirika. baada yakuimarisha vyombo vya uchunguzi demand ya huduma za DPP imeongezeka. nakubaliana na wewe kuwa kuna ya haja ya kumtengenezea mazingira mazuri ya kazi!