Swala la waislamu kuchinja ni la kisheria au ni ustaaarabu tu?

Ni ustaraabu wa wakristu pamoja na madhehebu mengine ila naomba ndugu zangu waislam mpitie vizuri quran na muombe roho wa MUNGU awape uelewa ili mjue kwani ndani yake kuna watu walioanishwa wanaweza kuchinja na je hao watu mi wapi?ikiwa quran inaitambua biblia kwa nini nyie msitambue ukristo?au mpagani ndie anatumia biblia?

Watu wa kitabu wanaozungumziwa mule (ndani ya quran ) Si wakristo wa sasa mnaoamini agano jipya ... Watu wa kitabu wanaozungumziwa mule walikuwa hawali nyama ya ngurue na watu wa kitabu wanaozungumziwa mule walikuwa na ujirani mwema na waislam ... Kizazi cha watu wa kitabu kilipotea kitambo ... Issue hapa kama ulivyosema muislam kuchinja Si sheria ya Bali imekaa ki ujirani mwema zaidi na kobiashara ili nyama ipate kununuliwa na watu wote ...
 
Ni ustaraabu wa wakristu pamoja na madhehebu mengine ila naomba ndugu zangu waislam mpitie vizuri quran na muombe roho wa MUNGU awape uelewa ili mjue kwani ndani yake kuna watu walioanishwa wanaweza kuchinja na je hao watu mi wapi?ikiwa quran inaitambua biblia kwa nini nyie msitambue ukristo?au mpagani ndie anatumia biblia?
Katika Quran kuna vitabu 3 vinatajwa, Tourat ya Musa, Zaburi ya Daud, na Injil ya Issa (Yesu) na Mitume ndio waliopewa vitabu (sasa Yesu hapo ana kitabu). Katika hivyo hakuna Biblia, labda utusaidie kutujuza Biblia ni kitabu cha nabii gani ? Hao wenye hivyo vitabu vitatu tunavyovitambua (Tourat, Zabur na Injil) wakichinja sisi tunakula ! Lakini shurti hivyo vitabu viwepo na wavifate kwa ukamilifu. Mbali ya hilo la kuchinja, tumeruhusiwa kuwaoa pia ! Je hivyo vitabu vipo kwa ukamilifu wake ?
 
Unaenda kwingine mkuu, lets discuss issue ya sheria za uchinjaji wa wanyama. Haya ya dini peleka sehemu yake husika..
 
Mkristo hachinji bali anaua ! Nimekupa aya katika post ya tatu, Mwenyezi Mungu anasema tukichinja tutaje jina lake na tumshukuru ! Kumbuka wanyama ni umma kama sisi ! Kuna nidhamu nyingi ikiwemo kisu kuwa kikali. Wengine wanaua. Tofauti ya Washirikina na Wanaoamini iko wazi !

duh, wewe kweli una yako! kwa hiyo mkichinja nyie huyo mnyama anaendelea kuwa hai (hafi)!? uchinjaji mnyama ni jambo la kisayansi zaidi na kama ulivyosema kisu kiwe kikali, damu nyingi itoke kwa huyo mnyama na pia usimsababishie maumivu na yote haya lengo lake kuu ni kuwa nyama iwe bora na salama kwa mlaji. mengine ndiyo kama ulivyosema masuala ya IBADA ambayo haya yapo kiimani zaidi.
 
Nimejibu post ya mtu aliye dai kuwa Quran inasema: watu wa kitabu wakichanja tunatakiwa tule, which is true ! Sasa akadai Yeye ana Biblia na anataka kuchinjia Waislaam akijilinganisha na watu wa kitabu. Watu wakitabu wakati wakichinja walikua hawataji jina Yesu, walimtaja YAHWEH ! FUATILIA CONTEXT KABLA YA KULALAMA ! Umeona eeeh !
 
duh, wewe kweli una yako! kwa hiyo mkichinja nyie huyo mnyama anaendelea kuwa hai (hafi)!? uchinjaji mnyama ni jambo la kisayansi zaidi na kama ulivyosema kisu kiwe kikali, damu nyingi itoke kwa huyo mnyama na pia usimsababishie maumivu na yote haya lengo lake kuu ni kuwa nyama iwe bora na salama kwa mlaji. mengine ndiyo kama ulivyosema masuala ya IBADA ambayo haya yapo kiimani zaidi.
Nimesema ni jambo la IBADA na linaendana na NIDHAMU, Je hao wengi wana nidhamu gani katika kulitekeleza hilo ? Wanamtaja na kumshukuru nani wakati wanachinja ? So tofauti iko wazi !
 
