Swali la kizushi kwa Dr Slaa, Mbowe, Mnyika, Mkumbo na Wanachadema

Wanzanzibar walifikiri lini kuwatendea chadema haki?

Haitatokea wala hakuna anaewania hilo litokee. Heshimu kauli ya "Zanzibar ni ya Wazanzibar". Wapenzi wa Chadema zanzibar wapo wana heshima zao sana lakini wako arginalised.

Jibu sawa na hapo juu haitatokea.
Mkuu,
Ni vyema ukawashauri CDM wajitangaze hivyo kuwa hawana interest na Zanzibar ili wale wanachama wao kule watafute vyama vyenye agenda na Zanzibar.

Kuna , mchangiaji mwengine pia anasema CDM ipo zaidi kusimamia maslahi ya Tanganyika...katika hili munarahisisha kazi ya CCM ya kui-brand CDM kuwa ni chama cha Bara, dini na ukabila. Sipendi niamini kuwa ni hivyo. Acheni ushabiki huu unaoutia dosari CDM.
Kuna haja ya CDM kuwekeza pia katika kupata wanachama wengi na kufungua matawi huko Zenj.
Au CDM isizungumzie Tanzania, izungumzie Tanganyika.
 
Mbowe alisema wakati wa mdahalo na Hamad Rashid kuwa Yeye (Mbowe) alienda kuzungumza na CUF (Hamad Rashid) kuwataka washirikiane kwenye kambi ya upinzani, alikuwa hajui kuwa CUF imeolewa na CCM?
 
Sasa mwita unataka mtoto akizaliwa tu ale mihogo na miwa? simpaka aote meno? wewe ulitaka CDM izuke tu vuuuuuuuuu ichukue zanzibar? Ndugu yangu Mwita hata Roma haikujengwa siku moja. Ni jukumu la kila mwanamapinduzi wa kweli kuijenga CDM ya miaka ijayo kwa kizazi kijacho.

Shukrani sana kwa majibu yako mapesi wewe ni grit sinka

Mohamed, kweli wewe ndo the only great thinker hapa jf.
Unatakiwa kufahamu kwamba huwezi kujisifia sana mbele ya watu hapa jf kwamba wewe ni bora kuliko wengine.
Nimekuona kule kwenye thread ya mtatiro ulivyokuwa unapandisha mabega juu kwamba unatumia pc yako wengine wanatumia za waajiri wao. Sasa huu kama sio ulimbukeni ni nini? Watu tumekutana hapa jf kila mmoja kwa namna yake sasa mtu unapoishiwa hoja ukaanza
kuleta vioja si tunakuangalia tu, na kusema nawewe kiistaarabu sio kwamba hatujui jino kwa jino.

sasa kama unajua kwamba roma haikujengwa kwa siku moja mbona unaikejeli cdm kutokuwa na mwakilishi visiwani zanzibar? Halafu unasema cdm ina wanaharakati, haina wanadiplomasia kweli wewe unaijua siasa ya kwetu ama umejawa jazba za cuf?
 
Sina uhakika kama wote mpo jamvini lakini nina uhakika kuwa Dr Slaa, Mnyika na Mkumbo tunao humu jamvini kwa maana nimeona post zao nyingi tu.


Nisiwachoshe na maelezo naomba niulize maswali mawili la pili likiwa na sehemu aa na be.

1.Kutokana na tamko lenu kuhusu KUB kuwa hamtawashirikisha CUF kwa kuwa imo ndani ya Serikali ya kitaifa je mtawashirikiasha UDP na NCCR - Mageuzi? na kama hamtawashirikisha ni kwanini?

2.Ninavyoona hamuwatendei haki Wazanzibari ambao miongoni mwao wapo wanaCDM kwa maana Serikali ya umoja wa kitaifa wao waliupigia kura za maoni na kura hizo ndizo zilizopelekea kubadilishwa katiba na kusomeka kama ilivyo sasa.



b)Je ikitokea siku moja mkashika nafasi ya pili Zanzibar na katiba inasema kuna Serikali ya kitaifa mtakubali ku join hands na walioshinda ili kuwatumikia wananchi?

