Surprise engagement party

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,605
6,071
Kuna rafiki yangu wa karibu anataka kumfanyia engagement surprise mchumba wake juzi alikuja kuniuliza if I have any idea how do it and make it unforgettable nikampa some ideas nikaona pia itakuwa sio vibaya nikiwashirikisha ma greti thinkazz pia kwa kuwa kuna watu wanaweza kuwa ideas ambao pia ni nzuri zaidi, mchango wenu ni muhimu nitaprint na kumpelekea ideas ambazo mtakuwa mmezitoa na kuzisuggest pia.
 
Hizo ulizompa ni zipi, ili tupate kuiongezea na kuavoid double-counting....!
 
Dah wengine hatuna eksipiriensi ya hizi pati mfululizooooo(engagement,kiitchen pati,bagi pati,sendiofu,reception ,kuvunja kamati,n.k.).tunajua moja tu ya kufunga ndoa kanisani.
Hebu tuwasubiri wataalamu akina asprin watuelezee...
 
duh... full copy n paste... ndo maana hatufiki...MAKE THINGS SIMPOO!!:confused2::confused2:
 
Kamuingage kanisani wakati wa kupeana mkono wa amani:welcome::welcome:
 
Suprise part hapo hela itateketea,,,kichen pati hela iliwe,,send off hela pia ichunwe,,,bado harusi na vunja kamati.

Hela yote iyo ungesave ungefungulia mradi si ungekua mbali mkuu?
 
Suprise part hapo hela itateketea,,,kichen pati hela iliwe,,send off hela pia ichunwe,,,bado harusi na vunja kamati.

Hela yote iyo ungesave ungefungulia mradi si ungekua mbali mkuu?

Mkulu sio mimi ni rafiki yangu ndio anataka kufanya hii kitu
 
MPE KISAGO CHA MBWA MWIZI AFU AKIWA HOSPITALINI... SHUKA NA BUNDA LA MAUA NA PETE ....OMBA RIDHA KWA HISANI YA WATU WA....!!!:becky:
 
MPE KISAGO CHA MBWA MWIZI AFU AKIWA HOSPITALINI... SHUKA NA BUNDA LA MAUA NA PETE ....OMBA RIDHA KWA HISANI YA WATU WA....!!!:becky:
Nimecheka sana sana sana,kisago tu chenyewe tayari itakuwa ni suprise so ukija baadae na maua plus pete itakuwa suprise ya pili.Lkn vp ukadhani unatoa kisago halafu ukapewa wewe?
 
MPE KISAGO CHA MBWA MWIZI AFU AKIWA HOSPITALINI... SHUKA NA BUNDA LA MAUA NA PETE ....OMBA RIDHA KWA HISANI YA WATU WA....!!!:becky:

Kiongozi unatokea kure Tarime? Imenibidi nicheke tu muraaaaaaaaaa weitu
 
Vijana vipi? Ubunifu hakuna tena siku hizi?

Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa mke wangu, ilikuwa hivi . . .

Nilimwalika yeye pamoja na marafiki zake na pia rafiki zangu wa karibu jumla tulikuwa kama 30. Wote walijua ni Birthday ya Mke wangu na walikuwa wanajumuika nasi tu. Tuliifanyia katika hoteli moja ya kitalii katikati ya jiji.

Baada ya kupata dinner ambayo ilikuwa ni buffet ya vyakula vya Kitanzania, hatimaye nilimwalika mke wangu kukata keki. Alipokuwa anakata keki, mara kisu kikawa kigumu, nikamwambia labda kuna kitu ajaribu kutoa. Alipotoa kulikuwa na kibox kidogo chenye saa ndogo nzuri ya kike ya dhahabu, alifurahi saana na kila moja alifurahi nasi.

Baada ya shamrashamra hizo, nilimwomba amalizie kukata keki, safari hii tena kisu kikakwama. Alipotoa kitu kigumu safari hii kulikuwa na kibox kidogo ambacho kimefungwa vema. alikitioa na kufungua ndani yake kulikuwa nana pete ya uchumba yenye vito vya Tanzanite na Diamond. Ni wazi kabisa alipigwa na mshangao huku machozi ya furaha yakimtoka . . . .

Kabla hajataharuki, kidume tayari nilikuwa nimeshachukua pete huku nikilalama "Will You Marry Me?" . . . . hakika kulikuwa na msisimko wa ajabu. Hakujivunga aliposema "YES MY BABY", mara nikamvisha ile pete. Baada ya hapo, tukaenda kufungua mziki huku ndugu, jamaa, marafiki na wapambe wetu wakituunga mkono . . .

Sister wangu moja aliniambia kuwa wakati BF wake anamvisha pete, walikuwa wawili canteen wanakunywa soda, kumbe kidume bwana shem, kaweka pete ndani ya glass kisha akamimina coca cola. Sister alipokuwa anamaliza kunywa soda akaona ile pete, kabla hajauliza, jamaa akamwomba "PLEASE MARRY ME"
 
Back
Top Bottom