Suala la waislamu kuchinja ni ustaarabu tu uliojengwa na watanzania, kumbuka serikali yetu haina dini kwa hiyo hakuna ulazima wa mwislamu kuchinja. Labda tu ieleweke kuwa kwa suala la biashara waislamu wachinje ili wenzao wa wawe na amani wanaponunua hiyo nyama

Kwa mfano wachinjaji wangekuwa wakristo. Sipati picha upande wa pili jinsi ambavyo wangekinukisha
 
Mimi ni mkristo. Nachukizwa sana na jinsi baadhi ya wachagiaji ambao wanaonekana dhahiri ni wakristo kwa kukosa ustaarabu. Ally kombo anachangia na anaelimisha vizuri sana kwa hoja tena bila jazba. Waislam wanaamini kuwa nyama halali ni ile iliyochinjwa na mwislam. Wewe mkristo chinja tu ule mwenyewe, usimpe mwislam maana utamkwaza. Uza nguruwe weka tahadhali ambao ni ustaraabu wa kwaida tu maana hata wafuga mbwa huweka tahadhali 'MBWA MKALI'. Mimi naomba nifahamishwe MWISLAMU NI YUPI? Sisi wakristo mfano ukikiuma baadhi ya makato ya mungu mfano uzinzi, say una kimada unakosa sifa ya kuuishi ukristo. Huwezi kushiriki sakramenti takatifu, huwezi kusimamia ndoa au ubatizo n.k. Je kwa waislamu mtu hata kama ni mchafu yaani mzinzi, mlevi, mwizi na kila aina ya uchafu, bado anasifa ya kuchinja? Kama la, basi mwislamu safi anayestahili kuchinja ni yupi?
 
Quran na vitabu vyote vya Hadithi hamna sehemu inayosema Muislamu pekee ndio anatakiwa achinje....Hilo wamejitungia tu...Mi nakula hata kama aliyechinja ni chizi.
 
Hayo yote ni maasiya, yaani ni matendo maovu. Bado hayakutowi katika uislaam ! Kubwa litakalo kutoa katika uislaam ni kuabudu asiyekua Mwenyezi Mungu ! (sanamu, miti, mizimu, alama, mnyama nk!) Binaadam wote wanazaliwa waislaam, wanatoka pale wanapobatizwa au kuanza kushiriki imani tofauti ! Vizuri akachinja mtu anaejua na mmemshuhudia anajiepusha na mambo mabaya
 
Quran na vitabu vyote vya Hadithi hamna sehemu inayosema Muislamu pekee ndio anatakiwa achinje....Hilo wamejitungia tu...Mi nakula hata kama aliyechinja ni chizi.
We kwakuwa una njaa, endelea kula ! Lakini ni wazi chizi hawezi kufanya nidhamu inayotakiwa katika zoezi zima ! Hata Quran imeruhusi katika kujiokoa usife njaa, ila baadae uombe toba !
 
ndo kaajila kao hako hawa mabwegeee
na wewe great thinker? kama huna point kuwa mtazamaji tu kama sisi, siyo lazima uchangie kwanza unaharibu thread na lugha ya taifa, kaajila ndo nini sasa.
ombi kwa mods; jaribuni kupitia michango ya baadhi ya watu ikibainika yupo kwa ajili ya kuharibu threads au anatoa points zisizo na mashiko mara kadhaa mnapiga permanent ban abaki kua mtazamaji tu. jukwaa linakosa mvuto kama zamani ambako wengi wetu tulipata shule ya maana kupitia jf.......
 
Mkristo hachinji bali anaua ! Nimekupa aya katika post ya tatu, Mwenyezi Mungu anasema tukichinja tutaje jina lake na tumshukuru ! Kumbuka wanyama ni umma kama sisi ! Kuna nidhamu nyingi ikiwemo kisu kuwa kikali. Wengine wanaua. Tofauti ya Washirikina na Wanaoamini iko wazi !

Tofauti kwamba kuna ushirikina ambao umeletwa na unawasumbua sana wale wanaoufuata na kuung'ang'ania bila hata kujua faida zake.
 
Ukristo ni ustaarabu na unatambua dini zingine zipo na kutambua jinsi ya kuishi nao bila kuwakwaza ili kuwapa nafasi kuitambua kweli.
Kuzingatia hilo haitaki kukwaza watu wanaodhani wakichinja wao ndio sahihi bali wengine wanaua.
Imewaachia waendelee na zozi hilo kistaarabu zaidi
 
Tukichinja sisi Waislaam kwa utaratibu tuliowekewa kwanza ni ibada na pili tunaonyesha shukrani kwa Mola wetu. Ukichinja wewe, chinja kwa raha zako na manufaa yako. Hatuhitaji ruhusa wala huruma ya mtu ! Ukichinja wewe hatuli kwa sababu hatujui umemtaja nani kuonyesha shukrani na utii !
 
Back
Top Bottom