Swali gumu:Nani kuongoza kampeni za CCM Arusha mjini?

Kama ccm wanataka kushinda jimbo la Arusha mjini hawanabudi kulifuta au waliunganishe na jimbo la arumeru magharibi vinginevyo hesabuni maumivu :kev:
 
Tatizo la CCM si mtu wa kugombea bali ni Chama Hata Dr slaa akaamua kurudi CCM na akagombea bado atakosa, tatizo si watu wa kugombeatatizo ni Chama kimechokwa watu hawataki kusikia CCM hata mkimshusha Yesu aje agombeaa kwa tiketi ya CCM bado atashindwa tu

Wameshindwa kabisa kugundua hili, wamebaki kutumia hela nyingi kununua watu kama kina Kabouru bila tija. Wajue kuwa si kila kitu kinaweza kununuliwa kwa pesa. Na Arusha CCM ndio watakaojutia hukumu ya kutengua ubunge wa Lema.
 
ccm waache hasira wasome alama za nyakati sio kitu cha kusadikika CDM bila kampeni watapita tume ya uchaguzi waitishe tu uchaguzi .Na ccm wasitumie vibaya hela za walipakodi zinahitjika kununua madawati, zahanati, dawa ,vitanda mahospitali,n.k
 
..Kinana siyo msafi bwana, ukizingatia ushiriki wake ktk uuzwaji wa mbuga ya Loliondo.

..pia alishawahi kuwa mbunge wa Arusha mjini, akasepa kugombea mwaka 1995 kwasababu uraia wake ulikuwa na utata.
 
Naamini huyu hakimu aliyetoa hukumu ya kumvua mbunge Lema ana agenda ya siri ya kutaka kuwaongezea umaarufu chadema, kwamba anataka chukua chako mapema waendelee kuumbuka, OK karibuni kwa mara nyingine mgalagazwe tena kwa hapo Arusha ni kifo cha Mende.
 
Wana jf kada mkongwe wa ccm,amenipa taarifa kwamba chenge ndiye atake ratibu kampeni arusha.ccm wameishiwa!
 
Watu wa arusha tumechoka maandamano . Tunataka mtu atakaetusaidia kupata maendeleo na kuipaisha arusha katika nyanja zote za uchumi. Mambo ya kutumiwa kama mfuko wa rambo hatutaki. utalii wa mikutano umeshuka sana hapa Arusha mambo ya ushabiki hatuhitaji .
Tayari mmeanza kununuliwa mapemaaaa but tutapambana nanyi sana je wewe unaishi hapa Arusha au umetumwa tu. Kesho njoo viwanja vya NMC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom