Swahiliwood

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
7,140
14,678
Taasisi ya MFDI-Tanzania iliyo chini ya mtengeneza filamu maarufu
raia wa Marekani, John Riber, wamegundua tatizo lililopo kwenye tasnia ya filamu
na wanataka kuonesha mfano, kwanza kwa kutoa mafunzo kwa waandishi
wa script waliofuzu vigezo vyao na watayarishaji, tayari wameshachagua watu
sita waliofuzu majaribio yao na watakuwa na workshop ya kuwaweka sawa kabla
ya kuwawezesha ili kutengeneza filamu ambazo wanaamini zitakuwa bora na mfano.
MFDI-Tanzania ndiyo waliotoa filamu ya Chumo...

BOFYA HAPA
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
hawa watu 6 walipatikana kwa vigezo vipi na mchakato ulianza lini?

MFDI waliandaa workshop iliyoshirikisha watu 26 ambao walichaguliwa
miongoni mwa majina kibao waliyoyapata, waliangalia zaidi sifa za watu.
Miongoni mwa washiriki maarufu waliohudhuria warsha hiyo ni pamoja na
Jacob Steven (JB), Mahsen Awadhi (Cheni), Suzanne Lewis (Natasha),
George Tyson, Hamisi Kibari, John Lister, Ali Yakuti (ambaye hakumaliza mafunzo),
Ali Mbwana (Bashiri Mpemba), Chrissant Mhengga, Rashid Faraji na wengineo.
Workshop ilifanyika kwa wiki moja kuanzia tarehe 22 Novemba 2011;

washiriki walipatiwa mafunzo maalum katika:
1. Kupata habari za kina juu ya Mradi maalum wa Swahiliwood, na malengo ya mradi huo.
2. Kupata mafunzo ya jinsi ya kuandika kwa kina kuhusu Behavior-Change Communication.
3. Kupata ufahamu wa malengo ya Communication katika Mradi wa Swahiliwood.
Semina hii ilikuwa ya ushindani kwa washiriki na ya kwanza katika mfululizo wa
warsha za uandishi wa script. Siku ya mwisho wa warsha hii kila mshiriki alipewa
wiki moja ya kuandika dhana (concept paper) kwa ajili ya filamu yake. Kutokana
na mitazamo (mawazo) iliyowasilishwa, stori sita zilichaguliwa na kupitishwa katika
duru ya pili ambayo itaanza Jumatatu 30 Januari 2012 ili kuziendeleza kwenye
script, ambapo script tatu bora kati ya sita zitaendelea katika kipindi chote cha
warsha kumi zitakazokuwa zimebaki, ambazo zimelenga katika hatua zote muhimu
za uzalishaji; kuanzia maandalizi muhimu (pre-production), uzalishaji (production),
uhariri (post-production), na masoko (distribution)...
 
Ahsante mkuu Bishop, nmekusoma vizuri kwa kiasi changu!
Ila nina maswali kadhaa ambayo yananigusa,
hivi ni wapi ilikubaliwa duniani kuwa industry yoyote ya movie lazima "wood" kwenye utambulisho wake?? Hivyo, je ni kweli industry za nchi zote zina hyo "wood"??
Nmeangalia movie za Congo, SouthAfrika, Senegal, Kenya, Zimbabwe sijaona mchango wa kiambishi "wood" katika ubora wa kazi zao, ila ni vipaji na teamwork ya idara zote!
Afu wadau kwa nini mnang'ang'ana na watu walewale??
Mbona kwenye tasnia kuna watu wanavipaji vya hali ya juu na hamuwaangalii au kuhangaika nao? Sitataja jina kwa maana we ni unawajua watu wengi wenye vipaji vikali ila wamewekwa benchi hadi wameacha tasnia yenyewe,
nimekuwa karibu sana na hao mastaa wengi na nina diriki kusema hamna cha maana sana tutafanya kama tutaendelea kuhangaika na watu wenye upeo wa namna hiyo!
Naisubiri hyo project!
 
........................
Afu wadau kwa nini mnang'ang'ana na watu walewale??
.........................................
Naisubiri hyo project!

Mi nadhani tatizo ni mifumo ya masoko tuliyoizoea. Utaratibu wa filamu kupelekwa kwa "Wadosi" unachangia hili kwa kuwa hakuna mdosi ambaye yuko tayari kurisk kuchukua filamu ambayo mtu maarufu hayumo kwa hofu ya kupata mauzo mabovu. Kingine ni stori kuwa na miundo ile ile hivyo inaonekana bora aigize mtu maarufu mambo yaleyale kuliko mtu mgeni kuigiza yaleyale ikiwa na maana wanunuzi wananunua "nani kacheza" na "siyo nini na kwa namna gani kimechezwa"!! Kuna tatizo la msingi hapa!!
 
