Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
- Thread starter
- #41
Hoja ya CHADEMA iko wazi kuwa chama kimoja hakiwezi kujifanya popo.........wanahitaji kuchagua moja katika ushirikiano na vyama vya siasa. Aidha kuwa kwenye serikali au la, that's simple. Sasa CHADEMA wakiwa serikali halafu wakataka kuwa kwenye kambi ya upinzani kwa upande wa pili wa JMT itakuwa ni unafiki kama wanavyotaka CUF kuwa.
Usisahau pia kuwa mambo ya Zanzibar hayatenganishwi na mambo ya bara kwa kisiasa. Kumbuka Raisi mstaafu BW Mkapa alisha wahi kumteua R. Hamad wa CUF kuwa mbunge wa bunge la JMT, pia Raisi JM Kikwete alisha wahi kumteua mh. Jussa kuwa mbunge wa bunge hilo hilo la JMT na yote haya yalifanyika kwa sababu ya miafaka yao ya Zanzibar. Sasa inakuwaje leo CUF wawe serikalini Zanzibar lakini wajifanye hawako serikali (ushirikiano ) na CCM???????????
CUF waache unafiki, waendelee na CCM au wajitoe wakae na vyama vingine
Hayo maelezo yanajibu swali gani kwenye kati ya haya?
"1.Kutokana na tamko lenu kuhusu KUB kuwa hamtawashirikisha CUF kwa kuwa imo ndani ya Serikali ya kitaifa je mtawashirikiasha UDP na NCCR - Mageuzi? na kama hamtawashirikisha ni kwanini?
2.Ninavyoona hamuwatendei haki Wazanzibari ambao miongoni mwao wapo wanaCDM kwa maana Serikali ya umoja wa kitaifa wao waliupigia kura za maoni na kura hizo ndizo zilizopelekea kubadilishwa katiba na kusomeka kama ilivyo sasa.
a) Je kwa katiba iliyopo Zanzibar ikitokea one day YES kwa CDM wakashinda wao na kufuatiwa na chama kingine cha pili mtaunda serikali ya zanzibar peke yenu?
b)Je ikitokea siku moja mkashika nafasi ya pili Zanzibar na katiba inasema kuna Serikali ya kitaifa mtakubali ku join hands na walioshinda ili kuwatumikia wananchi?"