Swali kuhusu internet package ya Airtel

voda kwa mchana hasa mikoani ni kimeo tu, hadi utegee usiku sana mambo yote Airtel na 400Mb natumia zaidi ya wiki na ninadownlod vitu kibao
 
mi nilinunua modem ya voda garama zilikuwa kubwa, nikaichakachuwa sasa natumia airtel nakula bata 24 seven
 
natumia airtel nakula bata 24 seven

Hongera mkuu, mimi hao jamaa jana wamenifanyia kitu mbaya sana, nimejiunga na package ya ya 3gb kwa elfu 15000 ndani ya dakika 30 pasipo kudownload chochote niliambiwa nimemaliza 3gb. Sina hamu nao tena.
 
Mkuu nadhani labda ilitokea matatizo ya kiufundi, ni wezi lakini sidhani kama ni wezi kiasi hicho,3gb kwa dk30 iwe imekwisha? hata kama kuna updates automatic kwa speed ipi ya kumaliza 3gb kwa dk30?
jaribu kucheck nao may be kunamakosa yalifanyika.
 
Hongera mkuu, mimi hao jamaa jana wamenifanyia kitu mbaya sana, nimejiunga na package ya ya 3gb kwa elfu 15000 ndani ya dakika 30 pasipo kudownload chochote niliambiwa nimemaliza 3gb. Sina hamu nao tena.

Mkuu inawezekana hukumalizia utaratibu wa manunuzi wa hizo gb, nilazima mwisho u-reply msg kwa neno yes kama hukufanya hivyo basi kosa ni lako.
 
ok! Hata mimi iliwahi kutoke lakini baadae kama sitatu mbele walinirudishia wenyewe bila ya kuwasiliana nao, watakurudishia tu.

Aisee! nitashukuru sana kama watafanya hivyo maana wamenikatisha tamaa kabisa.
 
Jee TTCL wameacha ule mpango wao wa kukata ikifika tarehe 30/31 ya mwezi?

Mimi huwa inaniboa kweli maana sometimes unakuwa mikoani ukirudi unataka uunge lakini tayari imefika kati ya mwezi basi lazima ufikiri mara kumi kwanza.
 
Kabisaa,
Vodacome is the best. Chukua unlimited ya wiki moja ama kwa mwezi. Hakuna tena usumbufu.
 
Kabisaa,
Vodacome is the best. Chukua unlimited ya wiki moja ama kwa mwezi. Hakuna tena usumbufu.

Mkuu unlimited speed yao kichefu chefu, kama ni mtu wa kudownload kwa sana hata haifai wala kuangalia youtube ni balaa.
Lakini kama kusurf kawaida jf, fb nk haina kwere
 
ZAIN aka Airtel aka Celtel aka TTCL aka MIC

ZAIN.jpg

Ukiangalia vizuri hizi takwimu zipo daily, monthly, yearly - daily inaweza kukupa mwanga wa nini ume-down-up-load kwa siku and yearly/monthly ni cumulative..

Mkuu wakati mwingine linatokea tatizo la kimtandao, kuna siku niliingiza kama 10,000 hv kwa kununua zile 400MB ambazo ni shilingi 2,500 sababu kila nikiweka natumia kidogo naambiwa hela imeisha, lakini baada ya siku kama 3 hv nilipokea sms kutoka Airtel wakiomba radhi kwa tatizo la kimtandao kwahiyo waliniwekea MB zenye gharama ya pesa niliyokuwa nikiweka.

Lakini kwa sasa nimehama kabisa AIRTEL nimeingia VODACOM ambapo nanunua bundle ya UNLIMITED siku 7 kwa 10,000 au bundle ya UNLIMITED mwezi mmoja kwa 30,000. Na-download hadi movies bila shida! Jaribu INTERNET YA VODACOM mkuu.

Hapo kwenye bold, hata mie ilinitokea. Kwa kuwa sometimes nakuwa porini, huwa natumia simu km modem. Nili surf muda mfupi sana na nikaambiwa kwamba salio langu limeisha. Niliboeka sana ukizingatia kwamba nilikuwa na kazi kibao za kufanya katika mtandao! Zain ni kimeo

Nikitaka kupata 400mb za airtel kwa 2,500 nifanyeje? Nimewapigia customer service, hata hawapokei simu na website yao haionyeshi bundle rates

Kuna ujumbe fulani unatuma katika namba zao.
Kwa habari zaidi hebu pitia hapa http://www.africa.airtel.com/tanzania/broadband-tariff-216

Hongera mkuu, mimi hao jamaa jana wamenifanyia kitu mbaya sana, nimejiunga na package ya ya 3gb kwa elfu 15000 ndani ya dakika 30 pasipo kudownload chochote niliambiwa nimemaliza 3gb. Sina hamu nao tena.

Pole. Ila voda pamoja na kwamba nimeitumia kwa muda mfupi, iko safi sana, nimeenda spidi yao na hawakati pesa ovyo ovyo kama zain.
 
Pole. Ila voda pamoja na kwamba nimeitumia kwa muda mfupi, iko safi sana, nimeenda spidi yao na hawakati pesa ovyo ovyo kama zain.

Mkuu, voda unatumia package gani? Na speed yake inafika kbps ngapi.
 
Kama kweli upo makini internet ya Airtel ndio ya kutumia, tatizo la Voda na hiyo unlimited ni wanabana speed downloading and uploading unafungua yahoo tu net inakuna nazi sana, unaenda kuoga unarudi bado inazunguka mambo gani hayo? Tuzungumze ukweli kwa zama za sasa hivi downloading nyingi ni za vitu vidogo vidogo sana ambayo Airtel inaweza kukufaa, kwa jinsi watu walivyokuwa makini sitegemei udownload software ya maana bure sana sana zinakuwa ni demo/trial version ambazo zinakuwa hazina dili. Ukitaka ujue ukweli angalia watu ambao wanakomaa sana na software za bure uone wanavyohangaika, mwangalie mtu ambaye amepata Window 7 ya ujanja ujanja anavyoteseka kidogo tu inakuja message get guinine window, au hata mwenye window vista ya ujanja wanabaki kuhangaika tu. angalia pia wanao download free antivirus ni tabu tupu. Yaani ukiwa na software za namna hiyo usiunganishe computer kwenye net, ukiweka tu kosa wameshavinjali na kublock.
 
Andika neno internet na tuma 15444 na utajibiwa kuwa unataka kununua 400 MB kwa 2,500.00. Itakubidi ujibu ndiyo. Baada ya hapo kula bata, mambo yote Airtell. Speed ya uhakika gharama nafuu.

Mkuu hii 400MB ina limitation gani kwenye muda wa matumizi? Inatakiwa itumike katika muda gani, mm nina modem ya Airtel ila napata shida sana na hizi package zao za siku & wiki!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom