Surprise kwa wanaume!!!

it's a creative surprise but don't forget to put in place contingency plans in case the unexpected happens (swali la kizushi: hivi kikaragosi chekundu kikizuka ghafla, bado kutakuwa na haja ya kulala hotel ya bei mbaya teh teh teh)
 
Habari zenu,
naombeni ushauri hasa kutoka kwa wanaume waliooa au walio kwenye mahusiano ya muda mrefu, pia wadada.
NB: NIKO SERIOUS TAFADHALI.

Ni hivi, nataka nimfanyie surprise mumewangu siku ya birthday yake mbali na kumnunulia zawadi siku ya birthday nitamfuata kumchukua kazini jioni (sio kawaida yangu) nitampeleka restaurant tukapate dinner for two a normal one hii huwa tunatoka mara kwa mara (not special prepared). Sasa nataka kubook hotel (not guest house) tukalale huko baada ya kupata dinner na kuamkia hapo next day which will be saturday tunapata break fast then nampeleka job coz yeye anaenda job saturday. Hii ya kulala hoteli hatujawahi tangu tulipotoka honeymoon. so hii ni out ya kwanza tangu tuoane. Kwangu mimi hili ni bonge la surprise ambalo nahisi litanitoa machozi ya furaha, ila nahitaji ushauri wenu wanaume hasa mliioa au walio katika mahusiano. Je mkeo au g/friend wako akikufanyia hv utafurahia au utashangaa au utafanyaje? naombeni msaada wa mawazo halisia iwapo ikitokea hv utarespond vipi kwa mkeo. TAFADHALI NIKO SERIOUS MATANI ACHA KWANI NINA MUDA MCHACHE WA KUFANYA HAYA.
Kwenye birthday yangu alinitoa out tukapata dinner baada ya kutoka job tulipofika home akanipa surprise gift.
Natanguliza shukrani kwa msaada wenu wa mawazo.

Je mna watoto? Hata mi wife alinifanyia hiyo kitu ila sikufurahi sana mpaka pale alipoletwa binti yangu wa miaka mitatu tukasherehekea nae. Iweje wewe ukashangilie birthday ya mumeo watoto wenu wapendwa muwaache Nyumbani? Kama hamna watoto basi imekaa poa.
 
hata sie tunawafanyia watoto wetu sana ila nimeona nasi tule maisha kidogo kukumbushia enzi na kuziba nyufa za mapenzi

Safi sana kwani mambo yote tunayofanya hapa duaniani lengo kuu ni kutafuta happiness na ndio maana mtu anajenga nyumba ya vigae wakati kuna mabati ya kawaida. vizuri kama na nyie mmeamua mle maisha maana hizi ela zinatakiwa zitutumikie sie na sio sie kuzitumikia
 
Kama ela itatosha mpitishe kwenye body massage ya ukweli hii itasaidia asije kataa kukupa kitu roho inataka kwa kusingizia uchovu wa kazi. Lol. Afu na hiyo hotel weka reservation usivamie tu ili wakupambie chumba kwa roses. Kusema honey moon vile. Hope you will all enjoy. Ikiwezekana tupe feedback jamaa alishangaaje.
 
2 my side,nitapokea kwa mikono na miguu yote miwili nitapofanyiwa chochote na mtu muhimu kiasi hiki.Namaanisha chochote,sina mipaka kwani mwenzako anapoamua kukufurahisha usiiharibu furaha yake.But nilichokua natarajia kutoka kwako ni kuwa unamjua mumeo kwa kuwa umeshamsoma,utakua unajua ni nini hasa hapendi na nini anafurahi.Maana unaweza ukampeleka maeneo ambayo yeye hapendi.Sisi wanaume tuna tofauti,ila wish u all the best!
 
Kama ela itatosha mpitishe kwenye body massage ya ukweli hii itasaidia asije kataa kukupa kitu roho inataka kwa kusingizia uchovu wa kazi. Lol. Afu na hiyo hotel weka reservation usivamie tu ili wakupambie chumba kwa roses. Kusema honey moon vile. Hope you will all enjoy. Ikiwezekana tupe feedback jamaa alishangaaje.

Una mambo wewe . . . . . . . . !
 
