Swali la kizushi kwa Dr Slaa, Mbowe, Mnyika, Mkumbo na Wanachadema

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,304
Heshima zenu waheshimiwa ndugu Dr Slaa, Mbowe, Mnyika na Mkumbo, Najua nyie ni wana JF mpo katika hii himaya ya kina invisible na uwepo wenu hapa jamvini umeleta tija kubwa kwa kutujuza mambo mbalimbali ya kimapinduzi na kisiasa.

Sina uhakika kama wote mpo jamvini lakini nina uhakika kuwa Dr Slaa, Mnyika na Mkumbo tunao humu jamvini kwa maana nimeona post zao nyingi tu.

Nisiwachoshe na maelezo naomba niulize maswali mawili la pili likiwa na sehemu aa na be.

1.Kutokana na tamko lenu kuhusu KUB kuwa hamtawashirikisha CUF kwa kuwa imo ndani ya Serikali ya kitaifa je mtawashirikiasha UDP na NCCR - Mageuzi? na kama hamtawashirikisha ni kwanini?

2.Ninavyoona hamuwatendei haki Wazanzibari ambao miongoni mwao wapo wanaCDM kwa maana Serikali ya umoja wa kitaifa wao waliupigia kura za maoni na kura hizo ndizo zilizopelekea kubadilishwa katiba na kusomeka kama ilivyo sasa.

a) Je kwa katiba iliyopo Zanzibar ikitokea one day YES kwa CDM wakashinda wao na kufuatiwa na chama kingine cha pili mtaunda serikali ya zanzibar peke yenu?

b)Je ikitokea siku moja mkashika nafasi ya pili Zanzibar na katiba inasema kuna Serikali ya kitaifa mtakubali ku join hands na walioshinda ili kuwatumikia wananchi?

Nina maswali mengi lakini hayo ni yamsingi mengine ya nyongeza yatakuja baada ya kujibiwa hayo maswali.

Naomba kuwakisha na kutoa shukrani zangu za awali kwa majibu yenu mazuri na yenye kunifanya niwe huru na haya maswali yanayoniumiza kichwa tangu mlipotoa tamko kuhusu kuwashirikisha CUF na vyama vingine kwenye Kambi ya Upinzani Bungeni.

WanCDM.

Mnapotoa mawazo yenu mjue kuwa ni wananchi wa Zanzibar ndio waliopiga kura ya maoni kupitisha marekebisho ya katiba na kuweka kipengele cha serikali ya umoja wa kitaifa. Na katika hiyo sheria imetamka bayana kuwa vyama vitavyopata uwakilishi vitaunda serikali ya kitaifa. Sheria haikutaja vyama gani ila imesema vyama na sio CUF na CCM peke yake.

Mohammed H. Shossi

Safarini Ngamiani,
 
Maswali yako ni ya kizushi,hayahitaji majibu toka kwa viongozi wa CDM....CUF&CCM(Zanzibar) ni part and parcel,wanaishi kwa kutegemeana,na ndio siasa za Zanzibar zilivyo....huku bara tofauti, CCM ya huku si ya visiwani...
 
Kwa muelekeo uliopo Chadema kupata kiti kimoja Zanzibar ni ndoto seuze kushinda kabisa.

Nafikiria CDM ni chama makini na kina mikakati ya muda mfupi na muda mrefu juu ya siasa za znz sitaki niamini maneno yako kuwa CDM hawana haja ya Zanzibar na wazanzibar.
 
1.Kutokana na tamko lenu kuhusu KUB kuwa hamtawashirikisha CUF kwa kuwa imo ndani ya Serikali ya kitaifa je mtawashirikiasha UDP na NCCR - Mageuzi? na kama hamtawashirikisha ni kwanini?,

Walishaungana na CUF kuunda kambi ndogo ya upinzani isiyo rasmi = out

2.Ninavyoona hamuwatendei haki Wazanzibari ambao miongoni mwao wapo wanaCDM kwa maana Serikali ya umoja wa kitaifa wao waliupigia kura za maoni na kura hizo ndizo zilizopelekea kubadilishwa katiba na kusomeka kama ilivyo sasa.

