Swali kwa Anna Kilango: Je, Kikwete alitutapeli kuhusu barabara ya Mkomazi-Same?

bangusule

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
291
190
ndugu zangu,
wakati wa kampeni za uchaguzi Jakaya Kikwete aliomba kura kwa wananchi wa Same Mashariki kwa ahadi kwamba atajenga barabara ya Mkomazi-Bendera-Kihurio-Ndugu-Gonja-Kisiwani-Same kwa kiwango cha lami. ahadi hiyo ilitolewa katika mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini Ndungu na Anna Kilango Malecela alikuwepo ktk mkutano huo.

wananchi walifurahishwa sana na ahadi hiyo. wananchi walicheza ngoma kwani walimwamini Kikwete kwa jinsi alivyotoa ahadi ile kwa kujiamini. barabara ya mkomazi-same imekuwa kilio cha wananchi wa wilaya ya same kwa kipindi kirefu toka tupate uhuru. barabara ilikuwa barabara kuu ya kuelekea Moshi-Arusha-Nairobi, kabla haijabadilishwa kwa kupelekwa upande wa magharibi ikienda msanjari ya reli ya kwenda Moshi.

mwingine aliyeahidi kujenga barabara hii ni Daniel Yona Ndhira. ilipoonekana kwamba ametutapeli, wananchi waliamua kumuondoa ubunge, bila kujali kwamba alifanikisha ujenzi wa sekondari katika kata 13 kati ya 14 katika jimbo letu. Yona alipelekewa taarifa tangu mwaka 2003 kwamba asijisumbue kugombea tena.

mimi bangusule na wananchi wengine wenye mtizamo kama wangu tunaamini Raisi Jakaya Kikwete hastahili kura zetu kwa mwaka 2010. tunashangazwa na kauli za mbunge wetu Anna Kilango Malecela na Shemeji yetu Mzee John Samuel Malecela kwa kumpigia debe Raisi Kikwete apite bila kupingwa na wanachama wenzake wa CCM.

Uraisi una vipindi viwili tu, hivyo unapompigia kura mgombea kipindi cha pili ni kumpa nafasi amalizie yale aliyoanzisha. humpigii kura kwa ajili ya ahadi mpya.
 
Ahadi nyingi tu hazijatekelezwa, lakini tambua kwamba kwa gharama yoyote JK atapita kwa ushindi wa kishindo come 2010

ha ha habari ndiyo hiyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom