Sumaye ndani ya Uingereza!

Status
Not open for further replies.
In short mkuu fanya research of what a current & retired government official is entitled to by law. Ukisha fanya your research njoo utuambie ni nini kafanyiwa au kafanya kinyume na sheria.
1.Ubalozi wowote wa Tanzania upo kuhudumia wananchi wake. Yeye kama kiongozi mstaafu alistahili kupewa gari la kutumia. Mbona hata nyumbani viongozi wetu wastaafu wanapewa misafara na ulinzi? That is something Sumaye will have for life.

2.Kila mtu ana imani yake na ana haki ya kui hubiri. Kwani mzee Mwinyi akitoka nje ya Tanzania aka amua kuhubiria Uislamu ata katazwa? Hiyo ya kuhubiri dini siyo neno as long as haja vunja sheria.

3.Huko unako dai kuzurura we ulitaka afanyeje muda wote? Hata ingekua wewe ungekaa hospitali 24/7. Tuwe na ubinadamu kidogo. Hata ingekua wewe unge tembea tembea. Kaenda kwenye check-up which means siyo lazima kuwa anaumwa bali ni kuangaliwa. Hata angekua anaumwa kama mtu ana sikia unafuu kwa nini asi tembee.

4.Utam linganishaje mbunge na waziri mkuu mstaafu? Mwakyembe ni mbunge which means ana privilege chache zaidi ya waziri mkuu/waziri mkuu mstaafu. Hata kimahesabu it makes sense, wabunge ni wengi kuliko mawaziri wakuu wastaafu kwa hiyo gharamu za kuwapa wabunge fulani ukiamua kuwapa wote ni kubwa kuliko kuwapa mawaziri wakuu wastaafu.

5.Kama nilivyo sema awali kuna privileges mtu anapewa kutokana na cheo alicho nacho au alicho kua nacho. Mafao haya lingani kwa kila mtu. Useme labda mafao ni makubwa kwa viongozi basi yapunguzwe kwa kurekebisha sheria iliyopo ila ukumbuke aliye juu aki punguziwa basi na aliye chini nae ata punguziwa. This would mean watu uta wabania pension zao na tayari ni hovyo as it is. I suggest you do your research well ukija jamvini unatupa something not just concrete but logical also. Siyo kulalamika tu just because mtu alikua kiongozi basi ukadhani kila utakacho msema watu wataku support.
 
Last edited:
Waziri mkuu mstaafu bwana sumaye alikwenda uingereza kwa ajili ya matibabu(medical check up).

Lakini badala ya kuwa hospitalini amekuwa akizurura kwenye miji ya uingereza kuhubiri dini,kama mgonjwa aliyetakiwa kupata matibabu nje ya nchi asingekuwa na nguvu ya kuzurura kwenye miji mbalimbali badala ya kuwa hospitali au kama ugonjwa wake haukuwa mkubwa kwanini atumie pesa za kodi kwenda nje? Wakati mwakyembe anapata huduma muhimbili?

,habari yake iko kwenye tanzania daima kwenye habari kuu maoni au kwenye picha za mtandao wa tzuk,com kwenye picha utamuona mheshimiwa sumaye akiwa kwenye ibada.

Hakatazwi kufanya ibada ila iwe kwa pesa zake sio kodi za wananchi.

acha hizo wewe....medical check up ..mtu huwa halazwi...anakaa hotelini na kwenda kufanya vipimo...that is called routine medical check up...ni haki stahili kwa kiongozi kuanzia ..jaji mkuu ,mkuu wa majeshi....mawaziri wakuu ,,rais etc.....

wabunge hawana haki hizo...., na waziri pia hawana ...zaidi ya kuhudumiwa wakiwa ofisini wakisha staafu basi!

afteral kusali muhimu....!!...
 
Hata mimi nisingeona tatizo isingekuwa wakina mama zaidi ya 13,000 (9/11 zaidi ya nne) wanakufa kila mwaka kwa kukosa huduma bora wakati wa kujifungua! Hawa ndiyo waliotufikisha hapa, basi angalau wangeonyesha empathy kwa wenzao. Hatuombi makuu. Wakunga na vifaa vya kutoa huduma wakati wa kujifungua katika kila zahanati. Wakati tukisubiri hilo, basi hizo check-up wafanyie kwenye hospitali za nchini kwetu sote.

Amandla......

Fund Mchundo:

Entitlement aliyokuwanayo ya kufanyiwa medical check-ups anatakiwa awe nayo mtanzania yoyote yule.

Na hiyo entitlement haijasema mtu aende UK tu. Angeweza kwenda Urusi, SA, KCMC au Cuba.

Labda liwepo shirika la bima la watu VIP, afu hilo shirika lichukue mzigo wa kuwalipia matibabu.
 
Kwa nini tusiboreshe huduma zetu au kukawa na hosp. moja maalumu Tz kwa kucheki afya za vingozi?

Hospitali kubwa kama KCMC unawapa uwezo wa vifaa na madaktari na ikibidi hata unaleta na madaktari toka nje!

The same applies kwa shule za serikali

Hivi lini huduma zitakaa ziboreke wakati viongozi hawatibiwi huko?

Au nje ni kujustfy ulaji wa pesa?

Mkuu, bado watafanya safari za Nje tu kwa imani ya kuhifadhi siri za magonjwa/afya zao....bwana nani 'KUPIMA' bado ni msamiati mzito sana kwa sisi Wa-Tanzania....we-umesahau ktk ile kampeni ya hiari ya kupima 'nanihiii' kuna viongozi walikuwa mstari wa mbele kabisa lakini majibu ya vipimo hivyo walitokanayo nyumbani??
 
In short mkuu fanya research of what a current & retired government official is entitled to by law. Ukisha fanya your research njoo utuambie ni nini kafanyiwa au kafanya kinyume na sheria.
1.Ubalozi wowote wa Tanzania upo kuhudumia wananchi wake. Yeye kama kiongozi mstaafu alistahili kupewa gari la kutumia. Mbona hata nyumbani viongozi wetu wastaafu wanapewa misafara na ulinzi? That is something Sumaye will have for life.

2.Kila mtu ana imani yake na ana haki ya kui hubiri. Kwani mzee Mwinyi akitoka nje ya Tanzania aka amua kuhubiria Uislamu ata katazwa? Hiyo ya kuhubiri dini siyo neno as long as haja vunja sheria.

3.Huko unako dai kuzurura we ulitaka afanyeje muda wote? Hata ingekua wewe ungekaa hospitali 24/7. Tuwe na ubinadamu kidogo. Hata ingekua wewe unge tembea tembea. Kaenda kwenye check-up which means siyo lazima kuwa anaumwa bali ni kuangaliwa. Hata angekua anaumwa kama mtu ana sikia unafuu kwa nini asi tembee.

4.Utam linganishaje mbunge na waziri mkuu mstaafu? Mwakyembe ni mbunge which means ana privilege chache zaidi ya waziri mkuu/waziri mkuu mstaafu. Hata kimahesabu it makes sense, wabunge ni wengi kuliko mawaziri wakuu wastaafu kwa hiyo gharamu za kuwapa wabunge fulani ukiamua kuwapa wote ni kubwa kuliko kuwapa mawaziri wakuu wastaafu.

5.Kama nilivyo sema awali kuna privileges mtu anapewa kutokana na cheo alicho nacho au alicho kua nacho. Mafao haya lingani kwa kila mtu. Useme labda mafao ni makubwa kwa viongozi basi yapunguzwe kwa kurekebisha sheria iliyopo ila ukumbuke aliye juu aki punguziwa basi na aliye chini nae ata punguziwa. This would mean watu uta wabania pension zao na tayari ni hovyo as it is. I suggest you do your research well ukija jamvini unatupa something not just concrete but logical also. Siyo kulalamika tu just because mtu alikua kiongozi mstaafu basi ukadhani kila utakacho msema watu wataku support.

mwambie...majungu kama haya ndio sehemu ya majungu ya uwongo waliokuwa wakipikwa salim ,malecela na sumaye ..kwa ajili ya urais.....sasa mnajuwa ,alecela na salim umri umeenda......mnaanza kumpachika sumaye madongo ...mnaogopa anachukua fomu 2010.....afteral sio siri kuwa SUMAYE could have perfomed better as a president kuliko huyu ze comedy..,jkwalker..

leave sumaye along !!
 
anayechezea pesa zetu za kodi ...na aliyemaliza akiba yote ya Taifa aliyoikuta ni jk ....kwa safari safari.....waacheni wastaafu!!
 
acha hizo wewe....medical check up ..mtu huwa halazwi...anakaa hotelini na kwenda kufanya vipimo...that is called routine medical check up...ni haki stahili kwa kiongozi kuanzia ..jaji mkuu ,mkuu wa majeshi....mawaziri wakuu ,,rais etc.....

wabunge hawana haki hizo...., na waziri pia hawana ...zaidi ya kuhudumiwa wakiwa ofisini wakisha staafu basi!

afteral kusali muhimu....!!...

Medical check ups ni haki ya kila mtu. Tusidanganyane hapa. Kinachotofautiana ni nani anayelipa bills za medical check ups. Na vilevile kufanyiwa medical check ups sio lazima ukae hotelini. Unaweza kukaa nyumbani na kwenda hospitali kufanyiwa check -ups zako.
 
Mambo mengine sio ili mradi tu unataka kusema. Hili sio jambo jipya na wala sio la kuumiza kichwa. Kama inaonekana shida basi suala sio Sumaye kujinyima asiende medical chekup wingereza, suala ni kubadilisha incentives za viongozi. Wewe ungekuwa sumaye ungefanya nini?
 