Mi nadhani tatizo ni mifumo ya masoko tuliyoizoea. Utaratibu wa filamu kupelekwa kwa "Wadosi" unachangia hili kwa kuwa hakuna mdosi ambaye yuko tayari kurisk kuchukua filamu ambayo mtu maarufu hayumo kwa hofu ya kupata mauzo mabovu. Kingine ni stori kuwa na miundo ile ile hivyo inaonekana bora aigize mtu maarufu mambo yaleyale kuliko mtu mgeni kuigiza yaleyale ikiwa na maana wanunuzi wananunua "nani kacheza" na "siyo nini na kwa namna gani kimechezwa"!! Kuna tatizo la msingi hapa!!

hapo ndipo ninaposhangaa. Ina maana ubora hauangaliwi kwenye hizi filamu? Kwa lugha nyingine hata kama filamu mbovu mradi kuna staa ndani basi! Pia hao mastaa walishushwa na ustaa wao? Uzuri wa mambo ya burudani ni kuwa mtu anakuwa staa kufumba na kufumbua. Tutawapiku tu hao wadosi soon
 
Industry ya movie kwetu hapa Tanzania inadorora kwa sababu ya kukosa watu ambao wako creative. Idea zao zimeanzia kwenye movie za kinaigeria na hivyo kupelekea kushindwa kutoa idea zao. Sasa hivi ukifuatilia wasanii wamekuwa madirector, wamekuwa maeditor wakati bado hata wao wenyewe hawajapata experience yoyote
 
Ahsante mkuu Bishop, nmekusoma vizuri kwa kiasi changu!
Ila nina maswali kadhaa ambayo yananigusa,
hivi ni wapi ilikubaliwa duniani kuwa industry yoyote ya movie lazima "wood" kwenye utambulisho wake?? Hivyo, je ni kweli industry za nchi zote zina hyo "wood"??
Nmeangalia movie za Congo, SouthAfrika, Senegal, Kenya, Zimbabwe sijaona mchango wa kiambishi "wood" katika ubora wa kazi zao, ila ni vipaji na teamwork ya idara zote!
Afu wadau kwa nini mnang'ang'ana na watu walewale??
Mbona kwenye tasnia kuna watu wanavipaji vya hali ya juu na hamuwaangalii au kuhangaika nao? Sitataja jina kwa maana we ni unawajua watu wengi wenye vipaji vikali ila wamewekwa benchi hadi wameacha tasnia yenyewe,
nimekuwa karibu sana na hao mastaa wengi na nina diriki kusema hamna cha maana sana tutafanya kama tutaendelea kuhangaika na watu wenye upeo wa namna hiyo!
Naisubiri hyo project!

Mkuu jouneGwalu,

Hata mimi nimekuwa napinga sana matumizi ya neno wood kwa kuwa hatuhitaji
hii miti ili kuifanya tasnia iendelee. Walio wengi wanadhani kuwa "wood" inawakilisha
tasnia ya filamu, wakati Hollywood ni eneo la kijiografia huko Marekani na halina
uhusiano wowote na tasnia ya filamu. Hata baadhi ya nchi ulizozitaja zipo kwenye
mkumbo huo, mfano Kenya (Riverwood), South Africa (Sandalwood). Nchi za Ulaya
zimekataa kuingia kwenye mkumbo huo kama zilivyo nchi za Francophone
(zilizotawaliwa na Ufaransa kama Congo, Senegal) ambazo hazitumii neno wood.

Kuhusu kutumia vijana wenye vipaji hili limedhihirika hata kwenye hii workshop
iliyoandaliwa na MFDI-Tanzania (Swahiliwood), wale wenye wenye majina makubwa
wamefeli, ba badala yake katika watu sita waliopita kuingia stage nyingine ni Bishop Hiluka,
Priscilla Mlay, Novatus Nago (Director wa CPU), Takura Maurayi (kijana wa ki-Zimbabwe
ambaye kwa sasa anaishi TZ), Chaiba Kombo na Timothy Conrady (Timamu Effects)…
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mi nadhani tatizo ni mifumo ya masoko tuliyoizoea. Utaratibu wa filamu kupelekwa kwa "Wadosi" unachangia hili...