Nina maswali mengi lakini hayo ni yamsingi mengine ya nyongeza yatakuja baada ya kujibiwa hayo maswali.

si kwamba Chadema hawataki kuunga mkono au kuthamini mchango wa vyama vingine kama cha mahalimu seif(CUF) na si kwamba kutounganisha kambi ni kutothamini watanzania wenzetu mliozungukwa na maji. lakini kikubwa ni kukwepa mtego walioingia CUF kwa CCM na kukubali kuuza chama chao kizuri kwa umakamo wa rais wa zanzibar na kuacha kazi inayotakiwa kuwatetea wananchi wa zanzibar
cha msingi ni bora CUF wajiunge kwenye kambi ya CCM........
pia si kwamba kutojiunga na chama chenye mizizi sehemu fulani ni kutothamini raia wa upande ule
kwa mfano je Chadema kutoungana na CCM bara ni kutowathamini wabara?

lazima watu waikomboe CUF kwanza kabla ya kudhani ni chama sahii cha upinzani
 
Mkuu mleta mada,najua wee msomi kwa elimu ya chuo kama sikosei Uhasibu,nakumbuka pale karibu na posta ila lugha ya kiswahili hauitendei haki. Kuna maneno mazito unayatumia kiasi kwamba yanawatisha watu. Si kweli kuwa Viewers wasiokujibu ni wanacdm,kumbuka jf hata non member anaweza kuview na angalia viewers wa jf kwa siku ni wangapi kama hawazidi hata members wa jf. Tena napenda uweke maneno yako vizuri,usitegemee kuuliza mbunge swali ukaweka title swali la kizushi,alaf ukute Mnyika,Mkumbo dr. ,wamekujibu.,haiwezekani. Alaf hata kama mtu akikupinga weka itikadi pembeni umjibu kwa weledi,ulivowajibu wachangiaji ni ajabu,mfano kagemro! Mwisho,napenda kujibu hoja japo mi stajatakiwa kukujibu sababu umewataka wanacdm kama Mnyika na mbowe,ila kuhusu kambi ya upinzani, Cuf waende kuwakilisha wananchi wala si kugombea vyeo. Kumbuka mwaka 95 CUF iliunda kambi pinzani yenyewe pekee,05 imelazimika kwa kuwa haikuwa na 12%ya wabunge,mwaka 2010 ndo cdm wanaunda kambi peke yao wana 12%+,pia CUF haikuandikishwa Zbar,ni chama cha kitaifa na kina sera moja. Mfano cdm iko Tz nzima,na hapa mfano kama hawajaridhika hawawezi kusema cdm kanda ya kaskazini wameingia msituni/wamehasi,alaf ukasema pande zilizobaki watakaa kidemokrasia,hapana,wakifanya jambo tunajua wamefanya jambo kama Cdm Taifa! Mtego wa ccm kuweka Cuf zbar ni mbaya sana. Mwisho,sikuweza kujibu hoja zako zote ila kumbuka kama Cdm wakishika hatamu wanakuja na KATIBA mpya na hawatabanwa na maswali yako bali watafanya "system overhaul". CCM walichokiweza miaka yote ni divide n rule. Mwaka 95 TLP walimpambanisha maasimu wao yule shushushu na kashfa ya kuwa na mke wa nje,mwaka 2000,2005 wakasema CUF ni magaidi na ni chama cha kidini,wakaleta mpaka makontena ya visu vya kivita vikiwa na nembo ya CuF,leo hii visu vipo hata k.koo vinauzwa wala haviitwi zana za kivita kama Mahita alivodai,na kwa kufanikisha ilo uliza leo hii mahita ni nani ktk vitegauchumi vya Tanzania. Mwaka 2010 wamesema Slaa,dr. ametumwa na wakristo! Na kweli watu wanatamaalaki kwa ili hadi rais katangazia tanzania bungeni adui wa nne UDINI. JE,ivi Tanzania Waislam/ au Wakristo hawapaswi kutawala? Kama ndo ivo Ccm kina dini gani kwa kuwakataa waislam/wakristo kwa nyakati tofauti? Ccm dini gani?wapagani? Pia angalia maana ya KUB maana kila ulipoirejea umekosea' Siku njema.
 
1.Kwa ninavyojua mimi cdm hawana mpango na siasa za Zanzibar maana siku za karibuni muunganiko huo wa nchi za Zanzabar na Tanganyika utavunjika na hivyo kila nchi iwe kivyake. Hivyo kuhusu malengo ya cdm Zanzibar kama yalivyo kwa watanganyika wengi wenye maono ya mbali ni kuomba Mola hilo limuungano lifilie mbali.

4. cmd hawana mpango wa kuunda serikali huko znz kama nilivyokwisha eleza haka kamuungano soon katakolapsi!

Mkuu,
Kwa nini CDM hawaungani na REv. Mtikila ili hii issue ya Tanganyika i-resonate vizuri?
Kama CDM wanamkakati huu tu basi waitaje Tanganyika kwa nguvu katika discourse yao, sote tunataka Tanganyika isikike na izaliwe upya!
Huu utanzania na Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar pamoja...mimi ni mmoja wa wanaoamini kuwa mwalimu alifanya makosa makubwa kubadilisha jina la asili la muungano wa Tanganyika na Zanzibar..kuiita Muungano wa Tanzania na baadae kusema kuna nchi moja tu Tanzania.
 
