We ulileta stori? au ulimchana live? Huko kwa mshenga na wajomba ndio kaenda kujichora.
nilimchana tu kwa hekima na taadhima.
We ulileta stori? au ulimchana live? Huko kwa mshenga na wajomba ndio kaenda kujichora.
Jamani mimi nimekuwa nikijiuliza hili swali:
Hivi mtu anapoleta shida yake hapa jamvini...hasa inapomhusu partner wake, ni kwamba huyo partner wake yeye huwa hatembelei maeneo haya ya JF??? Maana jinsi wahusika wanavyo elezea the whole situation, inakuwa so detail! mbona inakuwa rahisi kwa partner kujua kwamba hii inafanana na ya nyumbani kwake? Je, hauoni kuwa unaweza ukasababisha kukosekana kwa amani nyumbani , partner wako akianza kuhisi kuwa umesimulia jamii matatizo yake??
Nyie mnasemaje hapo?
Mara nyingi tu mimi nimehitimisha hivyo kwamba partner anayeandikwa kama anaingia huku atajijua kwamba mwenzake kaja kumchora huku. Kwa mfano yule anayependa perfume za mwenzie na hata hununua perfume za kike kama huwa anaingia huku atajifahamu tu kwamba kachorwa kwenye jamvi.
jf imeingiliwa! Nasema hivyo coz watu sasa badala ya kuleta mada zenye mashiko na zinazoibua hisia zetu vijana(hasa kuhusu umaskini wa nchi yetu na uongozi mbovu) tunajadili kuchorana kwa patna! Tupo makini kweli?
Asanteni kwa mawazo yenu. Ni kweli matatizo yanaweza yakawa yanafanana kwa wengi, ila kuna wengine kweli wanatoa detail za kutosha kabisa kujua hapa ni mimi nasemwa! Na sio rahisi kubadilika kwa haraka hivyo, kwamba umemuanika hapa jamvini akajiona then ajirekebishe!!?? sina uhakika kwa kweli!
Ila mimi ninavyofikiri na kuamini, ukiona partner wako ana tatizo kwanini usimwambie, ili mjaribu kutatua tatizo kwa pamoja na kutafuta ushauri kwa wengine???! Ninaamini katika mawasiliano ya pamoja, yanapelekea kujenga upendo zaidi na kuaminiana kuliko kupelekea jamii kwanza!!!
Kama litakuwepo tatizo basi nitaanza kumweleza kwanza yeye, then tutashauriana wapi tufatute msaada, Kama ni hapa JF basi tutakuja![/QUOTE]
Mhhhhh! Ni aje bana!? Check your emails.
Nadhani hapa anaongelea details kama nilikutana nae sehemu fulani baada ya kuongea nae hapa na akasema A, B, C na baadae tukafanya A, B baada ya kumjibu C, D, E... hivyo basi katika probability uwezekano ni mdogo sana mambo mawili kama haya kutoa kwa watu wawili within a short time.., mtu ukiangalia tu utahisi its me she/he is talking aboutSi watu wanauliza anonymously? Ni sawa na wale wanaouliza magazetini.
Kwani kuna mtu alikuja kusema mpenzi wangu fulani bin fulani?
Wanaongea tu kuhusu situation, na wanapewa suluhisho.
Mpenzi akiona nae analeta mada: hili la kuleta tatizo la ndani hapa JF imekaaje?
Could be trues huenda kweli ni Couple wana enjoy and this is like a game to them, pia huenda sio couple bali its the same person with multiple id's disorder... anything is possible.. (lakini sioni tatizo kama story ni plausible hata kama ni ya kutunga so long as it help others through the story)Kuna couple humu ndani hua wanaeleta sana matatizo yao.
Ukisoma tu thread zao, na majibu yao utajua jana walilalaje. lol
But siku hizi siwaoni, wote wawili.