Ni kweli 3D,

Kuna tatizo katika mfumo wa usambazaji. Wengi wa wasambazaji hufanya biashara ama
wakiwa Dar es Salaam au Mwanza, bila kupanua mtandao wa masoko yao sehemu nyingine
ndiyo maana Steps wamewapiga bao. Katika nchi zilizopiga hatua, filamu kwa kawaida huanza
na ‘box office' au kutolewa katika njia ya sinema, baadaye hutolewa kwenye video, kurushwa
kwenye vituo vya televisheni za kulipia, katika televisheni za umma, na hatimaye kwenye
vyombo vingine vya habari visaidizi (video games, katuni na kadhalika) na mwisho kutolewa
kama bidhaa rasmi (DVD, VHS) kwa matumizi ya nyumbani.

Nimekuwa nikiwashauri wasambazaji wa filamu kutafuta namna ya kupata mafunzo juu ya maarifa
yao kuhusu masoko. Masoko si kuuza tu bidhaa bali pia inahusu ushirikiano. Inahusu namna ya
kupanua mtandao wa mtu mmoja mmoja au kundi. Kama msambazaji ana duka Mwanza, na katika
miaka miwili, msambazaji huyo hajaweza kupanuka zaidi, basi ni bora akafanya mpango wa kutafuta
washirika wengine wa kibiashara au chombo/mashirika mengine kwa ajili ya usambazaji wa sinema zake.

Kuna vyombo/mashirika ambayo yamefanikiwa kuwa na mitandao karibu nchi nzima, wasambazaji/
wauzaji wa filamu wanaweza tu kushirikiana na mashirika hayo kwa ajili ya usambazaji wa sinema
katika maeneo mengi nchini. Hivyo kama mtandao wa usambazaji wa filamu wa msambazaji fulani
utakua na kupanuka zaidi, basi faida katika uwekezaji kwa waandaaji filamu pia itakuwa kubwa na
kuwafanya kuwa na pesa zaidi zitakazowawezesha kufanya utafiti, na watakuwa na uwezo wa kuwalipa
wasanii wao vizuri kuliko ilivyo hivi sasa.

Kwa sasa, asilimia ya watu wanaofaidika na uzalishaji wa filamu hapa nchini iko chini ya asilimia 5.
Watu wengine waliobaki katika tasnia hii hasa kwenye uzalishaji hawapati kabisa kile wanachostahili.
Hivyo, kama kutakuwepo soko pana zaidi kwa sinema, walio wengi wataweza kupata mishahara/
posho nzuri itakayowawezesha kuishi vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
hapo ndipo ninaposhangaa. Ina maana ubora hauangaliwi kwenye hizi filamu? Kwa lugha nyingine hata kama filamu mbovu mradi kuna staa ndani basi! Pia hao mastaa walishushwa na ustaa wao? Uzuri wa mambo ya burudani ni kuwa mtu anakuwa staa kufumba na kufumbua. Tutawapiku tu hao wadosi soon

Raia Fulani,
Unachokishangaa pia ni chanzo zha kudorora kwa tasnia yetu, ingawa wanadhani majina
ndiyo yanayouza. Kutokana na utafiti wangu, kuna vigezo muhimu viwili ambavyo vinaweza
kutuongoza katika dhana nzima ya mafanikio katika usambazaji filamu; (1) Maudhui/Mahitaji
ya Watazamaji (Content/Audience Connection) na (2) Jukwaa la Uwasilishaji (Media Delivery Platforms).

Maudhui/Mahitaji ya Watazamaji:
Kwa miaka kadhaa, sekta ya filamu Tanzania imeshuhudia utofauti mkubwa kati ya maudhui
katika hadithi zetu na kile watazamaji wanachokihitaji, na matokeo yake yameendelea kuyumbisha
mikakati ya soko na sera za usambazaji. Maudhui lazima yahusishwe moja kwa moja na mahitaji
ya watazamaji ili kuwe na nafasi ya mafanikio kwenye soko.

Maudhui yanayofaa katika kizazi cha leo ni yale yanayokwenda sambamba na watazamaji ndani
ya akili zao na kuihusisha jamii moja kwa moja. Mafanikio yanayotokana na maudhui yanategemea
sana mmenyuko wa watazamaji, na kujenga maudhui yaliyo kwenye mstari na mwelekeo wa
watazamaji na matarajio yao imekuwa vigumu, na sasa inahitajika kwa watayarishaji/ waandishi wa
script kujihusisha moja kwa moja na mtazamo wa watazamaji katika mazingira waliyomo. Kwa matokeo
haya, utafiti ni suala la kupewa umuhimu mkubwa kabla ya kuandaa kazi husika.