Madaraka mazuri jamani! MBOWE sasa ANATEMBELEA V8 ina Plate namba ya KUB
 
Mbowe alisema wakati wa mdahalo na Hamad Rashid kuwa Yeye (Mbowe) alienda kuzungumza na CUF (Hamad Rashid) kuwataka washirikiane kwenye kambi ya upinzani, alikuwa hajui kuwa CUF imeolewa na CCM?

Mkuu siasa ina maana pana unafiki na uzandiki haukwepeki!
 
Nilitegema kwamba hawataungana na nimegurahi kuwa hawajaungana

Maswali hayo hawana majibu pia hawana sababu ya kujibu (no incentive to do so) why? Wabongo wasahaulifu hawahitaji maswali magumu..

Good move Chadema keep it and (Mtagawanaje cake na waswahili mkuu?)
 
Tumlaumu nani kwa CDM kupata kura chini ya 5%? tuilaumu CUF na MTATIRO? Sometime common sense is common chama lazima kiwe na oparations kule kanda ya ziwa walifanya oparation sangara kwanini zanziba wasifanye oparation papa? Sote tunajua matunda ya oparation sangara kwenye mikoa ya kanda ya ziwa nina wasiwasi CDM wanaangalia sehemu yenye population kubwa zanzibar wapiga ni wachache pengine ni kama wa majimbo matatu bara ni mawazo yangu tu.

Kama unafahamu kwamba katiba ya zanzibar inataka chama kinachopata 5% ya kura ndo kishirikishwe kuunda SUK, mbona sasa inakuwa vigumu kutumia akili hiyo hiyo kujua kwamba kanuni za bunge zinatambua chama rasmi cha upinzani bungeni ni kinachokuwa na at least 12.5% ya wabunge na kiwe na idadi kubwa ya wabunge kuliko vyama vingine?

Kama cuf na ccm wameunda SUK zanzibar kwa mujibu wa katiba na vyama vingine vimekubali na kuheshimu, ni kwanini cuf hawataki kuheshimu kanuni za bunge zinazoipa chadema uwezo wa kuunda kambi ya upinzani bungeni.

Hebu jaribu kuwa mkweli kidogo mohamed ili angalau kuondoa ile dhana kwamba hamko serious.
 
Madaraka mazuri jamani! MBOWE sasa ANATEMBELEA V8 ina Plate namba ya KUB

Na hicho ndo anacholilia hamad rashid na cuf kwakuwa amewahi kuonja ladha ya V8 sasa anatamani walau apate unaibu KUB ama shadow minister, huyu jamaa ana njaa kali sana. Na enzi zile anatumia V8 ya serikali kwa kuwa KUB bado maliwaliza wabunge wenzake, walimpatia pesa awaletee magari akaingia mitini hadi soo lilipofumuka ndo akawalipa.
 
Kwa hilo nakubaliana na wewe na ujue pia muungano tunaoujua mimi na wewe ni tofauti na wanaujua kina Seif Sharif na Mzee Aboud Jumbe na Mzee Karume. Mzee Karume kuna kipindi alipoona anabanwabanwa na Nyerere alinukuliwa kuwahi kusema "muungano ni kama koti likikubana unalivua"

Pia ikumbukwe kuwa ziliungana nchi mbili wazanzibari wana taifa lao na bado lina exist kwahiyo tusiwaonee choyo na wivu tumtafute mchawi wetu alieiuza nchi yetu ya Tanganyika ikaondoka kwenye uso wa dunia.

Kuhusu CCM (ASP) na CUF (HIZBU) kuna mikakati ya haja kuiweka mizizi ya CHADEMA (UMMA PART) zanzibar wale wa umma part ya Abdulrahman Babu wataingia hapa na mchezo utanoga na kuwa mkazi zaidi.

Ua unaonaje mzee?

Unavyosema kuwa CDM wapenenetrate Zanzibar, sijui unamaanisha nini, maana tayari wako huko na ndio maana mgombea uraisi huwa anatakiwa kuwa na wadhamini wasiopungua kiasi fulani kutoka kila sehemu mbalimbali na Zanzibar ni "mandatory" labda kama unamaanisha kuwa wawe na majority members kuliko vyama vingine hiyo sawa. Lakini pia ukumbuke kila chama kina strategy zake na inawezekana in a long run Zanzibar itakuwa ni ngome ya CDM, wewe mwenyewe ni shaidi kwa sasa kuwa CDM angalau ina wapenzi kama si wanachama huko Zanzibar, kama utafanya utafiti mzuri na kulinganisha na miaka ya 95 au 2000.

