Swahiba mwingine wa Zitto ajitoa CHADEMA

Facts1,
Karibu sana ukumbini. Naona hapa utakuwa unamwaga facts tu. Safi sana!
 
Toni Kamkanda aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Dar es salaam miaka ya nyuma. Inashangaza habari hii kutolewa sasa. Katiba ya CHADEMA mpya ya mwaka 2006 haina tena cheo cha mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam. Kwa CHADEMA Dar es salaam ni kanda maalum, mikoa ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivyo, hakuna Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam wa vijana aliyehama chama. Wenyeviti wa mikoa yote hapa Dar es salaam wapo na wanaendelea na kazi zao kwenye chama kama kawaida. Hii habari inaandikwa leo wakati huyo Bwana alishahamia SAU miezi michache iliyopita tena alihama akiwa mwanachama wa kawaida. Kisa cha kuhama kwake ni kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2009 wa ndani ya chama aligombea nafasi zifuatazo na kushindwa Katibu wa chama Temeke, Mwenyekiti wa Vijana Temeke, Mjumbe Mkutano mkuu Temeke na zote akashindwa. Akaenda pia kugombea uenyekiti wa vijana Ilala napo akaanguka. Nipo alipohamia SAU ambapo taarifa zinaonyesha kwamba amepewa uenyekiti wa vijana Mkoa wa Dar es salam. Ni makapi tu yametoka, ametoka kapa.

Serayamajimbo

- I like this line, yaani sasa inaanza kuwa ni Chadema's classic Bwa! ha! ha! ha!

Respect.

FMEs!
 
watakaobaki ndio wana Chadema halisi. Nafikiri ndani ya Chadema hakuna uanachama wa kuzaliwa, uanachama hautegemei ulijiunga na umri gani miaka 10 au 60 wote ni wanachama, aliyejiunga mwaka 1995 na aliyejiunga leo wakati wa uchaguzi wote wana kura moja moja tu.

Sasa kama hakuna uanachama wa kuzaliwa iweje kuwe na wanachadema HALISI, WAKUJA na MAPANDIKIZI?

Haya matabaka ya uanachama mnayoyajenga na kuyaneemesha kwa minajili ya kuwahakikishia nafasi zenu na fikira zenu za kimikakati ndani ya chama yataendelea kuwagharimu....

omarilyas
 
Toni Kamkanda aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Dar es salaam miaka ya nyuma. Inashangaza habari hii kutolewa sasa. Katiba ya CHADEMA mpya ya mwaka 2006 haina tena cheo cha mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam. Kwa CHADEMA Dar es salaam ni kanda maalum, mikoa ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivyo, hakuna Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam wa vijana aliyehama chama. Wenyeviti wa mikoa yote hapa Dar es salaam wapo na wanaendelea na kazi zao kwenye chama kama kawaida. Hii habari inaandikwa leo wakati huyo Bwana alishahamia SAU miezi michache iliyopita tena alihama akiwa mwanachama wa kawaida. Kisa cha kuhama kwake ni kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2009 wa ndani ya chama aligombea nafasi zifuatazo na kushindwa Katibu wa chama Temeke, Mwenyekiti wa Vijana Temeke, Mjumbe Mkutano mkuu Temeke na zote akashindwa. Akaenda pia kugombea uenyekiti wa vijana Ilala napo akaanguka. Nipo alipohamia SAU ambapo taarifa zinaonyesha kwamba amepewa uenyekiti wa vijana Mkoa wa Dar es salam. Ni makapi tu yametoka, ametoka kapa.

Serayamajimbo
lol!:D:D
memba wewe ndo kwanza naku-mark leo

enewei,UMETULIA
 
mimi sishangai kabisa. Chama cha upinzani chenye msimamo ni CUF peke yake. CUF haiyumbishwi na vitimbakwiri. CUF ni chama chenye nguzo madhubuti kabisa. Matatizo ya CUF ni fedha tu. Pesa ndio imeadimika vinginevo ni chama chenye msimamo kwelikweli.
 
Code:
Swahiba mwingine wa Zitto ajitoa Chadema
broken-heart.jpg
Na Tumsifu Sanga
SWAHIBA mwingine wa Zitto Kabwe, ambaye naibu katibu mkuu wa Chadema, ametangaza kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga ma chama cha Sauti ya Umma (SAU).