Kitu ambacho mtayarishaji/ mwandishi anapaswa kujua kuhusu watazamaji wake ni muhimu sana
kwa mafanikio katika biashara ya usambazaji. Kujenga maudhui bila uelewa mkubwa na ufafanuzi kwa
walengwa, ni kama kufunga safari ya kwenda mahali bila kufikiria jinsi ya kufika huko. Kama maudhui
yako hayakushikamana na aina ya maisha au matarajio ya watazamaji wako, jua umewapoteza.

Kundi la kwanza la watazamaji wa filamu ni la akina mama wa nyumbani, wafanyakazi wa ndani, na
vijana wasio na ajira. Kundi la pili ni la watazamaji linalotokana na matokeo ya moja kwa moja ya kituo
cha Africa Magic kuonesha filamu kwenye familia za watu wa tabaka la kati na la juu wenye uelewa
mpana kwa maana ya kwenda shule.

Na bila shaka kuna kundi la tatu linalotokana na watazamaji Watanzania walio nje ya nchi na Waafrika
(hasa wanaojua au kukipenda Kiswahili) katika bara la Afrika na maeneo waliko. Ni muhimu kuelewa
kwamba kila moja ya makundi haya ya watazamaji yana muundo na mawazo ambayo ni tofauti sana
na kundi jingine.

Katika utazamaji filamu hizi, kuna dhana ambayo huendana na mitazamo ya watazamaji (matamanio,
maadili, na mtazamo wa mtu binafsi kulingana na uzoefu wake katika kuangalia kazi mbalimbali) na vitu
hivi huathiri namna watazamaji wanavyohusiana na dunia inayowazunguka, ikiwa ni pamoja na maudhui.

Kama mtayarishaji wa filamu, suala la kwanza unatakiwa kuwajengea msingi watazamaji katika maudhui
uliyoyakusudia, ukielewa kwamba unaweza kuwa bosi kwenye kampuni yako ya production; LAKINI
UNACHOKIFANYA SI KWA AJILI YAKO! NI KWA AJILI YA WATAZAMAJI NA HADITHI ZAO!

Jukwaa la Uwasilishaji:
Watazamaji wanahitaji pia majukwaa ya habari kama wanavyojali kuangalia maudhui. Falsafa hii
ni muhimu wakati unaposhughulikia maudhui yanayowafaa watazamaji. Maudhui ya jukwaa la
uwasilishaji katika dunia ya kisasa ya filamu hayaishii tu kwenye kazi ya usambazaji, yanakwenda
ndani zaidi ya kile hasa soko la filamu lilivyo leo. Jukwaa litasaidia kuwasilisha mawazo kwa watu
katika njia itakayojumuisha mitazamo yao.

Mustakabali wa biashara ya usambazaji wa filamu na masoko Tanzania unatokana na watazamaji
vijana. Watoaji filamu wanatakiwa kuandaa kwa uangalifu demography hii ya watazamaji na
kukutana nao katika dunia yao. Dunia hiyo hustawi kwenye kundi la kweli la teknolojia ya digitali.

Katika hatua hii itakuwa vizuri pia kuuchunguza mfumo wa usambazaji ili kupata ufumbuzi wa
kutangaza na kusambaza (promotion and distribution solutions) ambao umesaidia kurekebisha
tasnia katika nchi nyingine, ili uigwe katika sekta ya filamu Tanzania. Film is a brand, kama zilivyo
brand nyingine, kuzitangaza na kuzisambaza ni vitu vyenye umuhimu sawa.

Ili tuweze kupiga hatua kwenye suala hili tunahitaji nguvu kubwa kuielimisha jamii faida za kutumia
mitandao ya jamii inayoweza kusaidia utoaji habari za filamu na kujenga jamii yenye wafuasi, na humo,
mijadala inaweza kujadilika, kipengele muhimu kabisa cha kuleta ufahamu au kampeni ya kujitangaza.
Jumuiya hizi ni maeneo ambayo watu wanaotembelea wanaweza kupata habari zaidi, kushiriki katika
mijadala, kujiunga na majarida, na kubadilishana ujuzi na mawazo na watu wengine, kwa lengo la
kupanua wigo mkubwa wa watazamaji.

