Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi?

Mapinduzi kwa ccm ni kutoka hapa kwenda paleee kama kikwete alivyosema antaka watz wamkumbuke kwa lipi. Kwa hiyo kwa ccm ndo maana yao hapo.
 
....wameshindwa kuakisi maana na dhima ya chama chao,,,,instead wamepindukia katika ufisadi na ubadhilifu wa mali ya uma!
 
Naomba ufafanuzi juu ya hili jambo manake jina la chama mara nyingi kama si zote huwa ni kama kifupisho cha lengo na madhumuni yake. Sasa hiki chama cha mapinduzi kwetu MAPINDUZI maana yake nini sitaki kuamini kuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar ndio yanayozungumziwa hapo. Tell me Greatthinkers

Christian church movement! acha Nyerere apewe utakatifu tuu!
 
Wamepindua vilivyo vyema kuwa vibaya. Kutoka uadilifu hadi ufisadi.
 
Ukiingia kwenye anga zao kwa kuwapinga, wanakupidua, iwe kupindua uhai wako, ama kupindua maisha yako au wanapindua akili yako ili wabaki madarakani!
 
Ni mabingwa wa mapinduzi, mwaka 2010 walifanya mapinduzi kwa kuiba na kuchakachua kura za Dr Slaa na kumtangaza mkwere kuwa mshindi, kazi hiyo ilifanywa na TISS, NEC na JWTZ(kumbukeni kauli ya Gen. Shimbo kabla ya uchaguzi).Ila wajue kuwa mwosha huoshwa.
 
Kwa CC ya sasa ya CCM ni Msekwa peke yake anaweza kulijibu hili pengine na Kingunge kama bado analo angalau jino moja mdomoni!
Jamani humu hakuna hata mjukuu wa Kingunge au Msekwa awaulize hawa tupate jibu?
 
Jamani humu hakuna hata mjukuu wa Kingunge au Msekwa awaulize hawa tupate jibu?

Bado Bado sijapata jibu jamani pia napenda kuuliza swali la nyongeza ''Je Great Thinkers hamuoni kuwa huu ni umbumbumbu kujiita WANAMAPINDUZI pasina mapinduzi yeyote.
 
Chama hiki kikongwe cha siasa ambacho juzi kimejivua magamba, je ni mapinduzi gani kilicho yafanya hadi kikajiita chama cha mapinduzi?
Kama kilitokana na muungano wa Tanu na ASP kwanini hakikujiita chama cha Muungano?
 
Sio Chama Cha Mapinduzi ni Chama Cha Magamba, Chama cha Mapinduzi Nyerere aliishaondoka nacho
 
Mapinduzi yaliyofanyika ni kupindua umiliki wa chama kutoka kwa wakulima na wafanyakazi na kuwapa matajiri, wezi na mafisadi umiliki huo.
Kikwete aliwaambia wafanyakazi sizitaki kura zenu, je mwajiriwa anaweza kumkataa mwajiri wake?
 
"Tumeonewa kiasi cha kutosha,tumenyonywa kiasi cha kutosha,na tumepuuzwa kiasi cha kutosha.Unyonge wetu ndio uliotufanya tunyonwe,tuonewe na kupuuzwa.Sasa tunataka mapinduzi;Mapinduzi ya kuuondoa unyonge ili tusionewe tena na tusinyonywe tena."
Azimio la Arusha na siasa ya TANU ya Ujamaa na Kujitegemea-1967.
 
Mmeonewa na nani? Je mafisadi wataweza kuwanusuruni kutoka katika unyonyaji huo?
 
Tanzania inabidi tuchague

Chama Cha Mapinduzi: Je tunataka mapindizi kwa sasa?

Chama Cha Democrasia na Maendeleo: Je nchi yetu inahitaji Maendeleo pekee kwa sasa

Civi United Front: Je nchi inahitaji mseto kama wa CUF na CCM Zanzibar?

Haya ni mambo ambayo Watanzania wengi wanajiuliza kwa sasa je tunaenda wapi? Nchi yetu ingekuwa imegawanyika sana kama Sudan ningeshauri Mseto. Kama Nchi yetu ingekuwa imetawaliwa kiuchumi kama Zimbabwe ningechagua Mapinduzi lakini kwa sasa Tanzania inahitaji Maendeleo ya CHADEMA. Haya ni mawazo yangu wewe unafikiria nini?
 
Back
Top Bottom