Wanzanzibar walifikiri lini kuwatendea chadema haki?

a) Je kwa katiba iliyopo Zanzibar ikitokea one day YES kwa CDM wakashinda wao na kufuatiwa na chama kingine cha pili mtaunda serikali ya zanzibar peke yenu?

Haitatokea wala hakuna anaewania hilo litokee. Heshimu kauli ya "Zanzibar ni ya Wazanzibar". Wapenzi wa Chadema zanzibar wapo wana heshima zao sana lakini wako arginalised.

b)Je ikitokea siku moja mkashika nafasi ya pili Zanzibar na katiba inasema kuna Serikali ya kitaifa mtakubali ku join hands na walioshinda ili kuwatumikia wananchi?

Jibu sawa na hapo juu haitatokea.

Mohammed H. Shossi

Safarini Ngamiani,

Thanx big up
 
Maswali yako ni ya kizushi,hayahitaji majibu toka kwa viongozi wa CDM....CUF&CCM(Zanzibar) ni part and parcel,wanaishi kwa kutegemeana,na ndio siasa za Zanzibar zilivyo....huku bara tofauti, CCM ya huku si ya visiwani...

Swali la kizushi siku zote linakuwa linaukweli ndani yake linajipambanua kutoka uwongo na kujibiwa kuupata ukweli. Nadhani sisi sote tunataka kuijenga Tanzania moja na haina maana kugombea fito au sio mkuu.........
 
Maswali mazuri mkuu, tena naamini Dr. Slaa (PHD) atatupa majibu kwani ni mtu makini sana, simaanini wengine sio makini (msininukuu vibaya) ila napenda Dr anavyoweza kujibu hoja nzito kwa umakini zaidi
 
Walishaungana na CUF kuunda kambi ndogo ya upinzani isiyo rasmi = out

Wanzanzibar walifikiri lini kuwatendea chadema haki?

Haitatokea wala hakuna anaewania hilo litokee. Heshimu kauli ya "Zanzibar ni ya Wazanzibar". Wapenzi wa Chadema zanzibar wapo wana heshima zao sana lakini wako arginalised.

Jibu sawa na hapo juu haitatokea.

Thanx big up

Kwa ninavyovielewa hivyo vichwa yaani Mnyika, Dr wa ukweli Slaa, Mkumbo na Mbowe hawatakuwa na majibu mepesi kama yako. Ni wajibu wa Chama kuwa na mikakati ya kuweza kupenetrate kwenye ngome mpya na kuongeza wigo sitaki kuamini CDM watakaa na kubweteka wasifanye maipango ya kuweza kupata ushawishi Zanzibar. Chama chochote cha siasa lazima kiwe na mbinu za kusaka ushawishi nina imani thabiti kuwa wapo wazanzibari wanaoipenda CDM ni jukumu la CDM kuongeza idadi ya hao wanaoisupport unless CDM haitadumu"iakuwa namaisha mafupi" CDM kama chama cha siasa kisiangalie ya leo tu kiangaze ya miaka 5,10,15,20,25,30 ijayo na kadhalika.
 
Maswali mazuri mkuu, tena naamini Dr. Slaa (PHD) atatupa majibu kwani ni mtu makini sana, simaanini wengine sio makini (msininukuu vibaya) ila napenda Dr anavyoweza kujibu hoja nzito kwa umakini zaidi

Mimi naamini majibu yakitoka kwa yeyote yatakuwa yaliyo na busara na yenye kujitosheleza, hao watu nina imani nao kubwa sana.
 
Heshima zenu waheshimiwa ndugu Dr Slaa, Mbowe, Mnyika na Mkumbo, Najua nyie ni wana JF mpo katika hii himaya ya kina invisible na uwepo wenu hapa jamvini umeleta tija kubwa kwa kutujuza mambo mbalimbali ya kimapinduzi na kisiasa.

Sina uhakika kama wote mpo jamvini lakini nina uhakika kuwa Dr Slaa, Mnyika na Mkumbo tunao humu jamvini kwa maana nimeona post zao nyingi tu.

Nisiwachoshe na maelezo naomba niulize maswali mawili la pili likiwa na sehemu aa na be.

1.Kutokana na tamko lenu kuhusu KUB kuwa hamtawashirikisha CUF kwa kuwa imo ndani ya Serikali ya kitaifa je mtawashirikiasha UDP na NCCR - Mageuzi? na kama hamtawashirikisha ni kwanini?

2.Ninavyoona hamuwatendei haki Wazanzibari ambao miongoni mwao wapo wanaCDM kwa maana Serikali ya umoja wa kitaifa wao waliupigia kura za maoni na kura hizo ndizo zilizopelekea kubadilishwa katiba na kusomeka kama ilivyo sasa.

a) Je kwa katiba iliyopo Zanzibar ikitokea one day YES kwa CDM wakashinda wao na kufuatiwa na chama kingine cha pili mtaunda serikali ya zanzibar peke yenu?

b)Je ikitokea siku moja mkashika nafasi ya pili Zanzibar na katiba inasema kuna Serikali ya kitaifa mtakubali ku join hands na walioshinda ili kuwatumikia wananchi?

Nina maswali mengi lakini hayo ni yamsingi mengine ya nyongeza yatakuja baada ya kujibiwa hayo maswali.

Naomba kuwakisha na kutoa shukrani zangu za awali kwa majibu yenu mazuri na yenye kunifanya niwe huru na haya maswali yanayoniumiza kichwa tangu mlipotoa tamko kuhusu kuwashirikisha CUF na vyama vingine kwenye KUB.

Mohammed H. Shossi

Safarini Ngamiani,

Ahali yangu.

Chadema si chama cha kisiasa bali ni chama cha udugu, Ukabila na Udini.

Wao siku zote wanafakiri muafaka zanzibar ulitokea hivihivi tu bila CUF kufanya kazi ya ziada visiwani kwetu na matunda ndio haya tunayaona.

Nina imani Chadema hawawezi hata kidogo kuleta mabadiliko huku Bara peke yao bila kushirikiana na wenzao wa upi.nzani.

Chadema kidole kimoja hakivunji chawa. Unganeni mlete mabadiliko ya kweli.
 
Hafif mbona unahama kwenye mada? Kama huna jibu si ukae kimya? Kwani maswali haya yameelekezwa kwako? Huna jipya zaidi ya kupiga kelele kama debe tupu.
 
Utaona wanachadema wanaoulizwa wanaview na kusepa maana maswali yamesimama hasa yanabidi kujipanga ikiwezekana kuPM mwenye uelewa zaidi, napenda na kuwaheshimu hao wasoamao na kusepa nadhani watatafakari kwa kina maswali haya na Mungu atawafungua macho yao na kuona kilichojificha kwenye giza la upinzania Tanzania.
 
...

a) Je kwa katiba iliyopo Zanzibar ikitokea one day YES kwa CDM wakashinda wao na kufuatiwa na chama kingine cha pili mtaunda serikali ya zanzibar peke yenu?

b)Je ikitokea siku moja mkashika nafasi ya pili Zanzibar na katiba inasema kuna Serikali ya kitaifa mtakubali ku join hands na walioshinda ili kuwatumikia wananchi?

...

Maswali mazuri haya ingawa naona uendelevu wa mazingira hayo uko mashakani hasa kutokana na vuguvugu la kutaka kuandika katiba mpya. Sidhani kama muungano tulio nao utabaki kama ulivyo. Kisiasa, ukiacha CCM ambayo ilishajijenga kama chama dola, vingine vimeshindwa kujiimarisha katika pande zote mbili za muungano kwa uwiano unaotia matumaini. Hii inadhihirisha kupishana kwa kiasi kikubwa katika mitizamo ya kisiasa kati ya bara na visiwani.

