Suzan Mubarak atishia kuanika siri za Marekani hadharani!

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Suzan Mubarak atishia kuanika siri za Marekani hadharani!

2010-634277532062667362-266.jpg

Mke wa dikteta wa zamani wa Misri Hosni Mubarak amemwandikia barua Rais wa Marekani na kumtishia kuwa, iwapo Washington haitoingilia kati na kuzuia kuhamishiwa mumewe katika jela moja ya katikati mwa mji wa Cairo, atafichua siri za Washington kwa maafisa wa Misri.

Maafisa wa Misri wanataka kumuhamishia dikteta Hosni Mubarak katika jela hiyo ili kuzima hasira za wananchi baada ya kufahamika kwamba Suzan Mubarak, mwanaye Jamal Mubarak na maafisa wengine wa utawala wa zamani wa nchi hiyo walihusika katika tukio la uwanja wa mpira wa Port Saed ambapo makumi ya watu waliuawa katika ghasia zilizotokea baada ya mechi ya mpira wa miguu.
Uamuzi huo umepingwa vikali na mwenyewe Hosni Mubarak na familia yake ambapo inasemakana kuwa hata ametishia kuwa atajiua iwapo atahamishiwa katika jela hiyo ya mjini Cairo.

Wakati huo huo Kamati Kuu ya Uchaguzi ya Misri imetangaza kuwa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo utafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Juni mwaka huu.

Ahmad Shamsuddin mjumbe wa kamati hiyo amesema kwamba uchaguzi wa rais wa Misri utafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Juni na iwapo mshindi mutlaki hatopatikana basi duru ya pili ya uchaguzi huo itafanyika mwishoni mwa mwezi huo.
 
duh, mama amejitafutia ajali....watamkolimba tu. Alitakiwa azimwage tu hizo siri kama anazo. Amejinunulia kifo bila kulipia hata senti 50.
 
Kuna siri gani ya US isiyojulikana? mama anahaha tu kama Mwakyembe.
 
Mnadhani anajitafutia but labda amesha acha maagizo kwenye vyombo vya habari kwamba ikitokea chochote this is where you will find all the documents. Sio mjinga. Kama nyinyi na mimi tumefikiria kuna hatari lazima na yeye alifikiria, tena kabla yetu. She has a network of people around her, kumbukeni!
 
Maafisa wa Misri wanataka kumuhamishia dikteta Hosni Mubarak katika jela hiyo ili kuzima hasira za wananchi baada ya kufahamika kwamba Suzan Mubarak, mwanaye Jamal Mubarak na maafisa wengine wa utawala wa zamani wa nchi hiyo walihusika katika tukio la uwanja wa mpira wa Port Saed ambapo makumi ya watu waliuawa katika ghasia zilizotokea baada ya mechi ya mpira wa miguu.

mi hapo ni poamenishangaza kama ni kweli............................
 
walimtumia sasa ashakuwa kama .... Used asha expire wamemtupa. That is how US is. When they no longer need you au mambo yakienda vibaya they dump you.
Kweli dunia tambara bovu leo unaishi kama mfalme kesho waweza amka ukiwa huna kitu and the most wanted hunted by everyone.
 
Back
Top Bottom