Kuhusu suala la CDM kushirikisha vyama vingine vya siasa kwenye kambi rasmi ya upinzani bungeni, napenda kusema kuwa maamuzi ya CDM nimeyapenda hakuna mfano, kuunganisha nguvu kulitakiwa kuanzia kwenye uchaguzi na siyo kwenye uchaguzi kila chama kinasimama peke yake, then baada ya uchaguzi eti tuungane maana yake nini? Mfano Tarime, Kigoma mjini, segerea, na majimbo mengi tu kama vyama vya upinzani vingeungana na kusimamisha mgombea mmoja mwenye nguvu sehemu hiyo, upinzani ungekuwa na viti vingi sana bungeni.

Suala la muungano hata mimi huwa nashangaa viongozi wa CCM kuung'ang'ania sioni maslahi yoyote zaidi ya kuendelea kunyonywa na hao wenzetu.
 
Mkuu,
Chama kinachopata kuanzia jumla ya kura 5% ndio kinapata ushiriki wa kuunda serikali huko Zanzibar. Kwa bahati mbaya au kutokuwa na mikakkati imara vyama vyengine,ikiwemo CDM havikupata hiyo asilimia na hivyo kukosa haki ya ushiriki kuunda serikali. Sio kwamba CCM au CUF wana kauli juu ya hilo. Ni katiba ndiyo inayoelekeza hivyo.

je kanuni za bunge zinaelekezaje kuhusu KUB.
 
Very hot topic indeed! ila mimi nikiwa mwana cdm nadhani tunan haja ya kuwekeza Znz kwa sababu kwa sasa hakuna chama ambacho wananchi wanaamini kiko imara zaidi ya cdm. Post ya leo imedhihirisha hilo kwani vyama vya CCM na CUF havina ajenda mpya pengine ni wakati wa chama chetu kwenda kuamsha siasa zetu makini kule. Binafsi siamini kama CUF ni chama makini kwa kutazama safu yake ya uongozi na elimu zao vis-a- vis chadema. pia tukumbuke huwezi kuwa na hoja imara kama huna elimu tosha. Jamani tujipange kuichukua znz kwa mikakati makini.
 
Mbowe alisema wakati wa mdahalo na Hamad Rashid kuwa Yeye (Mbowe) alienda kuzungumza na CUF (Hamad Rashid) kuwataka washirikiane kwenye kambi ya upinzani, alikuwa hajui kuwa CUF imeolewa na CCM?

Gaiji habarrr yako bana, aise nadhani nilikumis.
Back to the topic, Nadhani suala la mbowe kwenda kuzungumza na cuf haitoshi kuonyesha kwamba alikuwa hajui kwamba cuf imeolewa na ccm. Nadhani katika mazungumzo baina yao watakuwa walipeana masharti ndipo kila chama kikaamua kuchukua mkondo wake, cuf wakaamua kuwakusanya nccr, tlp na udp na cdm wakaamua kusonga kivyao.
 
Mkuu,
Chama kinachopata kuanzia jumla ya kura 5% ndio kinapata ushiriki wa kuunda serikali huko Zanzibar. Kwa bahati mbaya au kutokuwa na mikakkati imara vyama vyengine,ikiwemo CDM havikupata hiyo asilimia na hivyo kukosa haki ya ushiriki kuunda serikali. Sio kwamba CCM au CUF wana kauli juu ya hilo. Ni katiba ndiyo inayoelekeza hivyo.
Kadhalika kanununi zinasema chama cha upinzani kitakachopata zaidi ya 12.5% ya viti ndicho kitakachounda kambi ya upinzani. Ndivyo kanuni zinavyoeleza
 
Unajua kuna kitu kinaitwa duty of secrecy kwenye startegy za mapambano ya aina yoyote yale iwe vita,biashara,siasa sasa ndoa ya CUF na CCM kwa kweli ni hatari kwa CUF na CUF hawa wezi kwnda kinyume na ndoa hiyo,sasa basi pamoja na maswli yako yote hayo naomba kitu kimoja kijulikane CUF wameshindwa kutoa assurance ya kuto ku disclose mbinu za medani za kutafuta ushindi kwa upinzani, hiyo ndio shida kubwa na hakuna atkayeamini kwa lolote watakaosema CUF.
 
Lakini kwa kuwa CUF tayari wameungana na ccm, na hata wakati JK akilihutubia bunge alizitaja serikali mbili zinzoongozwa na ccm ikishirikiana na cuf. Kwanini cuf wasikamilishe tu upande kushiriki vyema na ccm? tuliona wakati wa uchaguzi wa spika, naibu spika na wawakilishi katika mabunge ya sadec ambapo ccm na cuf walikuwa na ushirikiano murua kabisa. Haukuishia hapo tu, ila hata katika uchaguzi wa mameya kama kule mwanza, walishikamana vyema ccm na cuf. Kinachowafanya tena kutamani huu upande wa pili ni kitu gani? nadhani cdm wanakosa kuwa na imani nao kwa kutojua ajenda iliyo nyuma yao.
 
Back
Top Bottom