Swali kwa WAMAMA wenye watoto: Hivi kwa nini huwa mnafanya hivi???

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
70,955
93,932
Leo ni siku ya mapumziko ya mwisho wa wiki na nimejipumzisha kitandani kwenye hiki kibanda changu cha kupanga.
Mkononi nimeshika kijarida cha Sani na nafuatilia visa na vioja vilivyochorwa kwa mtindo wa vikaragosi na kuchagwizwa na maneno.
Ghafla nje ya chumba nilichopo ninasikia mwanamke akiporomosha matusi ya nguoni, nami nashusha kijarida chini ili nipate kusikia ni zogo gani linaloendelea(umbea suna huku uswahilini kwetu).

"We mwanaizaya hebu kuja hapa, hivi wewe nilikuzaa au nilikujamba?
Hebu nieleze mwana wewe usiye na haya, kwa nini umekula nyama zote kwenye sufuria?
Baba yako mwenyewe kutwa anazurura tu huko mtaani kama gari la taka na wala hanijali.
Mbwa mkubwa we kasoro mlio, na ukome kabisa kufunuafunua masufuria bila kuniambia.
Haya hebu nitokee hapa kabla sijakutukana...fyoooooooo(msonyo kama ule wa Ndoa ndoana kwenye Orijino Komedi)."

Huyo alikuwa ni Mama Wawili akimchachafya mwanae Kibakuli, na hiyo si mara ya kwanza kufanya hivyo kwa mwanae.

Sasa hapa nauliza swali kwa wamama, hivi ni kwa nini huwa mnaporomosha matusi mazito mazito kwa wanenu wa kuwazaa???
Hakuna namna nyingine ya kuwakanya wanenu hadi mtoe single na kuwashikia vipaza kama hivyo??

Karibu kujadili...

Copy to: Nivea, Lisa, King'asti, AshaDii, MwanajamiiOne, afrodenzi, Kongosho, BADILI TABIA, Paloma, mwaJ, Swts, Madame B, MadameX, Mamndenyi, Preta, marejesho, snowhite, Angel Msoffe, sweetlady, FirstLady1, FirstLady, Remmy, Zion Daughter, Kipipi, Roulette, Smile, Asnam, Binti.com, lara 1, Mrembo by Nature, Raiza, cacico, gfsonwin, Jeska, Lusile
 
sasa tunajadili nini hapa!!!mi situkanagi

Sasa hapa nauliza swali kwa wamama, hivi ni kwa nini huwa mnaporomosha matusi mazito mazito kwa wanenu wa kuwazaa???
Hakuna namna nyingine ya kuwakanya wanenu hadi mtoe single na kuwashikia vipaza kama hivyo??
 
Kutukana mtoto matusi ya nguoni kunaelezea mambo mengi
Kwa uchache yanaweza kuwa

1. Background ya mama, kama kalelewa kwenye matusi tegemea matusi
2. Mahusiano ya baba na mama, kama ni mabaya hasira zinaelekwa kwa product
3. Frustrations za maisha kwa ujumla, zinaelekezwa kwa mnyonge ambaye ni mtoto
 
Leo ni siku ya mapumziko ya mwisho wa wiki na nimejipumzisha kitandani kwenye hiki kibanda changu cha kupanga.
Mkononi nimeshika kijarida cha Sani na nafuatilia visa na vioja vilivyochorwa kwa mtindo wa vikaragosi na kuchagwizwa na maneno.
Ghafla nje ya chumba nilichopo ninasikia mwanamke akiporomosha matusi ya nguoni, nami nashusha kijarida chini ili nipate kusikia ni zogo gani linaloendelea(umbea suna huku uswahilini kwetu).

"We mwanaizaya hebu kuja hapa, hivi wewe nilikuzaa au nilikujamba?
Hebu nieleze mwana wewe usiye na haya, kwa nini umekula nyama zote kwenye sufuria?
Baba yako mwenyewe kutwa anazurura tu huko mtaani kama gari la taka na wala hanijali.
Mbwa mkubwa we kasoro mlio, na ukome kabisa kufunuafunua masufuria bila kuniambia.
Haya hebu nitokee hapa kabla sijakutukana...fyoooooooo(msonyo kama ule wa Ndoa ndoana kwenye Orijino Komedi)."

Huyo alikuwa ni Mama Wawili akimchachafya mwanae Kibakuli, na hiyo si mara ya kwanza kufanya hivyo kwa mwanae.

Sasa hapa nauliza swali kwa wamama, hivi ni kwa nini huwa mnaporomosha matusi mazito mazito kwa wanenu wa kuwazaa???
Hakuna namna nyingine ya kuwakanya wanenu hadi mtoe single na kuwashikia vipaza kama hivyo??

Karibu kujadili...

Copy to: Nivea, Lisa, King'asti, AshaDii, MwanajamiiOne, afrodenzi, Kongosho, BADILI TABIA, Paloma, mwaJ, Swts, Madame B, MadameX, Mamndenyi, Preta, marejesho, snowhite, Angel Msoffe, sweetlady, FirstLady1, FirstLady, Remmy, Zion Daughter, Kipipi, Roulette, Smile, Asnam, Binti.com, lara 1, Mrembo by Nature, Raiza, cacico, gfsonwin, Jeska, Lusile/FONT][/SIZE]
[/QUOTE]

Mara nyingi wamama wa hvo wanakuwa wana frustration za kuachwa, kuachiwa malezi wenyewe kwani wababa hawatimizi wajibu, au ndo tabia yake tu kutukana....
 
Hahahahahahaaaaaaaaaaa!!!!!! mimi umenifurahisha hapo "baba yako anazulura kama gari la taka"Loh!!!! sasa huyo mtoto siku akijamuona babaye si atamwambia kuwa yeye ni gari la taka.