Swahiba huyo, Toni Kamukanda anakuwa mtu wa tatu kujiengua kwenye chama hicho ambacho kinaonekana kuendelea kujijenga kisiasa, baada ya watendaji wawili wa ofisi ya makao makuu, David Kafulila na Danda Juju kujiengua baada ya kutimuliwa kazini.

Kamkanda anasadikiwa kuwa miongoni mwa wanachama waliokuwa wakiendesha kampeni kabambe kuhakikisha kuwa Zitto anatwaa nafasi ya uenyekiti wa Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita, kabla ya wazee kuingilia kati na kumshauri mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kumwachia mwenyekiti wake, Freeman Mbowe awe mgombea pekee.

Kamkanda, ambaye alikuwa mwenyekiti wa vijana mkoani Dar es salaam, alisema ameamua kuondoka ndani ya chama hicho kutokana na ubinafsi na ukabila uliokithiri kwa viongozi wa juu.

“Baada ya kubainika kuwa mimi Kafulila na Danda tuko katika mashambulizi ya kampeni ya kuhakikisha Zitto anakuwa mwenyekiti, ilianza mikakati ya kimya kimya kutufukuzisha uanachama lakini ilishindikana,” alisema Kamganda.

Kamganda aliongeza kuwa ndio maana kuna baadhi ya watu walifukuzwa uanachama kabla ya sisi kuchukua uamuzi wa kuondoka Chadema.

“Kama unakumbuka ndugu mwandishi kabla sisi hatujaondoka Chadema, kuna watu walivuliwa uanachama, ilikuwa tuvuliwe pamoja nao lakini kuna mtu wa karibu na Mbowe alimwambia hawa vijana waache wakae na baada ya hapo ikaanza fitina mpaka tulipoamua wenyewe kwa ridhaa yetu kuondoka,” alisema Kamganda.

Kamganda alisema uendeshaji wa chama hicho haufanyiki kwa misngi ya kiuongozi kutokana na maamuzi ya utendaji kufanywa na mtu mmoja hali ambayo inaashiria kuwa chama hicho kinaendeshwa kikabila na ubinafsi.

Chadema imekuwa ikitetereka tangu kipindi cha maandalizi ya uchaguzi mkuu baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombea uenyekiti na hivyo kusababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa viongozi. Lakini wazee na waasisi wa chama hicho waliingilia kati na kukinusuru chama.

Hata hivyo chaguzi za viongozi wa mikoa na jumuiya za Chadema zilikumbwa na matatizo mbalimbali yaliyoashiria kuwepo kwa makundi ambayo yalishaanza kukomaa ndani ya chama.

Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi, Kafulila, ambaye alikuwa ofisa habari wa Chadema, alitimuliwa kazini kwa madai ya kuvujisha siri za chama. Alitimuliwa sambamba na Danda, ambaye alikuwa akishughulikiwa masuala ya Bunge. Wawili hao walitimuliwa na mkuu wao kiutendaji, Dk Willibrod Slaa, ambaye anaongoza sekretarieti.
Code:

Code:
Hongera sana Kamganda ni haki yako kufanya na kuamua utakalo,

Ninachosikitika ni kuwa, huwa mnakaa humo halafu mnasema mabaya baada ya kutoka! hata kama kuna ukweli, still nyie inawaweka pabaya sana katika uaminifu, ina maana ungekuwa hakuna majungu ungeishi na hali hiyo ya ukabila na ubinafsi unayoisema?

Mwenzenu Zitto sijui anajimini nini, anawarushia makombora humohumo, ulitakiwa kusema ukiwa humo humo, uone moto wake ukoje, ukitoka utoke umeshasema ukiwa mwanachama.Huu woga wa kusema nje si mzuri sio kwa chadema tu hata kwa vyama vingine.

wakati unaona unawakomoa chadema, sisi wengine tunaangalia mustakabali wa upinzani kwa ujumla, watu wanadharau vyama hivi kwa sababu ya nyie mnaojitoatoa-UKIJITOA LAZIMA UJITANGAZE??,matokeo hawapigi kura na wanaopiga kura ni wana CCM wachache CCM wanaonekana wameshinda kwa kishindo , kumbe hamna lolote

Ukitaka kupima chadema utaona kesho Slaa au Mnyika anakimbilia kwenye media na kujibu tuhuma za Kamganda,utafikiri hawana kazi ya kufanya.

