Swali kwa Mheshimiwa Membe kuhusiana na Sakata la Gesi Mtwara

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,056
5,361
Wana JF,

nimekua najiuliza mambo meeeengi sana moja wapo ni Mh Membe anatokea Lindi/Mtwara maana jimbo lake
linapkana na mikoa yote miwili Lindi na Mtwara.

Ndugu huyu amekua anajipitisha kwa wanachama wa chama chake ili wamchague kuwa mgombea kiti cha urais
uchaguzi ujao (mimi sina shida na hilo).

lakini pia ni mbuge mmojwapo mwenye influence kuubwa sana kwenye kanda ya kusini kama mmbunge na waziri pia.

sio hapo tu Mh. membe ni mjumbe wa Kamati kuu ya CCM
.

Kwa maana nyingine anauwezo wa kupata taarifa sahihi, kushawishi wadau husika (serikali na wananchi) na kuhakikisha suala la Gasi linakwisha bila umwagaji wa damu tulioanza kuushudia.


SWALI KWA MEMBE: Ni kwa nini unahisi unaweza kuwa Rais wa nchi hii kushughulikia mambo makubwa ya kitaifa na kimataifa kama umeshindwa suala la MTWARA?


Ni kitu gani kina kupa kigugumizi ama kinakufanya usiwe msuluhishi mkuu wa mgogoro huo?


UKISHINDWA KUJIBU MASWALI HAYA, NAAMINI HUFAI KUGOMBEA KITI CHA URAIS maana kama hili dogo huwezi
hayo makubwa hutaweza.
 
ngoja tumsubiri ayajibu halafu tutarudi tujadiliane juu ya majibu yake.
 
ngoja tumsubiri ayajibu halafu tutarudi tujadiliane juu ya majibu yake.

Mwenyewe kapiga kimya ka halimhusu vile!!!Astakafirullah.MAULANA tumulikie waja wako.AMIN.
 
Mh.Benard Membe tunakutaka uje hapa jamvini ujibu haya,Kwanini unaona unaweza kuongoza Tanzania wakati huu mgogoro wa Mtwara umekaa kimya?Where are your skills in resolving conflicts?
Huu mgogoro ndio kipimo tosha kama kweli wewe unaweza kuwa fifth president of Tz
 
Umeona mtu yeyote wa Mtwara/Lindi anajihusisha na mambo ya kusuluhisha mgogoro wa gesi?
Si Membe , si MKAPA, si Mathias Chikawe, wote kimya kabisa, kama vile hawapo!
Nina shaka hawa wameji'side na upande fulani!
 
Mimi nafikiri kuiongoza tz nirahisi kuliko mnavyodhani, watz ni wasikivu sana ndugu.
 
Kama Membe anahusika na huu mradi wa vurugu za Mtwara basi anafit kabisa kufikiriwa kuwa Mgombea Urais,
 
Umeona mtu yeyote wa Mtwara/Lindi anajihusisha na mambo ya kusuluhisha mgogoro wa gesi?
Si Membe , si MKAPA, si Mathias Chikawe, wote kimya kabisa, kama vile hawapo!
Nina shaka hawa wameji'side na upande fulani!
Wanaogopa kuchomewa nyumba zao!
 
Sangarara,
Una pwenti fulani kali sana kichwani, lakini hutaki wenzako wafaudu!

PakaJimmy
labda kama unataka niongee maneno mengi, Bila kumtaja Membe, kwa wanaofuatilia harakati za namna inayoendelea Mtwara kama zinavyoendelea kutokea maeneo mengine na kwa mujibu wa Historia, nyuma yake huwa kuna watu wakubwa sana kwa maana ya nyadhifa za kisiasa au kiukwasi huwa wako nyuma yake kwa ama nia ya hovyo au ya heri kwa wananchi.

Kwa mtwara, fujo zinazoendelea ni za manufaa kwa wananchi, sio wa mtwara tu bali kote east africa na pengine ambako mafuta na mazao yao yamekutikana, tatizo ni kwamba wajasiriamali wa kifisadi bado wanaona opportunity za kujineemesha wao kama hawa ambao wamekwisha kula chao sasa.