Nionavyo, CHADEMA hawafikirii kuwa na mustakabali wa maana huko zenji (sera yao ni serikali tatu). Dalili zinaonyesha pia huo ndio mtazamo wa wengi. Kwa Katiba ya sasa ya Z'bar kutamka wazi kuwa ni nchi inaongeza uzito kwenye utashi wa kutaka muungano wa serikali tatu. Nadhani tutaishia kuwa kama U.K. ambapo Scotland na Ireland ya kaskazini wana vyama tofauti na England/Wales.

Hivyo, sidhani kama CHADEMA HATA wanawazia masuala ya Z'bar na katiba yake ya sasa kama ambavyo ungependa kujua. Wanacholenga ni ukamilishaji wa katiba mpya itakayobomoa status quo ya muungano.
 
Nadhani Chadema ilishasema ikiingia madarakani katiba itabadilika na kwahiyo mambo ya serikali zitakuwa ngapi na vipi zitaendana na hiyo katiba na sio katiba ya sasa
 
Katiba inayotakiwa kubadilishwa ni katiba ya Jamhuri ya muunga wa Tanzania na si ya Zanzibar. Na hata ikibadilishwa hiyo ya Muungano na kuweka serikali tatu , ya znz ya muungano/shirikisho na ya tanganyika bado katiba ya znz itaendelea kusomeka kama inavyosomeka sasa.

Na hata hii katiba inayopigiwa ukunga haiandikiki ikaisha leo ni jambo ya muda 2,3,4,5 years pengine so meanwhile tunayo hii ya sasa "titi la mama tamu hataka kama la mbwa" tuiheshimu na kuheshimu maoni ya wananchi wa Zanzibar tusiwabeze na kuwajeli. Nadhani CDM inahitaji wanachama kule ili kiwe na sura ya kimuungano zaidi basi ushauri wangu ni kuwa wasiwadhihaki wazanzibar kwa maneno ya kejeli wao ndio waliopiga kura za maoni na si kama inavyozungumzwa na viongozi wa CDM kuwa CCM na CUF wao ndio wamepanga.
 
Mkuu swali lako ni zuri na ni swali makini, lakini nina uhakika DR Slaa hawezi kukujibu swali hili kiufasahaa kwa sababu za kiitifaki, lakini kwa raia huru kama mimi ambae sina cha kupoteza naweza kukujibu kiufasaha kabisa kama una nia ya dhati kulijuwa hili.

Ni hivi mpaka sasa muungano wetu ni mashaka, wapo raia wa kawaida wa bara na visiwani ni marafiki wa damu kabisa, lakini ukichukulia kiujumla Wazanzibar wao hawajivunii Utanzania HATA ukutane na Mzenj U.S.A, U.K, CANADA, SOUTH AFRICA e.t.c utamsikia anajitambulisha kwamba anatoka Zanzibar na sio Tanzania, kumbuka U.K kuna Wiles, scot, isle man e.t.c lakini hawa hujitambulisha kwamba i come from U.K, kiufupi Watanganyika wanabaguliwa na Wazanzibar, hakuna chama kingine chochote kitakachoweza kuvishinda vyama hivi viwili kule zanzibar yaani CCM (ASP) nA CUF (HIZBU) SIPENDI KUWACHOSHA WASOMAJI MAANA SWALI LAKO LINAHITAJI MAJIBU KWA MAKALA NZIMA.
 
Nadhani Chadema ilishasema ikiingia madarakani katiba itabadilika na kwahiyo mambo ya serikali zitakuwa ngapi na vipi zitaendana na hiyo katiba na sio katiba ya sasa

Duh patamu basi hapo yaani mpaka wakiingia madarakani wataandika katiba mpya? je itakuwa ya matakwa ya nani? maana nyota njema huonekana alfajiri ikiwa leo hawataki kushirikiana na vyama vya upinzani na kutafuta mantasababu wakishika nchi itakuwaje? Mie I can smell something fishy here.....
 