Katika miaka michache iliyopita, mitandao imesaidia sana kufanya uwepo wa gharama nafuu katika
promotion and marketing kwa watengeneza filamu na hata kwa studio. Katika baadhi ya tasnia za
filamu za nchi zilizoendelea, ni nadra na kosa kubwa kutokuwa na tovuti ya kutangaza filamu kabla
haijaoneshwa kwenye majumba ya sinema.

Tunahitaji kuelekeza namna nzuri mitandao ya jamii inavyoweza kusaidia na kufanya kampeni yenye
kuleta mwamko wa namna ya kujitangaza kwa ajili ya watoaji filamu. Njia ya haraka na madhubuti ya
kujenga jamii ya watazamaji kupitia vyombo vya habari za mtandao ni kutengeneza dedicated website
ili kutoa makala, film clips, ku-downloads picha, miziki, soundtrack, wallpapers, na kadhalika.

Pia kuwapa mashabiki fursa ya kupata habari kuhusu maudhui/hadithi, wasifu wa waigizaji, na kuchangia
maoni yao na hata kuonesha interest zao katika filamu kwa jumla kutasaidia kuenea kwa taarifa au tetesi
za filamu. Mbali na kuwa na tovuti ya kujitolea, Kuweka filamu yako kwenye mitandao ya kijamii iliyopo ni
njia nyingine nzuri ya kuongeza jamii ya watazamaji/wafuatiliaji wa filamu.

Pia matamasha ya filamu husaidia kueneza taarifa miongoni mwa wakosoaji wa filamu na watazamaji,
na inaweza kuongeza umaarufu wa filamu na watazamaji kuwa wengi kama mapitio yake yatakuwa ya
kuvutia. Wakati sisi tukiendelea kukaa katika ulimwengu wetu wa 'uvivu wa fikra' sehemu nyingine ya
dunia inasonga mbele kwa kasi zaidi kuliko tunavyodhani.
 
Ndugu Bishop nimekusoma, na bila shaka nitaingia sokoni soon kuleta ushindani mpya.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Raia Fulani,
Unachokishangaa pia ni chanzo zha kudorora kwa tasnia yetu, ingawa wanadhani majina
ndiyo yanayouza. Kutokana na utafiti wangu, kuna vigezo muhimu viwili ambavyo ............................

Taratibu Bishop..ngoja niiprint kwanza post yako hii.
 
Bishop, nikupongeze sana kwa namna ya pekee sana unavyoweza kudemonstrate kuhusu industry katika namna inavyotakiwa kuwa, kutokea angle zote!
Wakati nakusoma hapo (japo mara kadhaa nmekusoma gazetini) nikawa najiuliza hivi ni kwa kiasi gani soko letu limezungukwa na watu wenye weledi na ujuzi wa namna yako!
Natamani ningekuwa natumia PC ili nipitie point kwa point katika kuijibu, ila umezungumzia Marketing na distribution system katika hali ya kweli sana ila steps wameegemea zaidi kwenye marketing, distribution wameisahau na wamekomalia zaidi Dar es salaam, nilikuwa Arusha hadi naondoka pale nlfanikiwa kumuona Agent mmoja tu, hlo ni tatizo sana hata tutakapo-takeover kutoka kwa hao wadosi tujue tunahitaji kuanza moja na mfumo wote.
Kuhusu "watazamaji" wetu ilo ni sahihi ila kuna movie (kazi) zinaweza kufanywa na kuyakusanya makundi yote hayo (japo kwa asilimia kubwa)...

Hebu wakati tunaendelea na mjadala, niambie!
Kuna kazi yoyote umefanya niitafute?
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Hebu wakati tunaendelea na mjadala, niambie!
Kuna kazi yoyote umefanya niitafute?

Kazi yangu mwenyewe sijawahi kufanya kwa kuwa kuna vikwazo
ambavyo vinanifanya nishindwe, ikiwemo kulazimishwa kutengeneza
filamu za part 1&2, kuwatumia wasanii ambao msambazaji anawataka
hata kama hawaendani na stori yangu na gharama nitakayotumia
katika filamu ambayo naamini itakidhi viwango hazitaweza kurudi
kutokana na kiasi ambacho hawa Wadosi wanalipa kwa producers.