Mpeleke baharini asubuhi pale umesikia adhani ya asubuhi akapige cha wima wima, na nyie mmezama kwenye bahari hio itakuwa ndo nzuri.


Hio sijui ya kwenda naye hotelini imeisha pitwa na wakati.


lol! jamani hapo naona ntaambiwa mchawi, alfajiri baharini cha wima! mmmhhhh! asante lakini ni ushauri wako nautia kapuni

Lakini pia sio mbaya hongera sana kwa kumpenda mme wako :yo:[/QUOTE]
huo ushauri balaaa! baharini alfajiri kimoja cha wimawima lol! kama si kushikana uchawi ni nn hapo mmmh asante ntauweka ushauri wako kapuni.
 
Hivi haya mambo yameshahalalishwa eeh!..naona mnayatamka kama mchezo vile!!

yaani watu skuhiz wameharibika vbaya na wanaoyaleta haya kwenye ndoa ni wanaume, na mwanamke akizoea balaa mistaki kabisa hii laana lol!
 
mmmh!...........n nzuri lkn mumeo anapenda aina hiyo ya mitoko mfano kama hapendi ishu za kulala hotelini asije akakushangaza maidia.

asante my dia yeye anapenda sana mitoko na huwa tunatoka wote out ila hii ya kulala ndo itakuwa first time
 
Wasiwasi wangu, kwa mfano wakifika katika hiyo Hoteli, mhudumu anamwambia mzee, "Muheshimiwa, tumekuandalia kile kile chumba chako cha kawaida?"
Naamini suprise ingeishia hapo hapo.

:focus: Kwa mimi ningekushauri utafute Hoteli za ufukweni kwa mfano pale Double Tree by Hilton pangekufaa kwa usiku mmoja pia Coral Beach napo ni pazuri maana pia kuna mandhari nzuri ya kujivinjari.

heheee mmmh! hapo kwenye bold hapo ntazimia na surprise kweli itaishia hapo, thanx for hotel suggestions i'll put them on my list.
 
Kwa mimi nahisi ntaku-do like never before sijui kama hiyo kesho yake utaweza hata kunipeleka huko kazini,ila imekaa vizuri sana na kama ntakuwa na kinyongo changu nahisi siku hiyo kitaniisha ila ukitaka kunipatia zaidi there must be at least 2 Beers hii itakufanya usinisahau maisha yako yote(that is me,i say me) maana kama alivyo commnet hapo juu gfsonwin mwingine inaweza kuwa majuto kwa arrengemnet zako zote ulizoandaa.

asante kwa mawazo napata picha kama akifanya kama unavosema lol! i hope in +ve that he will take it and enjoy akinibadilikia mbona ntakuwa mdogo nahisi ndo utakuwa mwisho wa surprise lol! naisubiria hiyo siku, thanx man
 
Umeniwahi super thinker maana ningeshangaa kama kuna mtu ambaye hataliona hili,kiukweli wanaume tunapenda sana kuwa surprised,lakini kale katabia ketu ka wivu huwa kapo palepale hivyo jitahidi sana surprise hiyo isizidi uwezo wako yakaanza maswali ya umetoa wapi?Kumbuka kuwa wanaume hata kama anakukabidhi pesa kila siku, siku utakapompatia kitu cha gharama na kama hajazoea basi aslimia kubwa huanza kufikiria kuwa kuna kijana anamsaidia kazi wakati hakuna ukweli wowote.Labda tu kwa kuongeza surprise wakati unamchukua toka kazini mwambie kabisa kuw leo ninakushangaza na tafuta kitambaa cha kumfunga machoni ili asijue mnaelekea wapi na umfungue pale mtakapokuwa mmeshakaa na huduma ipo mbele yenu..Nakutakia kila la kheri katika kudumisha ndoa yako

asante sana nimepata kitu hapa i'm putting on my list thanx much
 
Kwangu mimi ni YES! YES! YES! Ila angalizo: wakati wa mahanjumati mweleze kuhusu nia yako ya kulala naye hoteli na umpe jukumu la kununua chumba. Pia kama hayupo hapa JF na hajui kuhusu discussion hii ni vema zaidi. Otherwise so far so good.

asante CORAL hapa nimenote kitu, that kumbrief about whats next while we r eating, yeah t ll b gud.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom