Swali fupi kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Hivi karibuni Mh. Pinda ulitembelea nchi za Asia ikiwemo India. Kwa muda mrefu umekuwa ukilalama kwamba watendaji wenzako ktk serikali wanapenda magari ya gharama kubwa kama vile Landcruiser VX na kadhalika.

Sasa ulipotembelea India uliona mwenyewe kwamba hata waziri mkuu wa India ambaye kwa India ndiye mwenye madaraka ya kuongoza serikali anatembelea gari ndogo ya gharama nafuu sana. Pia viongozi wote wanatumia magari madogo ya kawaida kabisa.

Si kweli kwamba wahindi hawapendi magari ya anasa, nadhani jibu unalo kwani unaona wahindi wanaoishi Tanzania walivyo na magari ya kifahari sana. Ukweli ni kwamba serikali ya India inadhibiti matumizi yake ipasavyo.

Sasa swali langu kwako ni kwamba je, umeshindwa kushughulikia watendaji wa chini yako na wewe mwenyewe ili serikali yako iweze kupunguza matumizi ya magari ya gharama kubwa na anasa??

Naomba jibu.
 
Natumaini Mh Pinda ataliona swali hili kwani JF ni mtandao wa jamii yote na yeye anakaribishwa na namuomba majibu kupitia hapa hapa JF.

Ni kweli ataliona lakini si ajabu akiliona na akaamua kutoliona
 
Wenyewe watajitetea kuwa magari hayo "SUV'S" Yanaendana na mazingira yetu,yani yanafaa kwendae majimboni kutokana na ubovu wa barabara etc...Hata hivyo gharama hizo za mashangingi ingetumika kufacilitate miundo mbinu ili eventually cost iwe ndogo,lakini viongozi wetu i dont think they give a damn about it.
 
Ni kweli ataliona lakini si ajabu akiliona na akaamua kutoliona

Akiliona anaweza kuzungumza bila kutenda.

Mheshimiwa Pinda ana kipawa cha kuzungumza, kutenda anayozungumza sina uthibitisho!

Aliwahi kulalamika kama vile hana madaraka/mamlaka!
 
Hivi karibuni Mh. Pinda ulitembelea nchi za Asia ikiwemo India. Kwa muda mrefu umekuwa ukilalama kwamba watendaji wenzako ktk serikali wanapenda magari ya gharama kubwa kama vile Landcruiser VX na kadhalika.

Sasa ulipotembelea India uliona mwenyewe kwamba hata waziri mkuu wa India ambaye kwa India ndiye mwenye madaraka ya kuongoza serikali anatembelea gari ndogo ya gharama nafuu sana. Pia viongozi wote wanatumia magari madogo ya kawaida kabisa.

Si kweli kwamba wahindi hawapendi magari ya anasa, nadhani jibu unalo kwani unaona wahindi wanaoishi Tanzania walivyo na magari ya kifahari sana. Ukweli ni kwamba serikali ya India inadhibiti matumizi yake ipasavyo.

Sasa swali langu kwako ni kwamba je, umeshindwa kushughulikia watendaji wa chini yako na wewe mwenyewe ili serikali yako iweze kupunguza matumizi ya magari ya gharama kubwa na anasa??

Naomba jibu.

Tatizo nilonalo mimi hapa si mh.Pinda kwani maamuzi makuu kama hayo hawezi kufanya peke yake ladba nadhani wawakilishi wetu Bungeni wajenga hoja na mmoja atoa hoja binafsi ili bunge iishauri serikali kwa utekelezaji zaidi
 
Umejitahidi lakini itabidi utumie uhuru wako wa maoni na kujieleza ulichonacho kwa kumtumia barua ofisini kwake.
 
Swali ni zuri ila jibu lake huwezi kulipata kabisa..... labda wajukuu zako ndio wataweza kulijibu na kulitatua sio karne hii
 
Back
Top Bottom