Jirekebisheni Chadema , angalieni mbele, sisi tuko nanyi.msipobadilika; sahau! it is certain you may rule this country in the next century! wakati mjukuu wa saba wa Mbowe anaongoza Chadema!!
Code:

Gazeti la Mwananchi siku hizi linanipa raha sana.......ni hatari sana ukigundulika unatumika kwa maslahi ya kundi fulani la waovu kwenye jamii.
 
Code:
Toni Kamkanda aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Dar es salaam miaka ya nyuma. Inashangaza habari hii kutolewa sasa. Katiba ya CHADEMA mpya ya mwaka 2006 haina tena cheo cha mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam. Kwa CHADEMA Dar es salaam ni kanda maalum, mikoa ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivyo, hakuna Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam wa vijana aliyehama chama. Wenyeviti wa mikoa yote hapa Dar es salaam wapo na wanaendelea na kazi zao kwenye chama kama kawaida. Hii habari inaandikwa leo wakati huyo Bwana alishahamia SAU miezi michache iliyopita tena alihama akiwa mwanachama wa kawaida. Kisa cha kuhama kwake ni kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2009 wa ndani ya chama aligombea nafasi zifuatazo na kushindwa Katibu wa chama Temeke, Mwenyekiti wa Vijana Temeke, Mjumbe Mkutano mkuu Temeke na zote akashindwa. Akaenda pia kugombea uenyekiti wa vijana Ilala napo akaanguka. Nipo alipohamia SAU ambapo taarifa zinaonyesha kwamba amepewa uenyekiti wa vijana Mkoa wa Dar es salam. Ni makapi tu yametoka, ametoka kapa.

Serayamajimbo
Code:

Mimi gazeti la Mwananchi nilishaacha kununua. Ni subsidiary newspaper la gazeti la Uhuru
 
Mwenzenu Zitto sijui anajimini nini, anawarushia makombora humohumo, ulitakiwa kusema ukiwa humo humo, uone moto wake ukoje, ukitoka utoke umeshasema ukiwa mwanachama.Huu woga wa kusema nje si mzuri sio kwa chadema tu hata kwa vyama vingine.

!!

Nilishasema kwamba utaonekana kituko kama ukiamua kutoka then kesho yake unaita waandishi unaanza kubwabwaja, kama we kidume kweli kwa nini usikomae humohumo?. sasa ukibwabwaja wale wanaokuchukua katika chama kipya ndiyo wakuonee huruma kwakupe cheo kingine? si lazima kwenye chama uwe na cheo.

Bila uvumilivu basi siasa kwa ujumla hamtaziweza, ipo mifano mingi tu ya wanasiasa wavumilivu na wasio wavumilivu na walio wavumilivu wana heshimika. Mwanasiasa unapohamahama unaonekana huna misimamo ni sawa na changu mawindoni, You need to stick to what you believe to be a successful politician".

Kwa upande mwingine CHADEMA safisheni chama chenu, toeni mainzi wote, wanaosema Chadema ni ya wachagga si wakomavu wa siasa hao ni wavamizi na mi nawaita mainzi.

Weberoya nakusoma Mkuu.
 
Sasa kama hakuna uanachama wa kuzaliwa iweje kuwe na wanachadema HALISI, WAKUJA na MAPANDIKIZI?

Haya matabaka ya uanachama mnayoyajenga na kuyaneemesha kwa minajili ya kuwahakikishia nafasi zenu na fikira zenu za kimikakati ndani ya chama yataendelea kuwagharimu....

omarilyas

Ndugu Omarilyas

Niliposema wana Chadema Halisi sikumaanisha matabaka ni uanachama kwa vitendo, kuna wanachama waliojiunga kwa malengo tofauti na ya chama, kama lengo lako ni kukivuruga chama wewe hautakuwa mwanachama HALISI ndiyo maana nikasema mwanachama wa aina hiyo akitaka kuondoka na aondoke.
 
yana mwisho haya yote...na tutajua mwisho wake baada ya uchaguzi 2010...na bado mengi sana yatakuja, kuanzia kuitana majina, watu kuhamahama, kutukanana, kashfa zisizo na ukweli, za ukweli maana-kuna watu wanajua mabomu ya wenzao wameyakalia wanasubiri wachukue fomu...sisi wananchi yetu macho na umaskini, as am sure hayo yote hayatatusaidia katika kutuletea maendeleo ya watanzania, maana badala watu tujadili maendeleo na sera za vyama tunaongelea sijui nani kajitoa wapi!
 
Back
Top Bottom