Kama ni kwa heri, Membe is right
 
Mkoa wa mtwara hawana mwakilishi, kwa mara ya mwisho walikuwa na mbunge mmoja mbishi sasa ni marehemu Mzee Nandonde.....................baadaye hamna kitu, huyu membe kazi yake ni kukusanya hesabu toka balozi zetu basi........
 
Membe hana nafasi ya kutushawishi wanaMtwara tukamwelewa. Ana-indluence jimboni Rwangwa, gesi inatoka Mnazi bay, nearly 170 km from Rwangwa. After all wanaMtwara tunamchukulia Membe kama mwekezaji wa kawaida hapa Mtwara. Tulisham-disqualify looong time kuwa prezdaa wetu.
 
Membe hana nafasi ya
kutushawishi wanaMtwara tukamwelewa. Ana-indluence jimboni Rwangwa, gesi
inatoka Mnazi bay, nearly 170 km from Rwangwa. After all wanaMtwara
tunamchukulia Membe kama mwekezaji wa kawaida hapa Mtwara.
Tulisham-disqualify looong time kuwa prezdaa wetu.

Membe kawekeza hapo Mtwara? hebu tupe habar ndugu! Kuhusu membe kuhusika hapo sina neno jaman mm napita hapa.
 
Membe hana nafasi ya kutushawishi wanaMtwara tukamwelewa. Ana-indluence jimboni Rwangwa, gesi inatoka Mnazi bay, nearly 170 km from Rwangwa. After all wanaMtwara tunamchukulia Membe kama mwekezaji wa kawaida hapa Mtwara. Tulisham-disqualify looong time kuwa prezdaa wetu.

Mawaiba, nachelea kusema kwamba wewe si mkazi wa Mtwara. Yaani hata ujui Membe ni mbunge wa jimbo gani na wala gas inayosababisha vurugu inatoka wapi. Sasa kama hujui haya utatuaminisha vipi hayo ya Membe kuwekeza?

Membe hana kitega uchumi Mtwara, ni wapinzani wake tu wamekuwa wakihusisha vitega uchumi vya Shebi matelephone na ukaribu wake Membe na Shebi. Mzee wa mamvi alituma watu wake Mtwara kwenda kujaribu kumuhusisha Membe na hoteli ya Shebi mix na kuambulia patupu. Kama kuwekeza Membe angewekeza kwao Lindi kuliko gundulika gas nyingi mara tatu ya gas ya Mtwara. Tatizo la watanzania ni kuzani kila mwanasiasa ni mfanyabiasha wa aina ya mamvi na tujisent.

Kutaka Membe atoe tamko juu ya gas kwenye wizara ambayo hausiki na mkoa ambao hausiki ni jaribio jingine la kundi la mamvi kutafuta wimbo wa kutokea. Membe ndiye aliyeufanya moto wa gas usiingie Lindi baada ya kuongea na viongozi 300 wa Mkoa wa Lindi.

Na sisi JF wakati mwingine tunasikitisha; jana umeletwa uzi wa Membe kuchochea vurugu Mtwara leo tunamtaka aje atoe tamko.
 
Hataki lawama kote. Kwa wapiga kura na kwa tajiri yake jakaya

Mwenyewe kapiga kimya ka halimhusu vile!!!Astakafirullah.MAULANA tumulikie waja wako.AMIN.
.......MSIMAMO WA MEMBE NI WAZI NA WALA HAYUKO KIMYA, NAPENDA SANA STAILI ANAZOTUMIA HUYU JAMA....AKIONGEA MURJI (MB) WA MTWARA MJINI, NDIO MSIMAMO WA MEMBE.....LAKINI HII YOTE HAITOSHI KUFANYA SIO TU KUWA RAIS AJAYE BALI HATA SIFA ZA KUWA RAIS HAZIJAI KIGANJA (maoni yangu tu lakini)
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom