Kibirizi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 604
- 146
Gari ya abiria Summry ambayo ilikuwa inatoka Kigoma kwenda Dar leo imepata ajali mbaya maeneo ya Kifura karibu na makao makuu ya Wilaya ya Kibondo, bus hilo limegongana uso kwa uso na gari aina ya Scania huku likiwa na tela ambalo limesheheni mzigo wa cement, majeruhi waliwahishwa hospitali ya wilaya ya Kibondo wakati majeruhi kama wanne wakiwa hoi sana, dereva alipona ingawa naye majeruhi, lakini baadaye askari polisi walionekana wakihaha kumsaka dereva kwa kukagua kila gari inayopita.