Suprise nyingine kazi kweli kweli

Jana nilipomsabahi rafiki na ambaye pia ni jirani yangu pindi nimetoka kazini, nilimwona yupo na mawazo sana. Nakwamwacha, nikaingia ndani kwangu kisha mda siyo mrefu nikaenda kumsalimu na hasa kufahamu whats wrong on his side kwa sababu sivyo alivyo. Jamaa akanichana kwamba leo mchana alienda kufanya shopping ya waototo wake wawili, lahaulaa akakutana na mke wake face to face Kariakoo akifanya shopping huku akiwa na shosti wake. Mke wake bila hiyana akamwambia mmewe Surprise.

Tatizo juzi usiku aliongea na mke wake ambaye anafanya kazi wilaya moja ipo songea. Mke wake akamwambia mme wake yupo kijijini sana (Songea), kuna baridi sana, anatamani wawe wote na mengine mengi

Mke wake amepata kazi miezi kama sita hivi imepita kituo cha kazi huko songea, mume kabaki na familia hapa Dar. Je suprisee hizi kwa wanandoa zimekaaje?
Mambo ya Guest House hayo... Mkoa anaotoka=Dar es salaam, mkoa anaokwenda Dar es salaam.
Kwikwikwikwikwikwikwikwikwi....
 
Tusiwe na haraka jamani, kwani alikutana nao saa ngapi? Labda ndio alikuwa anaingia na gari ya Songea?


Ila mmh.....

Kama huyu mwanamke jana yake usiku walilonga "akiwa songea",kwa vyovyote safari angeianza asubuhi ya siku iliyofuata,na kwa vyovyote wasingekutana mchana Kariakoo ,maana ma-bus hata gari private toka Songea hadi Dar hufika jioni.Labda amwonyeshe ticket ya ndege,vinginevyo atakuwa ametumia technolojia ya jizani"Ungo".La sivyo,jamaa mali zake zinaliwa.
 
Back
Top Bottom