Super Market na Sukari

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Wakuu siju kama hii imeshawakuta, jana baada ya kutoka kazini kwangu nilipitia super market moja maeneo ya hapa jengo la ccm mkoa hapa Arusha majira ya saa 1 usiku katika kutaka kununua mahitaji yangu nikaona wacha ninunue na sukari angalau kilo tano,

chakushangaza nikaambiwa nikinunua sukari kilo moja inanibidi ninunue na kitu kinginge cha shilingi 1500 kwahiyo namaanisha kilo moja ya sukari inauzwa 1800, itanibidi ninunue na hitaji lisilozidi au na kuendelea shilingi 1500 na ni kilo moja tu ndio nitapewa, mimi nikasema sasa nataka kununua kilo tano akatoka jamaa mwenye duka nakuniambia aisee kama ni hivyo itanibidi ninunue vitu visivyopungua 30000, nikauliza kulikoni wakasema ni amri yakutoka kwa balozi! Basi nikaghairi na kwenda zangu mtaani.

Nilipofika mtaani nikasimama kwenye duka lililo jirani na nyumbani nikaona sukari pale ipo na bei ya kilo moja bei ni kama ileile niliyoikuta pale super market, nikamuuliza mwenye duka naweza pata kilo tano? jamaa akasema kama unahela kwanini nisikuuzie? basi nikanunua kilo zangu tano kwa bei ileile na kuishia zangu mtaani.Basi haya ndio mambo mseto toka hapa Arusha sijui kama hii kwenu wenzangu ilishawakuta.
 
mkuu,jengo la ccm super market ipi? ya kwanza au ya pili,ile ya kwanza kwanza wanauza vitu vyao expensive sana compare na hiyo nyingine
 
Ndalo nikweli kabisa ndiyo kinachofanyika kwenye supermarket hiyo nilishawahi kwenda hapo wakaniwekea mashariti hayo niliondoka nikaenda kununua dukani kwa 2000 kwa kilo halafu jamaa wana nyodo kishenzi niliapa kutokukanyaga supermarket hiyo..
 
Back
Top Bottom