Unajua mambo kama hayo yanatokana na ugumu wa maisha, na mara nyingi huku kwetu uswahilini unakuta mama mmoja kazaa watoto 5 na kila mtoto ana baba yake, wanaume wote hao wamemzalisha na kuondoka hakuna aliyemuoa, so anakuwa na msongo wa mawazo, ni jinsi gani atawalea, na kuwasomesha hao watoto, kwa hiyo unakuta hasira zooote za baba zinaishia kwa watoto.
Tena huyo kamtukana vizuri wengine wanawaita watoto wao majina ya viungo vya uzazi, mpk unabaki unashangaa, mm ilibidi niweke vioo kwangu ili nikiwa ndani nisisikie ya nje.maana huwa yanakuwa makubwa kiasi ambacho unajiuliza kuwa yule ni mwame au la!
 
Aisee.....naona kwa madai yake alikuwa hajaanza kutukana!

Anyways, wachangiaji waliopita wamesema yote, mimi nafikiri inalalia zaidi kwenye tabia ya mtu (ambayo obvious inatokea mbali, kwenye malezi yake mwenyewe) na frustrations za mtu kuachiwa malezi (si unaona kuna reference ya 'mtu anayezurula kama gari la taka - ningekuwa karibu nahisi ningecheka kwa nguvu...ama kuna watu wana maneno!)

Ila sio jambo jema, kwa sababu mama wa hivi anaongezea tu msururu wa wazazi watakao kuwa wanaporomosha matusi kwa watoto wao hapo siku za usoni....
 
Kitendo cha kutoa matusi na lugha chafu maranyingi hutokana na malezi au mazingira anayoishi mtu kuna mwingine unakuta mtoto hajamkosea kitu ila utamkuta anamuita majina ya ajabu mfano "we mbwa njoo hapa" au we ms***nge njoo hapa" wa mama wa style hii wapo wengi sana hasa USWAHILINI na wao kufanya hivyo wanaona ni sawa na nikitu cha kawaida na ndio njia ya kumuadabishamtoto kama huyo jirani yako alivyofanya.

Kiukweli kumtusi mtoto na kumtolea maneno machafu sio njia nzuri ya kumuonya mtoto na haimjengi bali humuaribu, kuna njia nyingi nzuri tu na za kiustaarabu unaweza kutumia kumuonya mtoto na akakuelewa na kutii pia, sio kumporomoshea mtoto matusi utafikiri unagombana na mke mwenza.

Kumbuka mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
 
....mhhhh watu8 kikubwa ni malezi na matatizo ya maisha, lakini sio justification ya kumtukana.
mtoto kama huyo unamnunulia nusu kilo ya nyama unampa yote yeye pekee..........hahahahaaa manake yaonyesha ana hamu sana na nyama! Lol!:mvutaji:
 
Last edited by a moderator:
Hata hausigelo kuiba mboga marfuku

Wee ukiona anapenda sana nyama, anza kununua extra kwa ajili yake bila kumwambia

Miezi 3 haiishi, unamkuta kashindia chai ya rangi hana habari na mboga

Utumbo ukiwa na njaa hata ufanyeje, mtu atadokoa tu

....mhhhh watu8 kikubwa ni malezi na matatizo ya maisha, lakini sio justification ya kumtukana.
mtoto kama huyo unamnunulia nusu kilo ya nyama unampa yote yeye pekee..........hahahahaaa manake yaonyesha ana hamu sana na nyama! Lol!:mvutaji:
 
Heheheh...akizoea sana nyama si ndio kama haya ya kutaka kudokoa chunguni..

....mhhhh watu8 kikubwa ni malezi na matatizo ya maisha, lakini sio justification ya kumtukana.
mtoto kama huyo unamnunulia nusu kilo ya nyama unampa yote yeye pekee..........hahahahaaa manake yaonyesha ana hamu sana na nyama! Lol!:mvutaji:
 
mweeee... leo umepania watukanaji lolz.
Kongosho amejibu vizuri sanaa, ingawa naona hzi tabia zimekaaa za ki uswahilini sana na za wamama wasio kuwa na busara. Wakati mwengine aina ya malezi huyo mama aliyolelewa inaweza kumfanya yeye kuwalea wanae vivyo hivyo.

Nachukia hii tabia.. na ukiachia mbali mapungufu ya kibinadamu huwa namwomba Mungu aniongoze niweze kuwalea vyema watoto atakaonijalia.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo kitu nimekujakugundua ni common sana mikoa ya Pwani....Kwatu bara sio kivile sana...huku adhabu kubwa ni tusi bila kujali kama mhusika anajitusi mwenyewe au anamtusi nani!
 
lolote unalomtendea mtoto litakurudia wewe kama mzazi
mfano ukimtukana mtoto tegemea nawe kutukanwa au kudharauliwa na mwanao
mtoto ukimpa sifa kwa jambo dogo tegemea atafanya makubwa zaidi ya kupendeza
wazazi jengeni tabia ya kuwasikiza watoto wenu,
wanapokosea waonyeni kwa upendo na furaha,kiboko au matusi ni kuharibu akili za watoto.
jaribuni kuchunguza watoto wanaofanya vizuri darasani ni wale ambao wazazi wao huwa nao karibu,huwapa moyo
huwakosoa kwa upendo na huwasikiliza.
kamwe usimchagulie mtoto masomo asiyo taka na kamwe usimchagulie mtoto future,mwache yeye mwenyewe achague.
huyo mama anaemtukana mwanae ategemee kuzalisha jambazi,kibaka au mtu mkorofi sana ktk jamii.
 
Back
Top Bottom