Mkuu mbona umekuwa mkali umeguswa nini?

hapaana sipendi unafiki....,inajulikana wazi kuwa matibabu kwa viongozi wastaafu yameainishwa kwenye sheria ....na yanasimamiwa na ofisi ya rais [utumishi]...why should we singled out names.........

tusijidanganye kuwa matibabu nje ni haki ya kila mtu.....sisi watanzania wa kawaida hadi tukaunge foleni pale wizara ya afya[ukifika unaambiwa kuna wenzako 500 mbeele yako wanasubiri kwenda ...]..,ila kwa wastaafu imeanishwa kabisa check up once a year,na kwenda matembezi if am not mistaken twice a year[total safari zinazolipiwa na serikali kwa mwaka ni tatu-fuull budgeted and paid]....kama hatutaki tubadili sheria ...ya mafao ya viongozi!!!

its true kuwa jk anafuja pesa kuliko kuingiza ndio maana amemaliza akiba yote ya nchi!...
 
Sumayes20Benjamin20Maira20Owino.jpg

GadoMrs_20and20Mr_20Sumaye20Owino20.jpg

Lulu.jpg
 
mwambie...majungu kama haya ndio sehemu ya majungu ya uwongo waliokuwa wakipikwa salim ,malecela na sumaye ..kwa ajili ya urais.....sasa mnajuwa ,alecela na salim umri umeenda......mnaanza kumpachika sumaye madongo ...mnaogopa anachukua fomu 2010.....afteral sio siri kuwa SUMAYE could have perfomed better as a president kuliko huyu ze comedy..,jkwalker..

leave sumaye along !!

Hiyo nyekundu hapo juu kwa sehemu nakubaliana na wewe kutokana na hali halisi tunayoiona ikiendelea hapa TZ, maana wizi wa mali za umma umekidhiri na safari za mheshimiwa zisizoisha. Mojawapo wa wapambe wa Sumaye alikuwa Magufuli na ilikuwa kuwa Magufuli aje kuwa PM kama Sumaye angekuwa rais. Sasa angalia utendaji wa Magufuli akiwa ametupwa kwenye wizara iliyodhanikwa kuwa haina maana yoyote. Je angekuwa PM ingekuwaje?
 
Mbona yuko health tu......alafu kwenye lile zoezi la kupima UKIMWI mbona alikula kona?

1.Mtu kuonekana ana afya haimaanishi ana afya. Unataka kuniambia unaweza kumtambua kila anayeumwa kitu kwa kumuangalia? Sasa haya mambo yakusema mtu anaonekana mzima ni ushamba.

2.Kaenda kwenye check-up. Check-up mtu unakwenda kuangaliwa afya na kubaini tatizo lolote linalo weza kutibika kabla haijaanza kuonyesha dalili za wazi.

3.Kuna anaye lazimishwa kupima UKIMWI? Kupima ni hiari wewe kama wewe kapime ujue afya yako hiyo ya wengine waachie wenyewe.
 
Huu ni unafiki, Sumaye si mtu bali Michuzi ndio mtu, Sumaye ndio anatumia pesa za walipa kodi Michuzi hatumii sio.

Acheni double standards
.
 
Hivi medical check up inajumuisha nini? Yaani hiyo check up haiwezi kufanyika Tanzania? Na kama haiwezi kufanyika Tanzania, tatizo ni nini - wataalamu(sijui hata unahitaji utaalamu gani) au vifaa au vyote viwili? Just curious..it doesn't hurt anything to ask.
 
Jamani kweli wa TZ tutaliwa mpaka tone la damu ya mwisho SUMAYE NI MMOJA WA MAFISADI WAKUBWA enzi ya MKAPA, lakini ndo hivyo anatanua kwa kodi yetu ma hela ya UFISADI kafika kwa kuinvest anakojua
 
hapaana sipendi unafiki....,inajulikana wazi kuwa matibabu kwa viongozi wastaafu yameainishwa kwenye sheria ....na yanasimamiwa na ofisi ya rais [utumishi]...why should we singled out names.........

tusijidanganye kuwa matibabu nje ni haki ya kila mtu.....sisi watanzania wa kawaida hadi tukaunge foleni pale wizara ya afya[ukifika unaambiwa kuna wenzako 500 mbeele yako wanasubiri kwenda ...]..,ila kwa wastaafu imeanishwa kabisa check up once a year,na kwenda matembezi if am not mistaken twice a year[total safari zinazolipiwa na serikali kwa mwaka ni tatu-fuull budgeted and paid]....kama hatutaki tubadili sheria ...ya mafao ya viongozi!!!

its true kuwa jk anafuja pesa kuliko kuingiza ndio maana amemaliza akiba yote ya nchi!...

Hiyo sheria waliyowekewa na wapambe wao? Uwezo wa kubadili sheria hatuna lakini wa kulalamika tunao. Hata hiyo mnataka kutuzuia? Yaani hata hiki kiduchu kilichopo mnataka mle bila hata kupigiwa kelele? Iko kazi.

Hawa unaowaita wastaafu ni watu wenye uwezo. Hawa walituomba kura zetu ili watutumikie. Tukawarudhia kwa matumaini kuwa watatufikisha mahali pema zaidi. Sasa huko hawakutufikisha halafu to add salt to injury mnatubeza kuwa wanastahili haya mafao kwa vile walitutumikia! Mafao ambayo nayo yanatokana na kodi zetu! Kwa nini sasa tusiulize? Sisi ambao wake zetu, binti zetu, mama zetu wanakufa kwa kukosa mkunga? Mbona hamtutakii mema?

Amandla......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom