Sumaye: CCM kaa chonjo

Kwa hili la Sumaye kugombea uenyekiti kanda, kaonyesha ukomavu wa hali ya kuwa yuko tayari kuwatumikia wananchi Kwa karibu zaidi. Kumbuka hata Mwl Nyerere aliwahi kujiudhulu/zulu vyeo vikubwa na kuchagua vyeo vya chini ili aweze kutumikia wananchi kwa karibu!
 
Chama kilichoshindwa kinakaria maneno ya kwenye taarabu,Magufuli hamjui sumaye vizuri,akitaka kumjua ajiulize jinsi atakavyozuia wanaccm kutoa rushwa nyakati za kura ya maoni ndani na kisha nyakati za kampeni.

Ccm ni rushwa na polisi,bila bk3 za kila mpigakura hakuna kura

Nikifikiria mihemko ya ccm nachooka kabisa,
Twendeni viwanjani mnahofu nn?
 
Haaaahaaa.. Kutoka kugombea Uraisi hadi kugombea Uenyekiti wa Chama...


Kweli ktk Maisha kuna rise and fall.... By the way Chadema mjifunze kuandaa viongozi sio kutegemea kutoka ccm


Sumaye na Lowasa wametoka CCM kutokana na hasira tu. Hasira zikiisha wanarudi CCM hao
 
Aliyewadanganya kuwa ukiwa mwanachama wa chadema ndio kujitambua ni nani??

Tangu lini Chadema imekuwa kipimo cha mtu kujitambua??

Kweli chama ambacho kinabadilisha gia angani na kuuzwa hovyo , hakina hata ofisi kwa miaka 20 ,ndio kiwe kipimo cha MTU kujielewa??

Bavicha kuna haja ya kupima bongo zenu, huenda mnamtindio wa ubongo.
 
Waziri mkuu mstaafu na mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Fredrick Sumaye ameitaka CCM kukaa chonjo kwani Chadema imedhamiria kutwaa dola mwaka 2020 na haitishwi na porojo za chama hicho hicho kinachoonyesha wazi kufilisika.

Sumaye amesema anayo kazi moja tu ya kukitumikia Chadema na kukieneza kuanzia vitongojini na wala hashtushwi na watu wanaomsakama kwani wanaonyesha hofu kubwa waliyo nayo kwake.

Sumaye alizungumza kwa kifupi sana wakati anaingia ndani ya kikao cha Kamati Kuu Chadema kutokana na swali aliloulizwa na mwandishi kuhusu jina lake kuwa kama agenda kwenye mkutano mkuu wa CCM leo.

Jina la Sumaye lilitawala ndani ya mkutano mkuu huo ambaye alitajwa sana kwa kejeli na viongozi kadhaa waliopata nafasi ya kuzungumza ndani ya mkutano huo.

Hiyo ni kuashiria Waziri mkuu huyo mstaafu ni kati ya watu wanaoitia kiwewe CCM.
Ulushawahi kuna WAP wazri....juu anagombania cheo cha udiwani ....dah hii njaa hatar sana...yaani from uwari ..kuu hadi kugombania ...hahahahhaaaa
 
Ulushawahi kuna WAP wazri....juu anagombania cheo cha udiwani ....dah hii njaa hatar sana...yaani from uwari ..kuu hadi kugombania ...hahahahhaaaa
Ukimaliza kushangaa pia jiulize kama ni rahisi mtu kutoka kuwa Naibu Katibu mkuu UN na kisha kwenda kuwa Balozi
 
Tangu ccm iasisiwe 1977, wananchi wake wameenelea kukabiliwa na ujinga,umaskini,magonjwa,ukosefu Wa madawati,nyumba za walimu,barabara mbovu,hakuna soko la wakulima LA uhakika,hakuna ajira"

M/ kiti mpya Wa ccm
Hivi watu hawajiongezi kuwa ccm imefeli na sera zake?
 
Watanzania tumetawaliwa na unafiki mkubwa sana. Kwanza kitendo cha Kikwete kwenda kwenye mkutano mkuu wa chama chake na kuzungumzia Sumaye na Lowasa ni UNAFIKI NA KUFILISIKA kisiasa na hata kiuongozi. Hiyo maana yake ni kwamba hotuba iliyotayarishwa iliwekwa Yale majina, kwa faida gani kwa Watanzania? Mtu aliyekaa Ikulu kwa miaka kumi na aliyekuwa mwenyekiti wa chama miaka kumi, halafu anamalizia kwa kutoa vijembe ni kukosa uvumilivu, kutawaliwa na umbea na unafiki ktk maisha. Lakini pili, Sumaye na Lowasa sasa ni wanachama wa Chadema, wao kushika wadhifa wowote ni wajibu na haki yao kama wanachama. Suala la kwàmba mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kushika madaraka ya chama ngazi za kawaida kuonekana ni kushuka thamani ni matokeo ya fikra mgando tulizolishwa na tunazoendelea kulishwa na Ccm. Na huo ndiyo UNAFIKI wa wanaccm. Mbona Urusi Putin alishika Urais, akarudi kwenye Uwaziri Mkuu na kisha Urais tenà? Na kwa nini kukaa unamfikiria mtu aliyekwisha kuondoka kwenye chama chenu? Taifa linabaki kushuhudia unafiki kwa watu walioaminiwa na wananchi na kucheza vigodoro tu kama kwamba dunia inatusubiri. Tunavaa mamitumba kwa sababu ya unafiki wenu viongozi, na kamwe hatutakaa tufanikiwe kupata maendeleo.


Wewe pia MNAFIKI MKUBWA NA UMEFILISIKA kisiasa..
yarudie maneno yako kinyume nyume ujione ulivyosheheni unafiki...
 
Back
Top Bottom