Sura mbili za karume

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
HIZI PICHA MBILI ZINATOA SURA HALISI YA UNAFIKI NDANI YA UONGOZI WA SERIKALI NA CHAMA TAWALA. KARUME HAPA HAYUPO LAKINI PALE YUPO...WHY?? KWA NINI??


8D6U9870.JPG

Kikao Cha Baraza La Mawaziri (BLM),Desemba 10, 2009 Karume (Rais wa SMZ) ambaye ni Mjumbe wa BLM kwa mujibu wa Ibara ya 54(1) ya Katiba ya URT hayupo hapa

2.jpg




Kikao Cha Kamati Kuu Ikulu Machi 28, 2010 (Karume na Viongozi wengine wa Juu wa SMZ wpo hapa japo si kwa rangi ya Kijani kama ilivyo kwa Rais Mstaafu Mkapa).


MTAZAMO:
<O:p> </O:p>
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ndio inatoa muundo wa Serikali yetu na kutambua uwepo wa vyama vya Siasa vinavyoweza kuunda Serikali. <O:p></O:p>
<O:p> </O:p>
Ibara ya 47(1) inatamka kuwa kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla ikiwemo kumsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano. <O:p></O:p>
<O:p> </O:p>
(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.<O:p></O:p>
<O:p> </O:p>
Ibara ya 54(1) inatamka kuwa kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe<O:p></O:p>
wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.<O:p></O:p>
<O:p> </O:p>
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye atkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza Mikutano hiyo.<O:p></O:p>
<O:p> </O:p>
(3) Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.<O:p></O:p>
<O:p> </O:p>
Note: <O:p></O:p>
<O:p> </O:p>
I: Katika Muundo wa uongozi wa Chama, Rais wa SMZ ni Makamu wa Mwenyekiti wa Chama kwa hadhi sawa na Msekwa (mtu wa kawaida tu katika uongozi wa Serikali. Rais wa SMZ hawezi kuongoza BLM kama ilivyo kwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.<O:p></O:p>
<O:p> </O:p>
<O:p> </O:p>
II: Katika Muundo wa Uongozi wa Chama cha Mapinduzi ambacho kinaongoza Serikali, nafasi ya Makamu wa Rais ambaye ndie Makamu wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ni kama haitambuliki kabisa!. <O:p></O:p>
 
Sasa kama yote unayajua, tatizo likowapi? Jamaa alitoka kidogo kaktika iyo picha alienda short call
 
Sawa, nafikiri chama si serikali, hata kama chama ndio kinaongoza serikali.
 
Back
Top Bottom