Mkuu swali lako ni zuri na ni swali makini, lakini nina uhakika DR Slaa hawezi kukujibu swali hili kiufasahaa kwa sababu za kiitifaki, lakini kwa raia huru kama mimi ambae sina cha kupoteza naweza kukujibu kiufasaha kabisa kama una nia ya dhati kulijuwa hili.

Ni hivi mpaka sasa muungano wetu ni mashaka, wapo raia wa kawaida wa bara na visiwani ni marafiki wa damu kabisa, lakini ukichukulia kiujumla Wazanzibar wao hawajivunii Utanzania HATA ukutane na Mzenj U.S.A, U.K, CANADA, SOUTH AFRICA e.t.c utamsikia anajitambulisha kwamba anatoka Zanzibar na sio Tanzania, kumbuka U.K kuna Wiles, scot, isle man e.t.c lakini hawa hujitambulisha kwamba i come from U.K, kiufupi Watanganyika wanabaguliwa na Wazanzibar, hakuna chama kingine chochote kitakachoweza kuvishinda vyama hivi viwili kule zanzibar yaani CCM (ASP) nA CUF (HIZBU) SIPENDI KUWACHOSHA WASOMAJI MAANA SWALI LAKO LINAHITAJI MAJIBU KWA MAKALA NZIMA.

Kwa hilo nakubaliana na wewe na ujue pia muungano tunaoujua mimi na wewe ni tofauti na wanaujua kina Seif Sharif na Mzee Aboud Jumbe na Mzee Karume. Mzee Karume kuna kipindi alipoona anabanwabanwa na Nyerere alinukuliwa kuwahi kusema "muungano ni kama koti likikubana unalivua"

Pia ikumbukwe kuwa ziliungana nchi mbili wazanzibari wana taifa lao na bado lina exist kwahiyo tusiwaonee choyo na wivu tumtafute mchawi wetu alieiuza nchi yetu ya Tanganyika ikaondoka kwenye uso wa dunia.

Kuhusu CCM (ASP) na CUF (HIZBU) kuna mikakati ya haja kuiweka mizizi ya CHADEMA (UMMA PART) zanzibar wale wa umma part ya Abdulrahman Babu wataingia hapa na mchezo utanoga na kuwa mkazi zaidi.

Ua unaonaje mzee?
 
Kwa ninavyovielewa hivyo vichwa yaani Mnyika, Dr wa ukweli Slaa, Mkumbo na Mbowe hawatakuwa na majibu mepesi kama yako. Ni wajibu wa Chama kuwa na mikakati ya kuweza kupenetrate kwenye ngome mpya na kuongeza wigo sitaki kuamini CDM watakaa na kubweteka wasifanye maipango ya kuweza kupata ushawishi Zanzibar. Chama chochote cha siasa lazima kiwe na mbinu za kusaka ushawishi nina imani thabiti kuwa wapo wazanzibari wanaoipenda CDM ni jukumu la CDM kuongeza idadi ya hao wanaoisupport unless CDM haitadumu"iakuwa namaisha mafupi" CDM kama chama cha siasa kisiangalie ya leo tu kiangaze ya miaka 5,10,15,20,25,30 ijayo na kadhalika.

Maswali mepesi stahili yake ni majibu mepesi.
Sasa kama hutaki majibu uliyopewa hapo basi ni dhahiri kwamba ulikuwa na maswali mkono mmoja huku ukiwa na majibu mkono wa pili.
Sasa endelea kusubiri majibu unayotaka ama vinginevyo ujijibu mwenyewe kwa kuwa tayari unayo majibu ya maswali yako. Na pengine watakuja kuomba kwako ushauri jinsi ya kupenetrate zanzibar na kuangaza miaka 30 ijayo kama unavyshauri.
 
Back
Top Bottom