Lakini nimewahi kushirikishwa kwenye kazi za wenzangu, ama kama
scriptwriter au consultant director. Ila mfano mzuri wa kazi nilizoshiriki
ni filamu ya Naomi Part 1 (2007) na Part 2 (2011), ambazo nilifanya
kazi kama director. Ni kazi nzuri sana kama ukizilinganisha na sinema
zingine za Kibongo, hasa kwa msuko wa stori na direction ingawa bado
Problem kubwa ni bajeti, zilikuwa kazi za bajeti ndogo mno kiasi unashindwa
kuweka mambo yote muhimu unayoyafikiria. However, kama soko
halitaboreshwa safari yetu itaendelea kuwa ndefu sana..
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kazi yangu mwenyewe sijawahi kufanya kwa kuwa kuna vikwazo
ambavyo vinanifanya nishindwe, ikiwemo kulazimishwa kutengeneza
filamu za part 1&2, kuwatumia wasanii ambao msambazaji anawataka
hata kama hawaendani na stori yangu ........................... Ila mfano mzuri wa kazi nilizoshiriki
ni filamu ya Naomi Part 1 (2007) na Part 2 (2011), ambazo nilifanya
kazi kama director. ..............................

Jana niliongea na vijana fulani ambao wana duka la kuuza DVDs za filamu. Niliwaambia kuhusu hasira yangu juu ya Part 1 na 2 (kwa maana ya DVD1 na DVD2) wakaniambia kuna filamu chache ammbazo huwa na DVD moja kama vile President ya Steven Mengele (Steve Nyerere). Wakasema wao wanadhani suala la DVD moja linawezekana ila ni lazima watazamaji wajue kabisa stori inaishia katika DVD hiyo moja na si kukatishwa.

Niliongea nao kuhusu kutotumia watu maarufu kwa sababu tu ya umaarufu wao, wakaniambia watu maarufu ndiyo huuza zaidi. Wakasema pia ikiwa mwandaaji ana nia ya kutotumia watu maarufu basi ni lazima filamu yake iwe nzuri kupindukia na aifanyie promo ya kutosha.

Sijaiona filamu ya Naomi, nitaitafuta japo katika clip moja niliyoona katika blog yako kuna msaniii Tabia (marehemu) nadhani ni Part 1 (2007). NIkifanikiwa nitakuja na comments zangu (niseme tu kuwa sitakuonea aibu au huruma kukurushia makombora kama kutakuwa na ulazima na sababu ya kufanya hivyo kwa sababu watu wenye ufahamu kama wako wanatakiwa kuutumia na si kuuacha uzamishwe na yeyote yule).

Suala la wadosi kukwamisha mambo linanifanya nifikirie kutafuta pesa na masoko yangu mwenyewe ya filamu nazofikiria kuandaa hapo baadaye (few years to come, may be two or less). Hata hivyo nitajaribu pia kuvuka boundaries za viwango vya filamu za sasa na wakati huo ili niweze kulazimisha dhana ya "fulani yumo" kufa. Ninafanya utafiti juu ya masoko pia. Siahidi mafanikio, naahidi majaribio.
 
Niliongea nao kuhusu kutotumia watu maarufu kwa sababu tu ya umaarufu wao, wakaniambia watu maarufu ndiyo huuza zaidi. Wakasema pia ikiwa mwandaaji ana nia ya kutotumia watu maarufu basi ni lazima filamu yake iwe nzuri kupindukia na aifanyie promo ya kutosha.

Sijaiona filamu ya Naomi, nitaitafuta japo katika clip moja niliyoona katika blog yako kuna msaniii Tabia (marehemu) nadhani ni Part 1 (2007). Nikifanikiwa nitakuja na comments zangu (niseme tu kuwa sitakuonea aibu au huruma kukurushia makombora...

Hahahahaaaaaaaa, ingekuwa kweli maarufu huuza kwa nini filamu zao
ndizo zinazofanyiwa promotion kubwa mno, kuanzia kwenye magazeti,
radio, televisheni, kwenye mabango makubwa ya barabarani hadi kwenye
magari ya matangazo!

Wabongo tumefungwa pazia ya ujinga machoni ili tusiuelewe ukweli, ingawa
Steps tayari wameshakubali kuwa filamu za hao maarufu zinawatia hasara
kubwa, kwa kuwa wanalipa pesa nyingi ambazo hazirudi kwa kuwa sasa hivi
hawana jipya na watu hawanunui tena... Anyway, siku moja tutafika...

Nampenda sana mtu anayesema ukweli hata kama unauma kwa kukosoa
pale penye makosa, lakini Watz walio wengi wamekuwa na tabia ya unafiki,
wanajifanya kukusifia unapokuwepo ingawa ukiwa haupo wanaponda, kwa
njia hii hawajengi bali wanabomoa...
 
  • Thanks
Reactions: 3D.

Similar Discussions

Back
Top Bottom